Mtayarishaji wa muziki Tanzania Tudd Thomas ndiye aliyetayarisha wimbo wa Diamond ‘MdogoMdogo’ ambao unafanya vizuri sana pamoja na wimbo wa Ommy Dimpoz ‘Ndagushima’ ambazo zote zimepata nafasi kubwa huku wasanii hao wakilipa mamilioni kufanya videos.
Akiongea katika kipindi cha Sunrise cha 100.5 Times Fm na Fadhili Haule, Tudd amesema kuwa alilipwa kiasi cha shilingi milioni mbili kwa kila wimbo katika nyakati tofauti.
“Kikawaida huwa wanasema sio vizuri kwa kuwa ni biashara lakini mimi niko real, ni two million kwa kila wimbo.” Alisema.
Ameeleza kuwa gharama za nyimbo hizo zilitokana na ukubwa wa nyimbo zenyewe na muda alioutumia kukaa studio na wasanii hao.
Tudd amesema wimbo wa ‘MdogoMdogo’ ulitengenezwa kwa muda wa miezi mitatu kwa kuwa ulikuwa wimbo mgumu kwao wote kwa kuwa ilikuwa idea mpya kwa wote, wakati wimbo wa Ommy Dimpoz ulimchukua miezi miwili kuukamilisha.
Ndiyo maana wao ni matajiri na wewe ni maskini tu. Wanakupa milioni mbili kuwafanyia kazi kwa kwa miezi miwili halafu wao wanakwenda kuitumia kazi hiyo kupata milllioni 10 kwa siku moja tu tena wanarudia rudia kwa muda mrefu hadi inawaingizia zaidi ya millioni mia moja! Mngejua jinsi maprodyusa wenzenzu kama wale wa Marekanei wanavokula bata msingekuwa mnakubali kutumiwa vile.
ReplyDeleteNkajua kakulipa mil10, ujinga huo.
ReplyDeletekaka milioni mbili ni ndogo sana, wanakunyonya hao, yani kumbe kuproduce huku ni cheap hv?
ReplyDeleteHuyu nae kumbe fala m 2 anaona peesa anakunja mgongo miezi mi3? Tutolee utaahira wako na utakufa maskini fxyuuuuu! !
ReplyDeletekwendaaaaaaaaa yan
ReplyDeleteujaifikia ata shopping ya mbwa wa madam.