Ufafanuzi Kuhusu ACT-Tanzania Kusaidiwa Kwa Karibu sana na Wanasiasa Wakongwe Nchini.

Ndugu watanzania, wapenzi na wanachama wa chama cha ACT-Tanzania, tunapenda kuwasalimu kwa salamu inayoashiria mabadiliko na uwazi!

Ndugu watanzania, kumekuwa na mfululizo wa watu mmoja mmoja, makundi ya watu, vyama vya siasa visivyofahamu ni kwa nini vipo na hata baadhi ya vyombo vya habari kulalamika kila kunapokucha na kila jua linapikuchwa kwamba Chama kipya kinachokuwa kwa kasi, kinasaidiwa kwa karibu mno na wanasiasa wakongwe nchini pamoja na viongozi wakubwa kutoka nchi za Amerika ya Kusini.Wamekuwa wakilalamika kwamba wanasiasa hao hutoa msaada wa kifedha, kiufundi na kimikakati kuhakikisha kwamba ACT-Tanzania inafanikiwa kuiongoza Tanzania na kuvipiga kumbo vyama vingine kwa mbali.Hata hivyo, mara zote, wamekuwa hawaleti vielelezo kuntu vya kuthibitisha taarifa na malalamiko yao hayo.

Tunapenda kutumia nafasi hii kuwaasa wale wanaolalamika kila siku kwamba; hakuna sababu ya wao kupata shida sana na kuumiaza akili zao, kwani ACT-Tanzania imeshaweka wazi kwamba itakuwa ilitoa taarifa zake za mapato na matumizi katika vipindi maalum.
ACT-Tanzania, Mapato na matumzi ya chama

Kuhusu kwamba kuna mbinu zinazofanywa na ACT-Tanzania kuhakikisha kwamba chama hicho kinavipita vyama vingine kwa kasi, na katika mipango hiyo kuna washiriki wengi na wadau wengi wasioonekana na wanaoonekana, chama hakina la kusema.

Kuhusu suala la kusaidiwa kiufundi na wataalam mbali mbali kutoka maeneo mbali mbali, hili ni jambo la kawaida kwa chama chochote makini kubadilishana uzoefu na ujuzi na watu wengine na kujifanza kwa watu wengine na ni vyema kila asiyejua jambo fulani, akatafuta kujifunza kutoka kwa anayejua na kwa kuwa hakuna mwanadamu anayejua kila kitu na ACT-Tanzania imeundwa na wanadamu basi ni wazi kwamba watakuwa waking'amua hekma na maarifa katika baadhi ya mambo kutoka kwa watu wengine. ACT-Tanzania tutaendelea kutafuta maarifa kutoka kwa watu mbalimbali duniani ili kuhakikisha kwamba shughuli za chama zinakuwa na ufanisi ambao haujapata kuonekana hapo awali katika historia ya vyama vya siasa nchini.

Kuhusu kile kinachotajwa kama hatari ya chama cha ACT-Tanzania kuungwa mkono na wanasiasa wakongwe na kupelekea vyama vingine kupotea katika ulingo wa siasa nchini, ACT-Tanzania hatuna la kusema zaidi ya kuwaambia watanzania kwamba ACT-Tanzania ni njema, na anayetaka kujiunga na ajiunge kwa moyo mmoja.ACT-Tanzania ni chama cha siasa, na chama cha siasa ni watu, hivyo hakuna jambo la ajabu kama chama kinachawishi watu kujiunga na watu wanaamua kikiunga mkono chama.

ACT-Tanzania,Tunapenda kuwaasa watani wetu wapunguze woga kwani chama hiki bado ni chama kidogo tu na wala hakina shida.


ACT-Tanzania.............Taifa kwanza leo na kesho,
Mabadiliko na uwazi ......Chukua hatua.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Asiyejuwa kuwa nyinyi ni tawi la mafisadi ni nani?!uroho wa madaraka umewajaa na nyinyi kamwe sio watu wakuwabadilisha watanzania!

    ReplyDelete
  2. Nani ataibadilisha tz jamani.....

    ReplyDelete
  3. Teh teh eh .Halooooo, shikamoo ccm na bebi wako ACT.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad