Mtuhumiwa wa kesi ya kujeruhi kwa kumng’ata sehemu mbalimbali za mwili mfanyakazi wa ndani, inayomkabili Amina Maige (42) amepatiwa dhamana jana baada ya mahakama kuthibitisha kuwa hasira kutoka kwa wananchi zimepungua.
Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Yohana Yongolo alisema ameridhishwa na ufafanuzi uliotolewa na Mwendesha mashitaka wa Serikali pamoja na Wakili wa mshitakiwa kuwa haki ya dhamana itolewe kwa kufuata masharti na kwamba hakuna uhalifu wowote utakaofanyika dhidi ya mshitakiwa huyo.
Hakimu Yongolo alitoa masharti ya dhamana ambayo yalimtaka Maige kutoondoka nje ya Dar es salaam bila ya ruhusa ya mahakama hiyo.
Pia alitoa masharti ya kuwa na wadhamini wawili wa kuaminiwa kutoka taasisi inayotambulika hapa nchini ambapo mdhamini huyo anaweza kuwa mwajiriwa, mfanya biashara na mkulima.
Alisema wadhamini hao watatakiwa kusaini hati ya makubaliano kwa kila mmoja kulipa Sh milioni tatu.
Aliongeza kuwa kesi hiyo itasikilizwa Julai 22 mwaka huu.
Maige alidaiwa Januari mwaka jana hadi Juni mwaka huu, alimng’ata na kumchoma na pasi sehemu mbalimbali za mwili wa mfanyakazi waje wa ndani Yusta Kashinde (20) na kumsababishia maumivu mwilini.
nikimkuta ktk angazangu ntamlamba vibao kazaa...
ReplyDeletekweli huyu anahitaji kichapo anajiona kashashinda hii kesi.
ReplyDeleteLabda ajifiche chamoto atakiona
ReplyDelete