Mchungaji Mtikila Amfunguliwa Kesi Askofu Mokiwa Kwa Kumshika Makalio

Mchungaji Christopher Mtikila amefungua kesi katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kumshitaki Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglican Tanzania Dk. Valentino Mokiwa.
Msingi wa kesi ni kwamba Askofu Mokiwa alimshika makalio Mtikila na kwamba kitendo hicho kilichotokea Juni 25 mwaka jana walipokutana maeneo ya Ilala, kimemdhalilisha.
Mtikila alikuwa ameitwa na Askofu kujadili tamko la la Mtikila kwamba Kanisa la Anglican linajihusisha na ufisadi, ukiwemo wizi wa vifaa vya Hospitali ya Mission ya Millo iliyoko Ludewa mkoani Njombe.
Mtikila alivyoitwa na Askofu Mokiwa ili kujadili hilo alifika na wenzake watatu wa taasisi ya Liberty International Foundation na wakakaribishwa kwenye moja ya jengo la dayosisi ya St. Nicholous, usiku wa saa 03:00.
Muda mfupi baada ya kikao kuanza, Askofu Mokiwa ambaye alikuwa na wenzake saba, alisimama na kuwataka wajumbe wote wakaguliwe kama kuna mtu ana kinasa sauti. Baadae Askofu Mokiwa nae alisimama na kuungana na wenzie kuwakagua kina Mtikila baada ya kuhakikisha mlango umefungwa.
Katika upekuzi huo ndipo tuhuma hizo zilipopatikana kutokana na madai kwamba operesheni hiyo ilienda mbali zaidi ya lengo la kawaida.
Wakili wa Upande wa mashtska aliiambia mahakama kuwa, "Mlalamikiwa alitangaza kuwa, kila mtu aliyekuwemo kwenye mkutano lazima apekuliwe na kwamba atakayekataa angetumia nguvu, kwa kuwa alikuwa na bastola, hakuna aliyebisha."
Alisema kisha akaendelea "Mshtakiwa (Mokiwa) alianza kupenyeza mikono yake kwenye shingo kuelekea chini kisha huko chini mikono ya mlalamikiwa ilionekana waziwazi ikipapasa makalio ya mlalamikaji".
Mchungaji Mtikila ameiomba Mahakama imwamuru Askofu Mokiwa alipe fidia ya shs. bilioni moja kwa kumdhalilisha.
Madhara zaidi ya kitendo hicho ni pamoja na mfadhaiko, masikitiko, wasiwasi, aibu katika jamii na kupata shinikizao la damu la mara kwa mara na matatizo ya moyo kila anapokumbuka kitendo hicho.
Kesi inasikilizwa kwenye Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, chini ya Hakimu Agness Mchome.

Quote of the Day:
Believe in yourself! Have faith in your abilities! Without a humble but reasonable confidence in your own powers you cannot be successful or happy.

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hahahahahahh kuna jambo hapo si makalio tu. endeleeni kutuweka wazi, muda si mrefu tutasikia kuna mtu alilawitiwa...

    ReplyDelete
  2. Tanzania tunamhitaji Mungu sana..

    ReplyDelete
  3. Hivi hili kanisa la Anglikana si ndio huwa kuna maaskofu wanaoliwa na wanaowala wenzao kiboga "mashoga"?

    ReplyDelete
  4. Hahaha hahaaaaa ........napita tu wakuu

    ReplyDelete
  5. Aisee kweli dunia imeisha, kama wazee wetu wanafanya vitu vya ajabu kiasi hiki vijana c ndo itakuwa balaa

    ReplyDelete
  6. Mmhhh hii ni zaidi ya hatare

    ReplyDelete
  7. Na bado utackia kashinda kesi..

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad