Baada ya jana kushuhudia kalamu ya magoli kwenye mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la dunia kati ya Brazil na Ujerumani, leo hii imepigwa nisu fainali ya pili kati ya Argentina na Uholanzi.
Matokeo ya mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Sao Paolo ni ushindi uliotokana na mikwaju ya penati wa 4-2 kwa Argentina.
Mechi hiyo ilikuwa ya kukamiana na kucheza kwa kujihami kwa timu zote mbili iliisha kwa sare tasa katika dakika 120 na hivyo ikaamuriwa ipigwe mikwaju ya penati.
Waliopata penati kwa Argentina ni Messi, Aguero, Garay, na Rodriguez wakati Robben na Dirk Kuyt wakifunga penati mbili za uholanzi huku Vlaar na Sneijder wakikosa.
Argentina sasa itaenda kucheza na Ujerumani fainali jumapili hii, wakati Uholanzi wakikutana na Brazil jumamosi kugombea medalinya mshindi wa 3.
Quote of The Day:
I hope everyone that is reading this is having a really good day. And if you are not, just know that in every new minute that passes you have an opportunity to change that.
gd 4argentina.kimbembe fainal
ReplyDeletesafi xana algentina komaeni mnusuru bara la america. imekaa poa xana hiyo.
ReplyDelete