Nape Kudhihaki Wanasiasa Wenzake kwa Kutumia Uzee Wao Sio Maadili ya Kiafrika Jitazame Upya!


Kila mara nyingi sasa nimemsikia Nape Nnauye katibu wa propaganda, itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi akidhihaki wanasiasa wa upinzani kwa uzee wao. Malengo yake ukiyachambua yamelenga kuwaaminisha wafuasi wa chama chake kwamba uzee dalili ya udhaifu na si lolote ktk utumishi wa kisiasa... Amediriki kuwaita mpaka majina kama Babu, wazee wanazeeka vibaya nk. Hivi ndani ya ccm, wazee wanajisikiaje kuona uzee ukitumika kama silibo na mbinu ya kueneza propaganda? Je, taifa lianze kuwaita wazee kama Mangula,salimu,kingunge nk majina anayotaka Nape. Sasa vijana wa ccm tuanze kuwaita wazee wetu majina kama, Babu mkapa,babu Mangula, babu wasira, babu Lowasa, babu Sitta, Babu kikwete, Babu Karume, Babu msuya nk?..... Jamani hata kama ni propaganda ya kuwabomoa wapinzani tusitumie utu wa binadamu kisiasa....mimi ninao wazee ktk uko nawaheshimu,nawaheshimu wazee wote bila kujali itikadi....wapinzani tupingane nao kwa hoja sio utu wao. Nasikitika Uvccm nao tumeambukizwa upuuzi huu! Nani kakwambia kutukana uzee ni turufu na ngazi ya kupandia kisiasa? Hio laaana! Nape kama huna mzee kwenu tafadhali sana wenye kujua thamani ya uzee utuache!....MWL NYERERE alithamini wazee kamwe hakuwahi kudhihaki uzee....uzee sio ugonjwa na ujana sio utakatifu..

Quote of the Day:
Believe in yourself! Have faith in your abilities! Without a humble but reasonable confidence in your own powers you cannot be successful or happy.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ah tushachoka nae huyu mpaka mikorogo

    ReplyDelete
  2. Hiyo ni age discrimination na pia ni form of harassment. Sijui ni Chama gani kinaweza ku tolerate ujinga kama huo. Katika Nchi yeyote ya kistaarabu ni kosa ku discriminate watu kwa sababu ya umri wao. Mbona yeye anapaka lipstick mdomoni na watu tumekauka???

    ReplyDelete
  3. mtoto huyo mpenda..........

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad