Slaa: Rais Kikwete ana Rungu la Katiba Mpya Sio Maaskofu wala Taasisi

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amemtaka Rais Jakaya Kikwete kujitokeza hadharani kutafuta suluhu ya kupata mwafaka wa mchakato wa Katiba Mpya kwa kuwa hakuna mamlaka nyingine zaidi inayoweza kuunusuru.

Pia, amewatahadharisha viongozi wa dini kuwa makini na kauli zao wanazozitoa za kuwataka wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kurejea bungeni Agosti 5.

Dk Slaa aliyasema hayo juzi katika mahojiano maalumu na gazeti hili, makao makuu ya Chadema Mtaa wa Ufipa, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

“Mwenye rungu la kuweza kutengua kitendawili hiki ili turudi bungeni ni Rais (Kikwete) mwenyewe, hakuna mwingine,”alisema Dk Slaa.

“Tatizo aliyesaini waraka uliowasilishwa na Warioba ni Rais mwenyewe, alisaini ukurasa wa kwanza na wa mwisho, kwa taarifa rasmi za kina Warioba, Rais alishirikishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba hatua kwa hatua na kwa kila hatua alisema sawa mchakato uendelee,”alisema Dk Slaa.

Alikumbusha kuwa wakati akipokea Rasimu ya Pili ya Katiba, Rais Kikwete alisema: “Mtapata rasimu, ijadilini na itapitishwa na Bunge. Kwa mwanasheria yeyote, lugha kujadiliwa na kupitishwa haitoi ruhusa ya kubadilishwa, inatoa ruhusa kuboreshwa. Ndiyo utaratibu wa sheria zote duniani.”

“Sasa anapofika mahali anayeleta wazo ni Rais, lakini kwa bahati mbaya anayekwenda kupindua pia ni Rais na amekwenda mbali zaidi kiasi cha kusema kwamba kama Serikali tatu ile ile ambayo yeye ameisaini itapatikana, jeshi litapindua nchi.

“Anayezungumza ni Rais, hakuna mamlaka nyingine inayoweza kutengua kitendawili hiki. Wanaweza kuja maaskofu, ...masheikh, asasi mbalimbali... hatimaye hakuna anayeweza kutengua kwa sababu aliyeufanya ni mwenye mamlaka ya juu,”alisema.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Raisi anapoweka sahihi kwenye rasimu ya katiba ni kuihalalisha kujadiliwa bungeni na sio kupitishwa na bunge. bungeni itajadiliwa na kufanyiwa marekebisho watakayoona wabunge yanafaa.mwishoni kitakacho toka bungeni kitapigiwa kura na wanachi wa tanganyika na zanzibar, wao ndio watakuwa na usemi wa mwisho juu ya katiba yao. slaa now days he has lost focus and determination at all, you can only lie people for a while bt not for all of their life!

    ReplyDelete
  2. mwenyezimungu awaumbue chadema kwa hila zao na ulafi. wamekalia kula ruzuku wao slaa na mbowe. wengine njaa. acha umaarufu wao ushuke

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad