Ripoti: Wasichana waliotekwa na Boko Haram hubakwa wakichukuliwa video

Wasichana zaidi ya 200 wa Chibok waliotekwa na kundi la Boko Haram wanadaiwa kuwa katika hali mbaya na ya kutisha zaidi senator wa jimbo la Borno anasema hufanyiwa vitendo vya kinyama kupita maelezo.

Akifanya mahojiano na kituo cha runinga cha Sahara TV, Senator Khalifa Ahmed Zanna wa Borno Central amesema amepata ripoti mpya kuwa wasichana hao waliotekwa siku zaidi ya 70 zilizopita hubakwa na wafuasi wa kundi hilo huku wakichukuliwa video ambayo baadae huoneshwa hadharani.

Senator huyo ameeleza kuwa ingawa hakushuhudia video hiyo lakini mtu aliyemsimulia matukio hayo alikuwa na video hiyo na alieleza kuwa msichana akimaliza kubakwa hupiga magoti mbele ya mbakaji na kumuomba amhurumie.

“Therefore the girl after being raped, she curled down to the man, kneeling down and begging him to please be patient. So disturbing. And although I didn’t see the video, the person narrated to me, he said he had the video, and he was narrating to me, and look at the situation.” Amesema Senator Khalifa.

Amesema mbali na wasichana hao waliotekwa, kundi hilo limewakamata wanawake zaidi ya 500 wanaokutwa barabarani au vijijini.

Mbali na tukio hilo la kinyama, amesema ripoti aliyopewa inaonesha kuwa kundi hilo hivi sasa halina chakula cha kutoshwa hivyo linaingia vijijini na kuwanyang’anya wanakijiji chakula walichonacho huku wakifanya matukio ya kinyama.

Kufuatiak matukio hayo wanakijiji wengi wamekimbia makazi yao na kuhamia mijini bila kujua hatima yao huku wengine wakiingia kwenye nchi za jirani.

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. boko haram sio waislam wa kweli ni wanafiki na ndio mana wan ajiita haram ni wana haram kweli.....m.mungu awalaani

    ReplyDelete
  2. boko haramu c waislam ni makafiri wanaoupakazia uisilamu,matendo yao hayafanani na hatamoja ya maadili ya uisilamu, hiyo ni mipango ya watu fulani katika kuukashifu uislamu, na M/Mungu atawalaani na kuulinda uisilamu INSHAALLAH.

    ReplyDelete
  3. Taarifa hii ni ya kutengeneza yan uongo(falsehood propaganda) eti nimeambiwa(ushahidi wa kuambiwa hauna mashko) wanabakwa kwa zamu,huu ni uongo uliokomaa!

    ReplyDelete
  4. Taarifa hii ni ya kutengeneza yan uongo(falsehood propaganda) eti nimeambiwa(ushahidi wa kuambiwa hauna mashko) wanabakwa kwa zamu,huu ni uongo uliokomaa!

    ReplyDelete
  5. admin acha usenge ce n watu wazima tunaopitia hii site af co wote ni wapumbav ka wewe

    ReplyDelete
  6. anaesema boko haram si waislam nani? vip alshababu? seleka je? taliban? alqaida? hamas?janjaweed nk yapo makundi zaid ya 100 ya kiislam na kaz yao ndo kama ya bokoharam..kwani jihad ni ya nini kama sio kuua watu waso na hatia? kuna haja ya dini ya kiislam kubadili sheria zenu

    ReplyDelete
  7. boka haramu maana yake ni (BOKO ni elimu inayotoleawa mashulen yaan formal education...! na HARAM maana yake ni haramu kwamba ni kitu kisicho faa) boko haram wenyewe wanataka elimu ya quran ndy itumike katika shughuli zote za kijamii ikiwemo shule lugha ya kufundishia iwe kiarafu pamoja na lugha ya kawaida. hyo ndy maana halisi ya boko haram

    ReplyDelete
  8. Ww mdau hapo juu qur ani yenyewe inaamrisha watu kusoma elimu ya kidunia na akhera, sasa hawa boko haramu na makundi mengine wanaopinga elimu ya kidunia hii sheria wameitoa kwa nani kwa maana uislamu hauwakubali hao boko na makundi mengineo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad