Siyo Bure Diamond Platnumz Kwa Hili Utakuwa Umelaaniwa, Huwezi Kumfanyia Baba Yako Hivyo

Stori: Erick Evarist na Gladness Mallya
Oooh! Nooh! Wakati akimpa mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’ gari la Sh. milioni 38 huku akitawanya mamilioni ya fedha kwenye matukio mbalimbali, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anadaiwa kunyemelewa na laana kufuatia baba yake, Abdul Jumaa kuugua na kuvimba miguu bila msaada wowote.


Kwa mujibu wa chanzo makini cha Ijumaa, baba wa staa huyo anayeishi Magomeni-Kagera jijini Dar, amekuwa akisumbuliwa na tatizo la kuvimba miguu na hakuna msaada wowote anaoupata kwani chanzo cha mapato anachokitegemea ni kodi tu ya nyumba ambayo anaipata kutoka kwa wapangaji wachache alionao.

BOFYA HAPA
“Yaani tunashangaa kusikia Diamond ana fedha nyingi, juzikati tuliona katika gazeti kamnunulia mama yake gari la milioni 38 (Toyota Lexus-Harrier) sasa kwa nini asimthamini baba yake hata kidogo? 
“Ukweli ni kwamba baba Diamond anasumbuliwa na tatizo la miguu kuvimba.

“Amekuwa akilalamika mara kwa mara lakini Diamond hatujawahi kumuona,” kilinyetisha chanzo hicho na kuongeza:“Juzikati hapa baba Diamond alishikika kwelikweli miguu, akaugulia mwenyewe ndani pasipo kuwa na msaada wowote tena nasikia mzee huyo hataki hata kuongelea lolote kuhusu Diamond maana haoni umuhimu wa kufanya hivyo wakati amemsusa muda mrefu sana.”

MATIBABU HAYAZIDI MILIONI
Katika aya nyingine, chanzo hicho kilidai kwamba ugonjwa wa miguu ambao unamsumbua mzazi huyo, gharama za matibabu haziwezi kufikia hata shilingi milioni moja za madafu achilia mbali mamilioni anayoyatapanya staa huyo.

“Ingekuwa tatizo kubwa sana, hapo sawa, kwa sababu miguu huwa inamvimba lakini akipata dawa za kutumia huwa inarudi katika hali ya kawaida, kwa nini lakini anamfanyia hivyo baba yake? Amemkosea nini?” Kilihoji chanzo hicho.

UTAJIRI WAKE WAANIKWA
Wakati chanzo hicho kikiweka nukta hapo kwa muda, mapaparazi wetu walipewa malalamiko mengine kutoka kwa jirani mmoja wa baba Diamond ambaye alimsihi amsaidie mzazi wake kwani anaamini uwezo anao kupitia kumbukumbu ambazo Diamond mwenyewe alizithibitisha kupitia vipindi mbalimbali vya runingani kama Take One na Spora Show vya CloudsTV.

Pia kwenye vyombo vingine vya habari zikiwemo redio na magazeti pendwa ya Global Publishers.
Jirani huyo alidai kwamba mwaka jana Diamond alitangaza kuwa ana utajiri wa Sh. bilioni moja ikiaminika kwamba mwaka huu umeongezeka mara dufu.

“Nakumbuka mwaka jana kupitia Kipindi cha Spora Show na kile cha Take One, Diamond alikiri kuwa ana mkwanja usiopungua bilioni moja, hiyo ilikuwa kwa mwaka jana, sasa mwaka huu unadhani atakuwa na shilingi ngapi? Aache hizo bwana, amsaidie baba yake hata kwa kumpa mtaji mdogo wa biashara ambao unaweza kumsaidia,” alisema jirani huyo.

MATANUZI YA DIAMOND, WEMA
Katika kuendelea kuichimba habari hiyo, mapaparazi wetu walinasa malalamiko kutoka kwa jirani mwingine wa mzazi huyo ambaye alieleza masikitiko yake kwa kulinganisha starehe ambazo staa huyo anazifanya na asali wake wa moyo, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu na maisha halisi ya baba yake.

“Mimi ni mfuatiliaji mzuri wa habari za mastaa, naona kila siku kwenye vyombo vya habari jinsi gani Wema na Diamond wanavyotumia fedha nyingi katika masuala ambayo hayana ulazima kiivyo.
“Sisi kama majirani hatupendezwi na hali hii, angekuwa anakuja angalau siku mojamoja kumuona baba yake kuliko kila siku kumhudumia mama yake pekee,” alisema jirani huyo.

TATIZO NI NINI?
Mapaparazi wetu waliingia mzigoni kusaka kiini halisi kwa nini Diamond amwage fedha nyingi kwa mama yake pasipo kumkumbuka japo kiduchu baba yake ambapo ilielezwa kuwa staa huyo wa Mdogomdogo hakuwa na ugomvi wowote na mzazi wake huyo.

“Kama ni ugomvi ulikuwepo kati ya mama na baba lakini Diamond hahusiki, tunashangaa kuona kama staa huyo naye anaweza kumsusia baba yake,” kilieleza chanzo na kuongeza:

“Mbaya zaidi nasikia Diamond amekuwa mzito kupokea simu za baba yake, sasa huoni kama siyo jambo la busara, mzazi ni mzazi tu hata iweje. Kwa mtazamo wangu kinachofuata ni laana.

“Kuna mifano ya watu wengi ambao waliingia kwenye laana za wazazi wao na wakajikuta kama siyo kufulia kama (wanatajwa mastaa waliofulia wa muziki Bongo) au hata kukutwa na umauti.
“Jambo hili si la kibinadamu tu, kwa wale wanaosoma vitabu vitakatifu watakuwa na mifano mingi ya watu waliowakosea wazazi wao wakalaaniwa.”

BABA DIAMOND ANASIKITISHA
Ijumaa lilipomtafuta baba Diamond kwa njia ya simu aliongea maneno ya kusikitisha huku akikataa katakata kumzungumzia kijana wake huyo.

“Jamani naomba mumuache Diamond na maisha yake, sitaki kabisa kusikia habari zake maana hata nikiongea naonekana najipendekeza kwake.

“Namshukuru Mungu, kama ni kuumwa kwa sasa naendelea vizuri na maisha yangu, niacheni nipumzike,” alisema mzee huyo kwa unyonge.

DIAMOND ANASEMAJE?
Alipotafutwa Diamond ili kumsikia anazungumziaje madai hayo, simu yake iliita bila kupokelewa. Tunaamini atasoma habari hii hivyo si vibaya akatutafuta ili afunguke kwa upande wake.

MAONI YA MHARIRI
Diamond ni staa mkubwa kwa sasa ndani na nje ya Bongo, uwezo alionao kifedha unapaswa kuendana na baraka za wazazi wa pande zote mbili. Vitabu vya Mungu vinatufundisha kwamba wazazi ndiyo Miungu wetu hapa duniani hivyo hata kama kuna kosa amefanya, mzazi atabaki kuwa mzazi tu. Hatutakiwi kumkosoa!

Quote of the Day:
Believe in yourself! Have faith in your abilities! Without a humble but reasonable confidence in your own powers you cannot be successful or happy.

Post a Comment

37 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. WEEEEE HAKUNA KITABU KINASEMA MZAZI NI MUNGU WA DUNIA LABDA HIII PAGE YAKOOO,,,,MUOGOPE MUNGU,,,,MTOA HABARI UTAPATA.LAAANA YA MUNGU

    ReplyDelete
  2. kila kitu kinatafuta sababu..sio mumloge then msingizie laana.Hamnaga laana

    ReplyDelete
  3. hakuna kosa linaloweza kuifuta thaman ya mzazi, wewe domo unamkosea mungu kila ck lakini mungu anaendelea kukujalia uzima na anakupa hivyo vyote ulivyo navyo, je wewe unaakili kuliko mungu?unakula hela na Malaya unamwacha babaako anahangaika eti alikutelekeza!!!! wewe unajema gani ulilomtendea mungu mpaka akupe vyote hivyo? afu eti umefunga !!!! mungu hachezewi namna hiyo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ulishaga wahi kukataliwa na mzazi wako ? Akakunyima malezi kama mwanae, Akakunyima elimu makusudi!! Mzazi ambae anaweza kumlaani mtoto na radhi ikashika...ni yule aliye timiza wajibu wake kama mzazi kwa mtoto. Baba Diamond...hayo ndio matokeo na malipo yako kwa kuwa mzazi ulie mtesa mwanao nakumnyima malezi.

      Delete
    2. I support

      Delete
  4. Namshauri Domo km kinachoongelewa ni cha kweli amsamehe mzazi wake na amhudumie,na mie nna kisa cha namna hii lakini nilimsamehe babaangu na nilimuuguza bahati mby Mungu alimchukua. Binadam ni kusameheana japokua maudhi ya hawa babazetu yanakera sana ukiyakimbuka. Jimtu linatelekeza familia kisa papuchi ya mwanamke mwingine,basi hata huduma kwa watoto hamna hajui mnakula nini,mnavaa nini,mwaishi wp na mnasoma vp. Baadae mnakua kwa juhudi za mama na Mungu wenye,mnafanikiwa kimaisha ndo jibaba hilo linaibuka oh mwanangu star,oh hanijali,oh cjui nini. Wewe ulipomtelekeza na pengine kumkana juu ulitegemea alelewe vp? What if Diamond angekua jambazi huyo babake angeibuka na kudai jamani hilo jambazi ni toto langu? C ameona dogo ana mkwanja ndo analalama,na hili ni fundisho kwa wazazi wa aina hii msipende kukwepa jukumu la malezi mkaliacha kwa kina mama mkipewa shit na watoto mjue mnastahili c kulalama mfyuuuuuxz!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kumsamehe mzazi wake kisha msamehe, na ndio maana diamond akafaanikiwa..sio lazima kumsaidia baba yake . Kwani huyo mzee alimsaidia nini diamond wakati kamleta duniani?????

      Delete
  5. Fundisho kwa mijidume mnamzalisha mwananamke mnamwacha anateseka na watoto, unadhani km huyo baba ana mpanga nyumba za kupangisha ina maana before alikuwa na maisha angalao kuliko mama wa Diamond? Huyo Diamond inaelekea amepitia machungu sana akiwa na mama yake huku baba yake akikataa angalao kumpa hata shilingi, huenda kuna kipindi alilala njaa huku baba akimnyima hata kumi ya mihogo.

    But all in all msamehe ili upate mema ya nchi. I can feel diamond's pain.

    ReplyDelete
  6. na wewe mpuuzi hapo juu we umejirekebisha nini kwa makosa unayo mkosea mungu?

    ReplyDelete
  7. Hata bibilia inasema apandacho mtu ndicho avunacho, wababa wengi ndivyo walivyo hata mimi baba angu mzazi alinikana na kukataa kunisomesha akidai mtoto wa kike nitaishia kupewa mimba, kwa neema ya mama yangu alikuwa ananifariji na kutia moyo ktk masomo. lkn bahat mbaya alifark nkiwa elimu ya sekondari.Nikasoma elimu ya juu kwa msaada wa ndugu licha ya huyo baba kuwa na uwezo wa kunisomesha.Leo hii nimepata kazi anaanza kulalamika ooh mtoto jeuri haniheshimu.Sasa je mzazi ka huyo utampa hata shilingi.Si bora ukasaidie yatima na watoto waliotelekezwa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kweli. Pole sana, ni wachahce sana wenye upeo wa kuelewa hili swala kiundani... I support

      Delete
  8. Hata bibilia inasema apandacho mtu ndicho avunacho, wababa wengi ndivyo walivyo hata mimi baba angu mzazi alinikana na kukataa kunisomesha akidai mtoto wa kike nitaishia kupewa mimba, kwa neema ya mama yangu alikuwa ananifariji na kutia moyo ktk masomo. lkn bahat mbaya alifark nkiwa elimu ya sekondari.Nikasoma elimu ya juu kwa msaada wa ndugu licha ya huyo baba kuwa na uwezo wa kunisomesha.Leo hii nimepata kazi anaanza kulalamika ooh mtoto jeuri haniheshimu.Sasa je mzazi ka huyo utampa hata shilingi.Si bora ukasaidie yatima na watoto waliotelekezwa.

    ReplyDelete
  9. Si alimkataa mwenyewe na kusema asikanyage kwake amepewa uchaw na mama ake ili amuue na akakataa kumlipia ada ya shule diamond alifikir asali siyo basi ajue mkuki kwa nguruwe na bado mbwa huyo mbona queen darleen pia mwanae na amlalamikii na mungu kampiga kofi la kushoto watoto wote aliowakataa wako na maisha mazuri.

    ReplyDelete
  10. WATEVA HAPPENS YULE NI BABAKO AM SPEAKING THIS THROUGH EXPERIANCE DIAMOND KI VOVOTE YULE NI MZAZI WAKO INGAWAJE LABDA ALIKUKOSEA WEWE MWACHIE MUNGU NDIO ATAKAYE MLIPIA. MADAMU UWEZO UNAO WEWE MSAAIDIE KAMA SI YEYE HII DUNIA HUNGEIONA. WEWE MSAAIDIE TU HAKUNA ZAIDI YA MUNGU. NA WEWE VEE CASH AKA NANA JUNIOUR UWA UPUUZI NDIO UMEZOWEA ONGEA GROW UP N BECOME LIKE A MATURED PERSON COZ U LOOK SO DAM STUPID.

    ReplyDelete
  11. kuna vitu zingine si vaku support jamani huyu nana joniar ndio vee cash utamwona akishabikia ujinga wa wema na dai za zingine.

    ReplyDelete
  12. kama Mungu anasamehe wewe nani usisamehe haijalishi alivyo kufanya yule bado ni baba yako. Wewe msaidie utapata malipo yako kwa Mungu. wewe vee cash uwa ni akilizako punguani ama ni ujinga umekunonga. ongea cha busara

    ReplyDelete
  13. kumbe vee cash ndiyo nana kila blog uyu dada yumo full matusi alafu anavyovojipendekeza kwa kuna wema hatar akiambiwa njoo uwe mbeva begi wabgu fasta atakwenda

    ReplyDelete
    Replies
    1. we mkundu mweusi unasema nini,,,,domo linbakuwasha unahamu yakunyonya boo...

      Delete
  14. hata kama alikukataa baba atabaki kuwa baba na thamani yake ya baba, wala hapana sababu ya kumsamehe wala nini kidini huyo ni baba yako na una haki ya kumshuhulikia ipasavyo ila tu mama utamshuhulikia mara tatu zaidi ya baba sio kumtenga unajukumu kama ni mtoto. ugomvi wa baba na mama waachie wenyewe, na baba nae ataulizwa kwa upande wake mbele ya haki juu ya malezi aliyokupatia. kama ni ushauri

    ReplyDelete
  15. jman mi cjui nani mkweli manake wandishi sometimes c wakweli ila ukweli ni kwamba ucmpilizie ubaya mzazi wake.fanya kama vile unavyowasaidia wengine, utazidishiwa

    ReplyDelete
  16. Mnapiga kelele bure anaeujua ukweli ni Dai na mama ake wamaisha Yao.sasa kama akiamua kumsaidia niyeye sio wewe useme.nawanaume mjifunze sio ukiona mtoto kafanikiwa ndio umfwate ukitaka msaada ukiyatupa we yatupe mazima sio mnasumbua watoto wakishafanikiwa.dai ukiamua kumsaidia nivizuri uamuzi niwako.asikushurutishe mtu.hakuna mwenyeroho ya Chuma hapa hata Dai namama ake waliumia sanakipindi chamsoto alisaidiwa nanani na bb ake alikuwa wapi.shilingi inakuwaga napande mbili ndiohivyo sasa kilasiku mifano ya wababa waliokataa watoto IPO ILA hawakomi.na mungu anawachapajee lazima ukae fimbo za mungu zinauma haya huyo Baba yukowapi sikakaaa sasa huyo ndio mungu fanya ushenz ikifika wakat utalipia ushenz Wako ndio kama hivyoo

    ReplyDelete
  17. Mimi nauliza kwa mnaoamini kuwa mungu yupo,mmemkosea mangapi mungu? na je ameacha kuwasaidia kwasababu mmemkosea? mbona mungu hawaachi bado yupo na ninyi? kama mungu angesema ukimkosea anakuacha nani angebakia, na nyie wanawake mnaoua watoto mungu kawafanyaje

    ReplyDelete
  18. Mwacheni mungu aitwe mungu.kunamtu dunia hii ni mungu km hamna basi ujue mwanasamu ni mwanadamu na mungu nimungu.siamlimtoa mwanae wapekee ilisie tupone.nawewe kamtoe basi mwanao wapekee afe kwa ajili yawatu wengine.ndiomaana unaweza ukasamehe ILA usisahau machungu ukilijua Hilo basi ukaeukijua huwezi mwanadamu ukawa namsamaha kama wa mungu.so kilamtu aishi kwakutenda wema.tupunguze unyama.msikatae watoto wenu badae muwatafute kwakuwa wanamaisha mazuri.kwani ulitumwa uzae kama huwezi kumlea?hlf useme mungu anasamehe ushasema mungu.cc ni wanadamu unasamehe lkn machungu huyasahau.

    ReplyDelete
  19. KWAKO DIAMOND,
    KUMBUKA BILA HUOY BABA YAKO WW USINGEKUWEPO HAPA DUNIA MBEGU ZA KIUME NDIZO ZILIZOKUFANYA UKAWEPO HAPA DUNIA,LIPA FADHILA ZA HIZO MBEGU ZAKE MENGINE MUACHE MOLA,NI KM MFANO WA BWANA SHAMBA ALIEPANDA MTI WA MATUNDA LAKINI HAKUUTUNZA,LIPA FADHILA ZA KUUPANDA MTI HUO...BABA HATABAI KUWA BABA YAKO TUUU
    MPE JAPO LAKI MOJA KWA MWEZI AU MSAIDIE BIASHARA HAJIENDESHEE MAISHA YEYE MWENYEWE,HAKIFA NA KINYONGO MAFANIKIO YAKO YATAINGIA DOSARI KWA KIASI FULANI
    NI HAYO TU.

    ReplyDelete
  20. WEWE VEE CASH MPUMBAVU SANA MATUSI NAFKIRI HIYO SIMU UMPEWA NA KINA WEMA MAANAKE DOH UNAVOJIPENDEKEZA NOMA NA WACHA KUTUKANA WENZIO STUPID IDIOL MONGER

    ReplyDelete
  21. ndio tabia za vee cash upumbavu tuuuu na matusi nafkiri hana la maana wala busara mtu mjinga mdomoni mwake hutoa matusi na mwenye busara huongea vya maana. tumechoka na matusi zako

    ReplyDelete
  22. Nakuunga mkono mdau 1:51pm

    ReplyDelete
  23. Achen usenge

    ReplyDelete
  24. Diamond nimesikia co Baba yake n Baba yake mlezi..alimchukua mama yake diamond akiwa na mimba ya diamond alilea mimba amabayo akutia yy mpk mtt kazaliwa ambauye ndo diamon mzee anamchango mkubwa ktk marezi ya diamond...ila kulitokea ugovi na kuachana Kati ya mama diamond na huyo mzee Abdul amabaye diamond anatumia Nina la ubin WA huyo mzee...leo diamond anashindwa kurudisha fadhila kwa huyo mzee kwa ugovi WA mama yake na huyo mzer

    ReplyDelete
    Replies
    1. Uongo mtupuuuuu Ni baba yake Wa damu.Mimi Ni ndugu Wa bi Sandra mama yake diamond.

      Delete
  25. jamni huyu admin afaa ampe onyo vee cash kwa sababu hutukana na kuna watu wazima huingia hapa ni heshima gani yani ulibadilisha jina ukidhani hatutokujua na matusi yake ni hayo hayo nana junior nkt

    ReplyDelete
  26. ahhhh kumbe vee cash ndio nana junior yule wa matusi loh kweli mdau umenena bora apewe onyo

    ReplyDelete
  27. wanaume mnatelekezaga sana watoto kwa mama zao mkidhani ni raha, mtoto anakua akiona mama yake anavyomhangaikia wakat huo baba anatanua tuu ,hiv unadhani mtoto haoni hayo yote? mnajua uchungu wa kutelekezewa mimba au mtoto,? mumuache diamond amuhangaikie aliyemuhangaikia kama ci mama yake kukazana asingekua hapo. hiyo ndo faida ya kukataa na kuwasusa watoto.

    ReplyDelete
  28. Huo ndo ukweli waambie 10:41 hawajui uchungu wa kutelekezewa mtoto

    ReplyDelete
  29. Jamani eeh Mwisho wa ubaya aibu. hamuwezi jua kiini cha ugomvi wa familia hii. na usiombe kitu kutelekezwa na baba. kina mama mara nyingi huwa kama kuku na vifaranga. mibaba mingi hua kama majogoo tu akishampanda temba hana mpango wa kujua keshataga yai la aina gani. akiona mafanikio ndo utaona jitu hilo ooh mie babake ooh sijui sie ndo shangazi zake tena mkome kama kuna mijitu ya aina hii. mi namsapoti sana Diamond. usimpe hata senti hilo libaba lililokutelekeza ila ukimkuta hana suruali nunua suruali na shati mpe kumsitiri. shwain kabisa mi napataga hasira kweli na miwanaume ya hivi.

    ReplyDelete
  30. dahh' kazi kweli kweli nan kama mama, wanaume cku hzi ndivyyo walivyo wantaka raha lakini kulea hawapotayari,

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad