Pati za Kajala za Kila Siku Zazua Jambo, Sidhani Kama Fedha za Sinema Zinaweza Kumpa Jeuri Hiyo

Na Musa Mateja
MAKUBWA! Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ameangusha pati nchini China kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na kuibua minong’ono juu ya chanzo cha jeuri hiyo ya fedha.

Kufuru hiyo ya fedha ilianzia jijini Dar katika bethidei ya mwanaye (Paula) hivi karibuni ambapo awali alikwenda kutoa misaada ya vitu mbalimbali katika Shule ya Sinza Maalum kisha kuangusha bonge la sherehe katika Hoteli ya Sea Cliff.

Baada ya vurugu hizo ambazo kimsingi zilidaiwa kuteketeza milioni kadhaa, siku chache baadaye (Julai 22, mwaka huu), kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, Kajala alitupia picha za sherehe yake ya kuzaliwa aliyoifanyia nchini China katika Mgahawa wa Waitaly uliyopo Guahnzu.

Chanzo kilichokuwepo katika sherehe hiyo kilisema, Kajala aliwaalika marafiki zake kibao wa nchini humo akiwemo mpenzi wake wa zamani, Petty Man ambapo walikula na kunywa kwa bili yake kitu ambacho wengi walihoji kuhusiana na alikozipata fedha hizo.

“Mh! Si bure kuna kitu, kufanya sherehe katika nchi za watu kama hivi si kitu kidogo lazima uwe na fedha za maana sasa hatujui mwenzetu ameitoa wapi hii jeuri,” alihoji mualikwa mmoja kupitia mitandao ya kijamii.

Kama hiyo haitoshi, shuhuda mwingine aliyechati na mwanahabari wetu alikwenda mbali zaidi kwa kuhoji juu ya kazi zake na pato analoingiza kupitia sinema.

“Nimefuatilia tangu alipoanza kuzitumbua fedha akiwa Bongo hadi huku China, sidhani kama fedha za sinema zinaweza kumpa jeuri hii, kutakuwa na mtu nyuma yake tu,” alisema shuhuda huyo ambaye hakutaka kuchorwa jina gazetini.
GPL

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. iv nyie watu me naona hamna cha kufanya mjue.....mlitaka akale kwa mama yenu au awaombe pesa? kapata mnasema akikosa mnasema mnataka aishije? nyoooooo****************kajala wamalize ikiwezekana dondosha nyingine

    ReplyDelete
  2. Kazi ya diamond hiyoo chezeya diamond weeee

    ReplyDelete
  3. we kumaa kweli diamond anahusika nini na kajala unataka kusema anamtia kajala ndo amana anampa mipesa au kuku kweli wewe

    ReplyDelete
  4. Kuku km kidogo tena kuku mdondo diamond ndiyo nani watakufira na diamond kila kitu diamomg

    ReplyDelete
  5. sisi yetu macho,tuangalie tuu mambo yanavyokwenda,yatakuja kujulikana baadaye wakishakamatwa na mzigo,wanaume wanaoishi china wengi wanauza madawa,sasa awe makini,tamaa mbele mauti nyuma,maana sasa hivi nawasikia watu wake wameshaanza kumwita bossy,

    ReplyDelete
  6. Fuck u kajala

    ReplyDelete
  7. Looooooooooooooo! innahu fanyayako dada.

    ReplyDelete
  8. ndio siku hizi Kajala anaitwa boss na mashoga zake,ana hela chafuuuuuuuu sijui kazipata wapi ghafla ghafla hivi yaani.mmmmh,tusubiri yatajulikana kama ya jack cliff,kumrudishia hela wema kajala kagoma,

    ReplyDelete
  9. Amrudishie wema hela kwani alikuomba, si kihere here cha wema, kwanza na yeye sio zake za CK

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad