Neymar amekutana na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza tangu aliporuhusiwa kutoka hospitalini ambapo alikuwa akipatiwa matibabu ya kufuatia jeraha la mgongo ambalo liliwashtua mashabiki wengi wanaozifuatilia fainali za kombe la dunia.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amesema alikuwa hatarini kupoza, kutokana na kubainika wazi kwamba endapo Juan Zuniga angemjeruhi sentimita chache kwenda chini angepata kilema cha maisha.
Mshambuliaji huyo aliyefunga mabao manne kabla ya kuumia wakati wa mchezo wa hatua ya robo fainali dhidi ya Colombia, pia amesema beki wa The Coffers, Juan Zuniga amempigia simu na kumuomba radhi kwa kumfanyia rafu mgongoni kwenye mchezo huo.
Wakati akizungumzia suala hilo Neymar akijikuta akibugujikwa na machozi
"Zuniga alinipigia simu siku chache baadaye kuniomba msamaha na kuniambia kwamba hakudhamiria kuniumiza," amesema Neymar. "Nimeukubali msamaha huu, lakini siwezi kulichukulia lile kama tukio la kawaida. Siwezi hata kusema lilikuwa tukio la makusudi, lakini kila mmoja anafahamu haikuwa kawaida. Namna alivyokuja, nyuma yangu, nisingeweza kujitetea.
"Namshukuru Mungu kanisaidia, kwa sababu kama pigo lile lingezama ndani kwa inch chache, ningeweza kupooza,"amesema Neymar huku akibubujikwa na machozi.
Neymar amesema hajui nini tatizo hadi Brazil ikafungwa 7-1 katika mchezo wa hatua ya nusu fainali na Ujerumani.
"Kilichotokea hakikutarajiwa. Lakini hata walipokuwa nyuma kwa 6-0, 7-0, hawakukata tamaa, waliendelea kukimbia, kuendelea kujaribu.
Sioni aibu kuwa Mbrazil, sioni aibu kuwa sehemu ya timu hii.
Ninajivunia kila mmoja katika wachezaji wenzangu,"amesema.
Quote of The Day:
Happiness is not something you postpone for the future; it is something you design for the present.
pole neymar
ReplyDeletepole sana neymar ndio mchezo msaheme tu
ReplyDeleteNdio Ukubwa huo. Na bado. Hiyo ni miaka 22 tu. Bado hujafika 40 ujioneee. Kumanyoko zako.
ReplyDeleteumekosa ustaarabu kabisa,kichwa mchwa wewe.
DeleteTriste, obtendra' as' Neymar
ReplyDelete