Mtangazaji Mwingine wa Clouds FM Anyakuliwa na BBC Idhaa ya Kiswahili

Anyway I saw This coming :Kijana Anorld Kayanda Aliyekuwa Mtangazaji wa Clouds FM Kipindi cha Jahazi Sasa Yupo BBC Swahili :
Hivi Ndivyo Alivyoandika kwenye Ukurasa wake wa Facebook
"Watu hawa (wengine hawapo pichani) walinipokea vizuri hadi nikaogopa pengine wameshanitafutia mteja wanasubiri nilale waniuze. Hii ni familia yangu mpya. Shukrani sana Dada Liz Massinga, John Solombi, Dada Halima Nyanza, Leonard Mubali, Dada Regina Mwalekwa, Hassan Mhelela, Dada Regina Joseph, Ben Mwang'onda, David Eric Nampesya, Baruan Muhuza na wengine wote. Mungu ameshanifikisha nchi ya ahadi kilichobaki ni kumtumikia. Sasa vijana waambie vijana wenzenu nao wawaambie wenzao katika ratiba zao watenge muda wa kuisikiliza Idhaa ya Kiswahili ya #BBC." Anorld Kayanda

Quote of The Day:
Don't judge each day by the harvest you reap but by the seeds that you plant.

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Yule aliyebora ataonekana tu na kunyakuliwa na wanaojua kutambua mtangazaji bora ni nani na kuwaacha wale ambao ni bora watangazaji. Aliyebora anaonekana tu hata akiwa ndani ya clouds na media nyingine, bungeni toka chama chote; viongozi wa timu za mpira, viongozi wa dini; Watanzania tuache kununuliwa na kuachagu kibovu na kuacha kilichobora kama WAMBURA alivyoenguliwa asigombee urais wa SIMBA SPORTS CLUB.

    ReplyDelete
  2. Yule aliyebora ataonekana tu na kunyakuliwa na wanaojua kutambua mtangazaji bora ni nani na kuwaacha wale ambao ni bora watangazaji. Aliyebora anaonekana tu hata akiwa ndani ya clouds na media nyingine, bungeni toka chama chote; viongozi wa timu za mpira, viongozi wa dini; Watanzania tuache kununuliwa na kuachagu kibovu na kuacha kilichobora kama WAMBURA alivyoenguliwa asigombee urais wa SIMBA SPORTS CLUB.

    ReplyDelete
  3. Nchi ya ahadi.hongera

    ReplyDelete
  4. Kibonde vipi haonekani tu jamani.au yeye amebaki tu kushobokea chama tawala na kwenyewe hata hawamuoni?!tatizo la watangazaji wetu wanahongeka kirahisi sana na kusahau taaluma yao na namna ya kubalance habari/taarifa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hana nidhamu bhana,

      Delete
    2. ndiyo anaongea kihunihuni sana,tofauti na umri wake

      Delete
  5. Hongera sana! Piga kazi

    ReplyDelete
  6. Namuombea Mungu Millard Ayo naye afike nchi ya ahadi

    ReplyDelete
  7. its true, Millard Ayo nchi ya ahadi ikukumbuke na wewe unastahili. Hongera kaka Anold Kayanda chapa kazi nakutakia kila la kheri Mungu akutangulie.

    ReplyDelete
  8. kaeni tayari kumpokea Millard Ayo nae ( mtu wa watu ).tunamuombea.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad