MATESO! Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark Productions inayoendesha shindano la kusaka vipaji vya muziki, Bongo Star Search (BSS), Rita Paulsen ‘Madam’ amesimulia mateso aliyopitia takriban mwaka sasa (siku 365) baada kuvunjika mguu mwaka jana alipopata ajali ya gari katikati ya Jiji la Dar.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwenye mahojiano maalum hivi karibuni aliponaswa na gongo linalomsaidia kutembea, Madam Rita alisema kwa kusikitisha kwamba, baada ya kupata ajali alitibiwa kwenye Hospitali ya Muhimbili lakini madaktari walimwambia aliteguka tu kumbe alikuwa amevunjika mfupa.
“Nimepitia mateso makubwa. Mwaka jana baada ya kupata ajali na kuvunjika mguu nilipopelekwa Muhimbili waliniambia nimeteguka tu, na wakaamua kunifunga hogo ambalo baadaye walinifungua na kuniambia nimepona,” alisimulia Madam Rita na kuongeza:
“Baada ya pale nilianza kujiachia hata niliposikia maumivu na kuwaambia walisema niukanyagie tu kwamba hali hiyo ingebadilika kwa sababu ulielekea kupona, kumbe nilikuwa nimevunjika kabisa mfupa na kama ningejua siku nyingi hata nisingejiumiza kiasi hicho.
“Ujue baada ya kuambiwa hivyo, nilishangaa kuona maumivu yanazidi, nikaamua kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kuuangalia zaidi mguu wangu kwa sababu maumivu yalikuwa yakiongezeka kila siku.
“Nilikwenda kwenye Hospitali ya Morning Site ya Afrika Kusini ambapo nilifanyiwa upasuaji na kugundulika nilivunjika mfupa na kwamba tayari nilipokuwa nikitembea ilikuwa ikipandiana.
“Ona sasa nilivyoteswa na mguu huu maana ajali nilipata mwaka jana na huu upasuaji nimefanyiwa mwaka huu Afrika Kusini.
“Naona bora pale Fame Centre (Dar) maana wao waligundua tatizo na kunishauri kwenda Sauzi ambapo nimefanyiwa upasuaji na mguu unaelekea kupona kwa sababu mwanzo nilikuwa natumia magongo mawili lakini ona leo ninajikongoja kwa gongo moja ambalo nalo si muhimu sana sasa.”
Pole sana Madam Rita Paulsen. Ndio utu uzima huo. Vumilia tu utafika kwani huwa majaribu ni mengi. Sali sana na umjulie Muumba wako kwani yeye ndio muweza wa yote.
ReplyDeleteEhh unakufa hvhv au unakuwa kilema hvhv nchi hii kizembe tu.haya angekuwa hanahela ya kwenda sauz.madaktari nini nyie mbona mmezidisha uzembe hatakama siwote mnaboa.
ReplyDeleteNdio Akomae na Jiji. Ndio mpango mzima. Mtu mzima hovyo. Unateguka halafu kabla hujapona vizuri unajirusha.....utashangaaa.....
ReplyDeleteAfadhali ulikuwa na uwezo wa kwenda sauzi ungekuwa mlala hoi kilema ungekipata madaktari wa bongo hamna kitu ni wa first aid tu kwingine tunamuachia MUNGU
ReplyDeleteHivi Dr. Shabani wa mifupa MOI yupo? jamani hata kwa mkataba wakulipwa pesa zaidi wangekuwa wanawarudisha madaktari wazuri na waliobobea kulikoni kuwaacha wanaenda kufanya kazi nchi za nje! Wazuri wapo ila ni wachache mno, hawa wapya hawana experience ya kutosha wakati mwingine wanashindwa na kwa nini wasiseme uwezo wetu umeishia hapa!then wakushauri ukatibiwe nje ya nchi kama unaweza kulikoni kusema uongo kulikoni na kuwaharibia watu maisha hivhivi. Nimendika hayo kwa sababu kuna ndugu yangu alipata tatizo na kupewa majibu kama ya dada Rita na kwamba hana tatizo kumbe ana tatizo kubwa tu, alijua hivyo baada ya kutibiwa kwingine. Mungu ibariki Tz na watu wake.
ReplyDeleteanapenda wanaume wenye hela usikute washaluambukiza mingwesu,wanaume matajiri wanaumwa!!!!full desseas
ReplyDeletePole Madam maisha ni ups and downs
ReplyDelete