Wakati wananchi wengi wakifikiri kuwa NHC inakua, inaendelea inatanuka, inashamiri na kupendeza lakini mambo sivyo yalivyo.
NHC ni bomu litalolipuka ndani ya miaka miwili hadi mitano, kama hayatafanyika mabadiliko ya kimsingi katika strategy, approach na focus, kutoka hii ya sasa.
Wakati mchechu akipata sifa kupitia visibility ya physical infrastructure, financially shirika halina hata mia. Miradi mikubwa waliyoifanya haifanikiwi kama wanavyotarajia huku riba za mabenk zikiwa palepale.
Malengo ya NHC hayaendani na ukweli halisi wa maisha ya watanzania ambao ndo walengwa wa miradi yao. Kwa mfano nyumba za vyumba viwili zilizoko kigamboni zilimlenga kijana aliyemaliza chuo na kuanza kazi, kijana asiye na familia. Nyumba hizi zinauzwa kati ya 50 Mil hadi 75 Mil bila kodi na riba. Kijana gani aliyeanza kazi ataweza kulipa pesa hizo? kwa mshahara gani??
Kukurupuka huku kwa Mchechu kumesababisha NHC kujenga miradi mingi tena kwa mkopo lakini response ya watanzania ni ndogo na haiendani na mategemeo yao. Hii inamaanisha NHC watashindwa kurejesha mikopo yao ndani ya wakati , Jambo litalosababisha mabank kuhodhi miradi hii.
Kwa wataalamu wa costing, Mabank yanamwingiza choo cha kike mchechu, na kimsingi shirika hili litafilisiwa hapo baadaye. Just a simple financial forecasting analysis will tel you this.
Kwa watazamaji wa nje, majumba haya na miradi hii wataona ni mafanikio ndani ya muda mfupi, lakini JE nini kinaendelea baada ya hapo.
Mpaka sasa MERU residance Arusha kuna apartment ziko empty, na ni mradi wenye zaidi za miaka miwili sasa( MAJANGA).
Mchechu's ambitions does not reflect the tanzania economy, he is way far from the reality, na hii inakuja kuiua NHC.
Source:Jamii Forums
point...noted miradi haiendani na watanzania
ReplyDeletehamna lolote, ni fisadi moja limetoa hela kwa huyu admn aandike utumbo huu kumchafua tu mchechu, tanajua hilo, hizi nyumba zitawasaidia wengi
ReplyDeleteMikoani lazima response itakuwa slow kwa hizo nyumba. Hio ni shauri ya mfumo wa serikali kuwekeza miundo mbinu na
ReplyDeleteVitega uchumi vingi dar es salaam na kuinyima miji mingine mzunguko stahili wa Pesa. Sio kosa la mchechu hilo.
watanzania tuache midomo tutapotea , mchechu ni zawadi kutoka kwa mungu .
ReplyDeletemidomo yetu ilimuondoa keenja jiji , tujiulize nini kimefanyika baada ya keenja kuundoka ? zaidi ya usanii na fedha kupotea
kuna wakubwa wanataka kumuondoa mchechu kwa maslahi yao binafsi
ReplyDeletetuwe macho watanzania , mchechu akiondoka wakubwa watagawana nyumba
zote za NHC , tutabaki tunalialia kama kawaida yetu
Kama una akili timamu and you have a very small knowledge of Tanzania economy....bas utajua kuwa nyumba za NHC haziendani na hali halisi ya watanzania alichokifanya mchechu sio kigeni wala muujiza watu kama yeye wapo wengi tu TBC alikuwepo Tido leo hayupo tunaye Mshana na shirika linasonga mbele...strategy ya Mchechu imefeli nyumba hizo ni expensive sana zile za dodoma medeli apartment nazo zimemdodea mwaka wa tatu huu....za kinondoni anazojenga hivi sasa anatumia gharama sana kuzitangaza kwa miradi yoote ya shirika la nyumba ambayo ni ya kitaifa inapaswa kuwa cheap na ya kusaidia wananchi...mtu anaepingana na ukweli huu basi atakuwa amebarikiwa na mungu kuwa na kipato kizuri cha kuweza kumudu gharama hizo ndio maana hawezi kuelewa anapoambiwa kuwa kuna watu hawana milioni 90 za kununua nyumba ambazo mchechu anadai ni za bei ya chini...Nawakilisha
ReplyDeleteMdau hapo juu. Ushawahi jenga nyumba..? Do you know anything about ujenzi ?.ulitaka hizo nyumba ziuzwe bei gani? Let me tell you something.Gharama za ujenzi ,VAT na kodi za serikali katika vifaa vya ujenzi
DeleteNdio vinavyofanya gharama za hizo nyumba zinakuwa kubwa.
Mchechu has nothing to do with that.
Keep that for your record
Mdau USA
we hapo juu ukapimwe , mshana kuna kitu anafanya ?
ReplyDeletetbc siyo mfano mzuri wa kutoa huna unachojua
wanaomchukia mchechu ni wengi , ni wale waliotaka wapewe nyumba
ReplyDeleteza nhc kama zawadi kwa sababu tu wanaishi ndani ya nyumba hizo ,
waondoke na wengine wapate matunda ya uhuru , watu wana vitukuu ndani
ya hizo nyumba wameganda kama KUPE