Akizungumzia sakata la kuibuka kwa watu wanaojitangaza kuwania urais, Askofu mstaafu ndugu Valentine Mokiwa amesema kuwa nchi ya Tanzania bado ni changa sana hivyo haipaswi kuongozwa na wanyoa 'unga' maarufu kama 'vipara'.
"Nchi yetu bado ni changa sana hivyo sii busara kuongozwa na wanyoa 'unga'.Tunahitaji damu iliyokomaa kutuongoza". Alisema Mokiwa huku akionekana dhahiri kumlenga mmoja wa watu ambaye ametangaza nia ya kuwania urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania hivi karibuni kupitia kituo kimoja maarufu duniani cha runinga ya idhaa ya Kiswahili.
Quote of The Day:
Don't judge each day by the harvest you reap but by the seeds that you plant.
wewe ni mtanzania kama watanzania wengine na usiwasemehe watanzania waliowengi hayo ni maamuzi yako peke yako. Watanzania tunahitaji viongozi vijana wenye uchu wa maendeleo na sio hao wazee wako hao wenye uchu wa madaraka, wameshatuibia sana na bado hawatosheki. Tanzania itaendelezwa na vijana na sio hao wazee wako hao unaowapigia chepuo waliochoka wanapumulia gesi. Unatugawa watanzania kwa rika zetu na baadaye utatugawa kwa imani zetu. Nyinyi viongozi wa dini wengine bure kabisa hata mantiki huna na ninyi ndio mtatupeleka watanzania pabaya.
ReplyDeleteBaba Askofu hayo ni maoni yake na sababu zake za kutowaamini vijana ngazi ya urais wa nchi, hawasemei watanzania au waumini wake, hayo ni yake ni uamuzi wa msomaji kuyakubali au kuyakataa.Wewe unautaka uongozi wa vijana, unachofanya ni kutaka kuzipa uongozi familia za hao wazee unaowaita wezi waendelee kutufisadi. Hawa vijana wakitaka tuwaamini warejeshe zuruma/wizi wa wazazi wao kwa umma, nina maana kila walichozurumu,fedha, majumba, mashamba, viwanja na majina ya mitata...mfano MAKAMBA ST. mwenye jina ana sifa gani kitaifa? Kila kijana unayemuona anasoma seminari sio anatafuta upadri, wengi wanatafuta ma.slahi
DeleteBaba Askofu yupo sahihi kabisa na lengo lake halikuwa kumsema Makamba kwamba ni mnyoa kipara la hasha alikuwa anataka kuelezea watu wenye tabia na hulka za January Makamba.unajua watawala wa CCM wameshaona hii nchi kama ni shamba lao la kufanyia chochote maana wameshajimilikisha na watanzania ni ng'ombe wao wa kuwafanyia kazi.ukijaribu kuangalia kwa makini utagundua kwamba hawa wezi wa ccm wametumia pesa za watanzania masikini kuwasomesha vijana wao kwenye shule nzuri ndani na nje ya nchi na baadae kuwapenyeza kinyemela kwenye nafasi nyeti serikalini lengo ni kuwawezesha kuendelea kuwanyonya watanzania.wakati huo huo watoto wa wakulima na wafanyakzi masikini ambao ndio walipa kodi na wenye rasilimali wanaishia kulundikwa kwenye shule za kata zisizo na walimu au chochote cha kufundishia ambao wanaishia kupata zero mwisho wa siku.kwa hiyo unakuta viongozi wanabakia kuwa tabaka lile lile kila siku na ndio maana utaona majina yale yale yanajirudia kila siku kwenye nafasi nyeti za serikalini.sio bahati mbaya haya mambo yametengenezwa. Watanzania tuamke tukomboe taifa letu.dawa pekee iliyobaki ni kuking'oa tu ccm madarakani kwa njia ya sanduku la kura na hakuna haja wala kuhangaika kufanya harakati zinazoweza kuleta maafa na vita visivyo na sababu yoyote kwa nchi yetu ya asali na maziwa.Fikiri.....chukua hatua!!!!
ReplyDeletetatizo hao ni wizi wa kura sasa ndugu yangu tutawaondoa vp na tumeshawachoka kinoma ......
ReplyDeleteShughulikia kanisa lako wewe mpumbavu wa maisha
ReplyDelete