Ndege Nyingine ya Malaysia Yaanguka Ikiwa na Watu 295

Ndege ya Malaysia, Boeing 777 iliyokuwa inatoka Amsterdam kwenda Kula Lumpur imeanguka Mashariki mwa Ukraine karibu kabisa na mpaka wa Russia, leo, July 18.

Kwa mujibu wa CNN, waziri wa Malaysia anaehusika na mauala ya Usafirishaji amesema kuwa abiria 280 na wafanyakazi 15 waliokuwa kwenye ndege hiyo wamepoteza maisha.

Tweet ya Malaysia Airlines imeeleza kuwa ndege hiyo ilipoteza mawasiliano baada ya kutoka Amsterdam.

Kumekuwa na taarifa za awali kuwa ndege hiyo ilipigwa na na Ukraine, taarifa ambazo zimekanushwa na raisi wa Ukraine.

Rais wa Malaysia ameeleza kupitia twitter jinsi alivyosikitishwa na tukio hilo na kudai kuwa wataanza uchunguzi wa tukio hilo haraka iwezekanavyo kufahamu chanzo.

Tukio hili linatokea wakati ambapo bado ndege ya nchi hiyo, Flight 370 iliyopotea March 8 Mwaka huu bado haijapatikana.

Quote of the Day:
Believe in yourself! Have faith in your abilities! Without a humble but reasonable confidence in your own powers you cannot be successful or happy.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. INNA LILLAH WAINA ILLAH RAJIUN
    MUNGU AZIWEKE MAHALI PEMA ROHO ZA WATU WALOTANGULIA BILA HATIA
    NA ALLAH AWAPE SUBIRA WOTE WALOPOTELEWA NA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI.

    ReplyDelete
  2. Naamini hizi ni sadaka haiwezekan kampuni ya malaysia airline abiria wanapotea.kwa wng na tn kwa mazingira ya kutatanisha

    ReplyDelete
  3. Hao hawaja potea bali ndenge imeanguka au ujui kusoma hapo juu wameandika nn.Mola awalaze mahala pema na awape subra kwa wafiwa wote ameen

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad