Mimi na watanzania wenzangu tunasikitishwa sana na kauli za kujirudia rudia za Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe akitumbukiza Tanzania katika LAANA. Mara hii Membe ananukuliwa na Vyombo vya Habari akilaani ISRAELI kwa mauaji yanayoendelea huko Gaza.
Mimi binafsi nimefuatilia vyanzo vingi vya Habari kuhusu yanayoendela Gaza, na haya ndiyo mambo 6 niliyojifunza:
Hamas inayoongoza Gaza ndio walianzisha misuguano hii kwa kuwateka vijana watatu wa Israeli na kasha kuwaua. Kitendo hiki kilipongezwa sana na Hamas huko Gaza, kuashiria palikuwa na mahusiano ya moja kwa moja kati ya watekaji na chama hiki cha Hamass.
Hamas walikuwa wakirusha roketi kuelekea miji ya Israeli bila kujali yatawaua raia au la, kitendo ambacho ni cha uchokozi.
Israeli inatumia teknolojia kubwa sana kuyaharibu maroketi hayaya Hamas kwa kutumia IRON DOME SYSTEM kabla hayajaleta madhara yoyote. Ndiyo maana hadi sasa, hakuna muisraeli hata mmoja ameuliwa na roketi hizi zaidi ya 1,000 zilizorushwa na Hamas hadi sasa.
Hamas haitambui uwepo wa Israeli. Kwa maana nyingine, Hamas katika ILANI yao, wameapa kuwafurukusha Israel wasiwepo kabisa eneo lote la Mashariki ya Kati.
Hamas wanahamasisha raia wa Gaza wasiondoke maeneo yale hatarishi ili watumike kama ngao ya kibinadamu (human shield) wakidhani Israeli itawaacha warushe tu roketi,
Israeli inatumia njia za kisayansi kuwatumia watu wa Gaza meseji kwenye simu zao kuwatahadharisha wasiende maeneo yanayotarajiwa kupigwa mabomu. Hili ni jambo la kistaarabu sana, huwezi kulitarajia wakati wa vita. Ubishi wa tahadhari kama hizi ndio umepeleka raia wa Gaza kudhuriwa na mashambulizi ya Israeli.
Baada ya maelezo hapo juu, tujiulize kama Taifa, Je, Membe alitaka Israeli wakirushiwa maroketi na Hamas wakae kimya wasiyajibu? Membe ukiwa Waziri wa Mambo ya Nje, upo tayari kuona miji ya Dar es Salaam au Dodoma ikirushiwa maroketi na nchi jirani, na Tanzania tukaae kimya tu kwa sababu Tanzania ikijibu inaweza kuua raia wa hiyo nchi ya jirani chokozi?
Waziri Membe umeonesha udhaifu mkubwa ulio nao katika tasnia ya diplomasia za kimataifa na mambo ya nje kwa kutojua historia ya mgogoro huu, na kitendo chako cha kuegemea upande mmoja ni cha aibu na fedheha kwa wizara unayoongoza. Miaka ya nyuma uliwahi pia kunukuliwa ukilaani Israeli pale ulipoalikwa kama mgeni wa siku ya Palestina katika Ubalozi wao hapa Dar es Salaam.
Waziri Membe tunakuhakikishia kuwa, kiitendo chako cha kuilaani Israeli hakiwezi kupita kimya bila kupingwa na Watanzania. Umelaani Israeli lakini laana yako ikurudie wewe mwenyewe na familia yako. Ni aibu kubwa kwa mtu kama wewe unayetamani kuongoza ofisi kubwa kuliko zote hapa Tanzania (IKULU) unatamka maneno ya laana hata kabla hujapewa ofisi.
Imeandikwa, HESABU 23: 8 “Nimlaanije, yeye ambaye Mungu hakumlaani? Nimshutumuje, yeye ambaye Bwana hakumshutumu?” , Ni wazi kuwa Anayelaani ISRAELI naye ANALAANIWA. Anayebariki ISRAELI naye ANABARIKIWA. Tunamshukuru Mungu kwa kutuonesha Moyo ulio nao ili waakati wako wa kugombea urais ukifika tukuweke kwenye jalala la milele. Waziri Membe Umetegwa kwa maneno ya kinywa chako mwenyewe.
By proisra via JF
Quote of the Day
You are always a student, never a master. You have to keep moving forward.
SEMA MIMI SIO WATANZANIA WOTE WAPO PAMOJA NA WEWE
ReplyDeletemwandishi wa hii post BICHWA EMPTY
ReplyDeletemwandishi wa hii post BICHWA EMPTY
ReplyDeletelaana hii haitakuja Tanzania ng'o iende kwa Membe na familia yake na ukoo wake.amen!!
ReplyDeleteTena arekebishe maneno yake si wa Tz wote ni mtazamo wake mimi si surpot israel kwa kuua innocent chidren na wote wasio na hatia Ahsante muheshimiwa Membe
ReplyDeleteIsraeli wamebarikiwa ww ni nani uwalaani? Mimi nawabariki Israel, Amen!!
ReplyDeleteAmen
DeleteNi kweli Israel wamebarikiwa kwa kuwa na "mikono ya damu" maana walimuua hadi mungu wao Yesu.
Deleteunajuä sana kuwajibu wajinga, wapumbav na wafuata mkumbo. Hao walimuu hadi mungu wao tena muisraeli mwenzao hawana mana kabisa hao jamaa na kuhusu laana walaaniwe mara ngapi.
DeleteMungu awasamehe maana hujui unalojibu kwa Taifa Teule La ISRAEL, ushangai why Nato, us wanakaa kimya na yanayoendelea. Usamehewe bure
Delete''Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumuhisi baba yangu,naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?Yatatimizwaje basi maandiko ya kwamba hivyo ndivyo vilivyopasa kujiri?"KWA HIYO HAPO WANDUGU ILIKUWA ILI YATIMIE YALIYOANDIKWA"
DeleteUmenigusaje! haleluya.
DeleteMembe unajua kweli unachoongea? ni kwa nini uroho wa madaraka ukufikishe mahali ambapo si pema? sifurahii mauaji yanayotokea ila kamwe siwezi kuilaani ISRAEL! hiyo laana iwe juu yako na kizazi chako mwenyewe.
ReplyDeleteMtoahoja hii hajuwi pia maana ya diplomasia. Membe hawezi kutoa kauli nzito kama hii bila kushauriana na mkuu wa nchi pamoja na mamlaka zingine muhimu za nchi. Kauli hii ni ya nchi, hivyo kama huipendi hama nchi. Halikadhalika, hata Umoja wa Mataifa na mataifa mengine makubwa duniani yamelaani mashambulizi haya ya Israel dhidi ya Gaza. Watu pekee wasiweza kuishutumu Israel ni mashetani wenzao Marekani. Kuhusu uhalali wa Israel kushambulia Gaza, ni wazi mtoahoja hafahamu mambo. Dunia nzima inafahamu kuwa Israel inaikalia kwa mabavu ardhi ya Gaza. Mgogoro huu ni mkongwe na hata Umoja wa Mataifa ulishapitisha maazimio lukuki kuitaka Israel iondoke katika ukanda wa Gaza kwa sababu inakaa kwa mabavu. Hivyo, vyovyote iwavyo, wavamizi hapa ni Israel na Hamas wanapigania ardhi yao.
ReplyDeletehivi kule kwenu Kimbiji wakija watu kuvamia na kuchukua ardhi yenu watakua wamebarikiwa?
ReplyDeleteTena laana iwashukie kwa ushenzi wao....licha y ardhi walioikalia kwa mabavu lkn haiwatoshi wanataka n Gaza.tena kwa kuua maelfu y watu. wasio n hatia.......
ReplyDeleteHao wadau wanaoiunga mkono israel walaaniwe wote,walaaaniwe waisraeli woooote
ReplyDeleteIMEANDIKWA.
Delete..Kweli imeandikwa.. kama hujui kitu bora ukae kimya. ofcoz awalaaniea Israel atalaaniwa .kwa ushauri piga kimya pita ivi
DeleteAsante ndugu,pia ubalozi wa Israel kutokuwepo nchini ni tatizo kubwa lililopo baina ya sisi na israel,viongozi wapo wapi ?
ReplyDeletealietoa hii post hajui alitendalo and analeta mambo ya kisiasa na mgawanyiko wa chama jitambua pichwa rungu.
ReplyDeleteYoyotte anaesapot isirael alaaniwe.na piaatakua ameshiriki kumuua muguwao,mtu aliemkana mungu anakuaje mtakatifu? Hebu tembeeni isirael kwa sasa simbali mwendemkajue ukweli, ndiomana ckuhizi kunamadhehebu makubwa watuwanazidi kutoka kwasababu yakujua ukweli, ulifika isirael ukirudi kuwezikuepotenakwahilo zehbi, nendeni,wacheni kubishana,mbona wenzenu kila mwaka wanaenda kwao?.
ReplyDeleteEwe mwenyezimungu waangamize wote wanaomuabudu mwingine badala yako wewe bila kuwa sahau wote wanaoabudu miti ya surplus iliyochongwa sanamu ya Yesu ikiwa na nepi tu mwilini kwake, Ameen.
ReplyDeleteHao waisrael walaani wamekalia nchi ya wapalestina kwa mabavu jerusalem yote ilikua mali ya wapalestina waisrael wakaichukua kwa mabavu wakawaachia saiv wanaitaka na gaza tena kwa kumwaga damu za watoto wazee walemavu n.k alafu wewe mtoa mada unatetea wewe ndio unafata mkumbo soma historia nan mmiliki halali wa ardh ukanda wa gaza mbulula wewe
ReplyDeletemwandishi huyu taahira kabisa! big up membe
ReplyDeletewatu wamemuua hadi mungu wao yesu alafu mna wachekea? Eti membe amekosea? amekosea wapi? unajua majukum ya membe wewe? Membe ameongea ukweli mtupu,na mimi na watanzania wote tuna laani mauaji haya vikali!
ReplyDeleteWaswahili wanasema kila baa na paka wake na kila masika na mbu wake. Huyu aliyeandika mada hii ndiyo zuzu wa zama hizi. Tanzania kupitia Membe imelaani tu mauaji haya haramu ya raia wasioweza kujitetet wa Gaza. Lakini mtu mwenye akili zake anaponda. Nchini Afrika Kusini chama cha wafanyakaji wa viwanda vya chuma (National Union of Metalworkers of South Africa - NUMSA) kinaishinikiza serikali ya nchi kumtimua balozi wa Israel kutokana na mauaji haya. Sasa huyu zuzu mawazo ya kumwona Membe kakosea anayatoa wapi? Diplomasia hii ameisomea wapi?
ReplyDeleteMTOA HOJA CHOKO
ReplyDeleteTaifa liliobarikia na maandiko yanatimia.Amen
ReplyDelete..Huyu mwandishi anafaa sana kuwa mwamuzi wa taifa letu,, big up sana.ukweli ndo utabaki palepale Isue serius za Mambo ya nje haifai kwa watu wenye mawazo kama ya Membe na washauri wake so lazima laana iwapate wao na matokeo mtayaona..
ReplyDelete