Msajili: Mbowe, Dk Slaa Hawana Sifa Kugombea Uongozi Tena Chadema Baada ya Kipengele cha Ukomo wa Uongozi Kuondolewa Kinyemela

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imesema  Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa hawana sifa za kugombea tena uongozi wa chama hicho kwa kuwa wanabanwa na katiba yao.

Akizungumza jana ofisini kwake baada ya kuzungumza na Mbowe, Msajili Msaidizi, Sisty Nyahoza alisema walipata malalamiko na kuyafanyia kazi, ikiwa ni pamoja na kupitia kumbukumbu walizonazo na kubaini kuwa kipengele cha ukomo wa uongozi kiliondolewa kinyemela katika katiba ya chama hicho.

Alisema kwa kawaida vyama vyote vinapofanya mikutano huwapelekea muhtasari, hivyo Chadema nacho kiliwapelekea kumbukumbu ya Mkutano Mkuu wa mwaka 2006, lakini hakuna sehemu yoyote iliyoondoa ukomo wa uongozi.

“Hivyo, hawa tayari wana vipindi viwili, wakichaguliwa katika uchaguzi unaokuja hatutawatambua. Wakitaka wabadili katiba kwa njia halali ambayo ni ya mkutano mkuu na si vinginevyo,” alisema.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Mbowe alisema hakuwa tayari kulizungumzia, akieleza kwamba amefika kwenye ofisi hiyo ya Msajili kwa masuala mengine.

“ Siwezi kulizungumzia suala hilo kwa sasa, likifikishwa kwenye Kamati Kuu ndipo nitalielezea,” alisema Mbowe.

Baadaye Ofisa wa Habari wa Chadema, Tumaini Makene alisema kwamba Msajili alimwita Mbowe ili kumshawishi asaidie wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) warejee katika Bunge la Katiba.

“Mwenyekiti alibainisha kuwa msimamo wa Ukawa upo wazi kwamba hawatarudi katika Bunge hilo hadi pale maoni ya wananchi yatakapoanza kujadiliwa na msimamo huo hautabadilika,” alisema Makene akimkariri Mbowe.

Makene alisema baada ya kutoa msimamo huo, hakuna maongezi mengine yaliyoendelea baina ya Mbowe na Msajili.

Alipoulizwa iwapo Msajili alionyesha nia pia ya kuushawishi upande wa pili wanaotaka serikali mbili, Makene alisema hawezi kufahamu, japo kwa nafasi yake, Mutungi ana uwezo wa kufanya hivyo.

Alipoulizwa iwapo Msajili pia alizungumzia suala la ukomo wa uongozi linalodaiwa kubadilishwa kinyemela, alisema: “Kuhusu hilo Chadema tunafuatilia kwa kina taarifa zinazozagaa zikionyesha correspondence (barua) zinazotoka kwa Msajili wa Vyama juu ya Chadema na tutakapokamilisha tutatoa taarifa.”

Gazeti hili jana lilichapisha taarifa iliyonukuu barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chadema, ikieleza kuwa kipengele hicho katika Ibara ya 6.3.2 (C) kiliondolewa kwenye katiba bila idhini ya mkutano mkuu wa chama hicho.

Jaji Mutungi alisisitiza kuwa mkuu wa chama hicho ndiye wenye mamlaka ya kurekebisha katiba, hivyo baada ya kupitia muhtasari wa Mkutano Mkuu wa mwaka 2006 suala la kuondoa kipengele cha ukomo wa uongozi halikuonyesha kujadiliwa katika mkutano huo.

Hata hivyo, akizungumza kwa simu juzi, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema kipengele hicho kiliondolewa kwa vikao vya chama ambavyo ni wilaya na mkoa.

Hoja hiyo iliwasilishwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na ambaye sasa si mwanachama wa chama hicho
Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Msajili huyu wa vyama ameanza kuvaa viatu vya ' lile zee la hovyo' babu john tendwa.Kumbe sifa moja kuu ya kuupata usajili wa vyama ni kiapo cha kuishughulikia chadema?Hakika francis nakuahidi hutaweza kushindana na nguvu ya umma,tuachie chadema yetu na ww endelea na ccm yako.

    ReplyDelete
  2. Mbona Vituko didhi ya chadema haviishaji? Ccm imeifanya chadema kama mke mwenza.Kete zao zote za ukabila,udini,ubadhirifu,ugaidi,zitto na vibaraka wenzake zimefeli vibaya,mbona ccm hawajifunzi kuwa chadema ni mpango wa mungu na hawataiweza?

    ReplyDelete
    Replies
    1. acha uongo wewe mchaga na chama chako cha chadema nenda zako na chama chenu cha ukabila

      Delete
  3. Chadema wataishia kupiga domoo tu,kuitawala hii nchi ni ndotto za alinacha.

    ReplyDelete
  4. Kisharu ndikampojo uko sahihi kabisa,hawa jamaa wanatakiwa waonyeshe ukomavu wa Demokrasia kwenye chama chao.kama msajili piga chini hawa watu wawili chama si mali yao binafsi.

    ReplyDelete
  5. kama kweli analosema msajili kuhusu kubadilishwa kinyemela katiba ya CHADEMA ? ovyo kweli

    ReplyDelete
  6. ni kweli hakuna katiba isiyo na ukomo wa kugombea inamaana atagombea mpaka miaka hamsini si itakuwa kama kingunge halafu agombee urais wapi na wapi ataweza hiyo mikiki ya urasi si atakufa mapema

    ReplyDelete
  7. katiba ilibadilishwa na mgombea ataweza kuendelea kama atahitajika na baraza kuu la chama, tatizo nyie sisieeem matumbo joto, Mbowe ni kiboko yenu, na Mungu tubariki upenzani uingie IKULU.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad