Mr Nice Afunguka Kuhusu Utajiri Wake wa Bilioni 1.5 na Jinsi Ulivyotoweka Ghafla

Mr.Nice akifunguka kuhusu utajiri wake ulivyotoweka ghafla!. Katika hali yakushangaza, Lucas Mkenda au maarufu kama Mr.Nice, finaly afunguka kuhusu utajiri wake na sababu za kushuka kwake kimuziki, katika moja ya interview.

Mr.Nice alidai kuwa hajui ni nini haswa kilichotokea ila yote hayo ni mipango tu ya Mungu. Mr.nice alizidi kufunguka na kusema kuwa, alikuwa na jumla ya zaidi ya shilingi bilioni 1.5 zote zikiwa katika account mbalimbali hapa nchini, na hela zote hizo zimetoweka katika kipindi cha muda mfupi bila yeye kujua zimetumikaje.

“Kaka naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu, kwani sikuwahi kumdhulumu mtu wala kuiba cha mtu, pesa yote nilikuwa naipata kwa hali, naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu wala si mkono wa mtu” alisema Mr.Nice.

“Niliwahi kumiliki zaidi ya milioni elfu moja na mia tano kwenye bank tofauti hapa nchini, pesa hizo zilitokana na kufanya shoo nyingi za nje ya nchi kama. Marekani,Uingereza, Ujerumani, Sweden, Holand, Dubai, SouthAfrica na kwingineko, na kila shoo nilikuwa napata pesa ndefu sana” 

Alimalizia star huyo kutoka Tzee na mwanzilishi wa staili ya TAKEU.


Mbali na kushuka kwake kimuziki Mr.Nice anakiri kuwa ana-miss sana enzi hizo kwenye show zake zisizoweza kusahaulika na machozi huwa yanamtoka kila akumbukapo show aliyopiga nchini Rwanda.

Ambapo hadi waziri wa nchini humo aliweza kumsubiria airport kumpokea tena kwenye red carpet huku akisindikizwa na magari ya polisi, pamoja na mashabiki wake lukuki waliojaza uwanja huo wa ndege kushuhudia ujio wake.

Quote of The Day:
Thousands of candles can be lighted from a single candle, and the life of the candle will not be shortened. Happiness never decreases by being shared.

Post a Comment

18 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Still u have a time bro! Don't loose hope wakati bado uhai na una nguvu!

    ReplyDelete
  2. Thubutuuuu! labda auze unga.

    ReplyDelete
  3. Malipo,ulinyanyasa sana wadada wewe,omba Mungu akurudishe kwa njia nyingine,lakini muziki Ni kwishneh

    ReplyDelete
  4. Mkipata ela huwa mnajisahau Sana wanawake Na nyinyi starehe nyie mnatala mjulikane mtaa nzima haraf hamfanyi vitu vya maana hata nyumba huna nasikini ya mungu, nakuonaga hapo AIKA au PK unang'ang'a sharubu bia moja masaa 7,kwajinc ulivyokuwa staa haraf bado unaishi pale kwenu kwenye kile kijijumba pole lazima ulie coz ulichezea bahat, Na bahat hairyd Mara 2.

    ReplyDelete
  5. HUWEKUIJUA NEEMA ULIYONAYO MPAKA SIKU ITAKAPOONDOKA. mfano siku ukipata maradhi ndio utajua umuhmu wa hiyo afya uliyonayo. Pole sana bwana SASAMBU.!

    ReplyDelete
  6. HUWEZI KUIJUA NEEMA ULIYONAYO MPAKA SIKU ITAKAPOONDOKA. mfano siku ukipata maradhi ndio utajua umuhmu wa hiyo afya uliyonayo. Pole sana bwana SASAMBU.!

    ReplyDelete
  7. Tusubiri Dimond naye kuja kujuta

    ReplyDelete
  8. Bora diamond ananyumba kadhaa mjini hata akichuja hawez kuwa Kama mr nice, lazima ela atakuwa nazo za kubadilishia mboga

    ReplyDelete
  9. sasa hizo pesa zote sasa nani ataamini zilikuwa zikiexist kiukweli

    ReplyDelete
  10. huu ujumbe umfikie domo maana anahisi ye ndo wa kwanza tz kumbe wengi tu washapita bado na yeye awapishe wenzake

    ReplyDelete
  11. huu ujumbe umfikie domo maana anahisi ye ndo wa kwanza tz kumbe wengi tu washapita bado na yeye awapishe wenzake

    ReplyDelete
  12. Kila mtu Ana zamu Yake ya kushine,sasa Hivi Ni Damond .

    ReplyDelete
  13. Kutesa kwa zamu

    ReplyDelete
  14. Labda aokote pochi ya mzungu wa Geita mgodini,hahahaaaa kurudi chat Nice ni ndoto!

    ReplyDelete
  15. Wote Mnao mponda Domo(dimond) kawivu kanawauma..
    DImond tuko juu kwa sasa...! Eti mnasubiri naye afulie...achen hzo!

    ReplyDelete
  16. Waache 2 watasubir xana na ndokwanza anapasuwa mbingu,yule Mtoto anaakili Tofaut na 9ic,Mr 9ic nilikuwa namuangalia 2 wakat ule anakuja magomen bar ya machen wakt uwo kwa machen machen kweli kulikuwa 9ic alikuwa anakuja na msafara kula mbushii tena starehe mpk saa 1 asubuh w2 wanaenda makazin yey yupo bar,kweli akili ya binadamu eti wadau?

    ReplyDelete
  17. mipango ya mungu??? mkipata hela mnajisau mnajifanya kila kitu ndo nyie..malisha maisha club nzima..unadhani ela zinajiongeza ukitumia?? the more u spend the more u loose.. kaskilize tena wimbo wa ladyjaydee historia..

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad