Wimbo wa Basi Nenda wa msanii kutoka Mwanza, Mo Music kwa haraka haraka ni moja kati ya nyimbo tatu bora zaidi za wasanii wapya kwenye mkondo mkubwa wa muziki uliofanya vizuri zaidi mwaka huu.
Hata hivyo wimbo huo ulianza kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na WhatsApp hata kabla haujapata nafasi kwenye radio na TV hadi sasa una mzunguko mkubwa na kumuwezesha Mo Music kufanya shows nyingi akizunguka Tanzania.
Mo Music ameiambia The Chart ya 100.5 Times Fm kuwa wimbo huo ulikuwa wimbo wa majaribio kwao na kwamba hakufikiria kama ungekuwa mkubwa kiasi hiki ingawa mashairi na melody zilimpa picha nzuri awali.
“Nilikuwa naimani kwamba message, melody pamoja na vitu nilivyotengeneza nilkuwa naimani hii ingekuwa kubwa, lakini sio kwa ukubwa huo uliotokea kwa sasa hivi. Lakini kitu kikubwa nachoweza kusema ni kwamba hii Basi Nenda ilikuwa nyimbo ya Majaribio. Kwamba hii nyimbo ilikuwa plan B, kwamba tunaijaribisha hii nyimbo halafu inayokuja ndio itakuwa nyimbo inayotoka.” Mo Music ameiambia The Chart ya 100.5 Times Fm.
Amewata mashabiki wake wausubirie ujio wake mwingine na wasiwe na wasiwasi kwa kuwa kinachokuja ni kikubwa zaidi.