Mastaa wa Bongo Wasusia Arobaini ya Marehemu George Tyson



Jamani! Katika hali ya kushangaza, mastaa wa filamu Bongo wamesusia kumbukumbu ya siku 40 ya aliyekuwa muongozaji maarufu wa filamu nchini, George Otieno ‘Tyson’ aliyefariki dunia kwa ajali Mei 31, mwaka huu.

Shughuli ya 40 ya Tyson ilifanyika Alhamisi iliyopita nyumbani kwa aliyekuwa mkewe, Beatrice Shayo maeneo ya Sinza-Mapambano, Dar ambapo mastaa mbalimbali walialikwa lakini hakuonekana hata mmoja hali iliyosababisha chakula na futari iliyokuwa imeandaliwa kubaki huku wasanii wa vikundi waliohudhuria wakirudia mara mbilimbili.

Akizungumza na gazeti hili, Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba aliyekuwa kwenye shughuli hiyo alisema anashangaa mastaa wa filamu kukacha ishu hiyo kwani alimpa taarifa Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Nyerere’ kwamba awaambie wahudhurie.

“Nimewaalika wasanii wote lakini hakuna aliyekuja hata mmoja, ukweli wasanii hatuna ushirikiano kwani Tyson ndiye mwanamapinduzi aliyeigeuza sanaa kutoka kwenye kuuza sura hadi kuwa biashara hivyo walipaswa kumpa heshima yake,” alisema Mwakifwamba.
GPL

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad