Tundu Lissu: Wachungaji, Maaskofu na Masheikh ni Wala Rushwa.

Wakati akichangia katika mdahalo wa ‘Nani anataka kuwazuia Watanzania kupata katiba mpya, jijini Dar es Salaam na kurushwa na kituo cha ITV, Gazeti la Nipashe limemnukuu Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, akisema baadhi ya Maaskofu na Masheik nchini ni viongozi wanaopewa chakula, vinywaji na pesa kama rushwa. 

Lissu alinukuliwa akisema, “Akina Sheikh Jongo (Thabit Norman) na Jongo mwenzake (Hamid Masoud), Askofu Muhagachi (Amos), Askofu Mtetemela (Donald) na Mchungaji Mgimwa wapo 166 wote hawa ni wana CCM na wameteuliwa na Mwenyekiti wa CCM, wanaitwa kwa Waziri Mkuu, kwa mawaziri wanapewa hela, wanapewa chakula, vinywaji maana yake ni wala rushwa …”.

Ukiyasikiliza na kusoma madai ya Tundu Lissu bila kuyachambua kimantiki unaweza ukadhani ni mambo ya kawaida kisiasa lakini kiuhalisia ni madai ambayo yanagusa taasisi na viongozi ambao uongozi wao unagusa misingi ya kiroho kwa wananchi ambayo hukumu yake haifanywi na binadamu bali na Mwenyezi Mungu. Viongozi wa Taasisi za kiroho ni wajumbe wa Mwenyezi Mungu.

Heshima na utu wa taasisi za kidini nchini ambazo zilipeleka viongozi wake kwenye Bunge la Katiba ambao leo wanaodaiwa na Tundu Lissu kuwa ni wala rushwa, lazima ziheshimiwe kwa njia ya kumtaka Tundu Lissu atoe pia ushahidi wa madai yake.

Kwa lugha nyingine, Tundu Lissu anadai taasisi za kidini (kiroho) zimejaa wala rushwa!. Really? 

I believe these are extremely serious allegations and needs solid evidence. Madai ya Tundu Lissu hayawezi yakapita bila kupata majibu ya uhakika.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Admn hua ckuelewi elewi cjui hua unavuta bangi,kichwa cha habari kimekaa kiuchonganishi kenge wewe,acha kupotosha watu mfyuxzuuuuu

    ReplyDelete
  2. Inawezekana huwa anayaona yanavyotendeka ndio maana amesema. Siwezi kukubali wala kukataa kwasababu viongozi wa dini nao ni binadamu wana tamaa na hisia kama tulivyo wengine ndio maana unasikia siku hizi nao pia wanabaka kwahyo tusitishike na neno viongozi wa dini, pia miongoni mwao wapo wanaopotoka.

    ReplyDelete
  3. Hao ni matunda ya ccm na bebi wake ACT ya zitto.

    ReplyDelete
  4. Kweli mkuu Tundo sema wasiwasi

    ReplyDelete
  5. NYOTE NAONA MNAPOTEZA MDA SOLUTION TUNDU AKAMATWE APELEKWE POLISI HAWEZI KUDHARARISHA VIONGOZI WETU KIASI HIKI TATIZO LAKE NI UJUAJI KUPITA MIPAKA INAMAANA YEYE AKIINGIA MADARAKANI NDO ATAKUWA MTAKATIFU.NDUGU ZANGU WASWAHILI WANASEMA FUMBO MFUMBIE MJINGA MWELEVU ATAFUMBUA HUYU AMBAYE HANA IMANI NA WATU, HATA VIONGOZI WA DINI MPAKA ANAWAZUSHIA KASHIFA KUSUDI MADAI YAKE YAPITE BAADA YA KUONA HAWAMUUNGI MKONO HUYU AKIPATA NGAZI YA JUU ATAHALIBU SANA NCHI.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad