Ukweli Kuhusu Kuzikwa Kwa Balali 'Kabari Lake Laonekana'

Mkazi wa Kijiji la Luganga, Wilaya ya Mufindi, Iringa, alikozaliwa Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Daudi Ballali analazimika kutumia saa 32 kufika katika kaburi la kiongozi huyo lililopo eneo la Silver Spring, Maryland nchini Marekani.

Ndugu wa Ballali (pichani) wanaweza kutaka kwenda kuona kaburi la ndugu yao, kutokana na ukweli kwamba wengi wao hawakuwahi kupata fursa ya kumzika Gavana huyo ambaye alikuwa kiongozi wa juu kabisa wa taasisi kubwa inayosimamia masuala ya fedha na uchumi wa nchi.

Mwandishi wa gazeti hili alisafiri kwa saa 24 kutoka Dar es Salaam hadi Washington, Marekani ambako alithibitisha pasi na shaka kwamba Ballali alizikwa Mei 21, 2008 katika makaburi ya Gate of Heaven, baada ya kufariki dunia akiwa nyumbani kwake Maryland, Mei 16, mwaka huo.

Safari hiyo ya siku kumi, ilianza Alhamisi Juni 26, 2014 hadi Jumapili, Julai 6. Mwandishi wa habari hizi aliligundua kaburi hilo baada ya kwenda makaburi ya Gate of Heaven kwa siku tatu mfululizo.

Siku ya kwanza, mwenyeji wa mwandishi ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sasa alimfikisha katika makaburi hayo, lakini kaburi la Ballali halikuonekana na hata mwandishi alipokwenda siku ya pili peke yake, kaburi hilo pia halikuonekana kwa kutokana na ukubwa wa eneo hilo.

Siku ya tatu, Mwandishi wa Mwananchi alilazimika kuomba msaada wa Ofisi ya Makaburi ya Gate of Heaven, ambayo ilimsadia kuonyesha eneo lilipo kaburi hilo, hivyo kuwezesha kupata picha zake.

Kaburi lake liko katika msitari wa mwisho kabisa na Ukanda wa Kijani wa miti iliyozunguka makaburi ya Gate of Heaven, likiwa limeandikwa jina la kiongozi huyo, pamoja na maneno ya Kiingereza yanayosomeka “When the heart weep for what it has lost, the soul rejoices for what it has found”.

Maana ya maneno hayo ni kwamba “wakati moyo ukiomboleza kwa kile kilichopotea, roho hufurahi kwa kile kilichopatikana”. Kaburi hili limezungukwa na makaburi mengine kadhaa ambayo si ya Watanzania, kwani kwa haraka kutokana na mazingira yalivyokuwa, Mwandishi wa Mwananchi hakuweza kuona kaburi jingine lenye majina yenye asili au kuwa na mwelekeo wa asili ya Tanzania.

Uthibitisho huu ni tofauti na hekaya za miaka nenda rudi zilizogubika kifo cha kiongozi huyo, ambaye tangu alipoondoka nchini kwenda Marekani Agosti 2007, hakuwahi kurejea na badala yake zilisikika taarifa za kuugua kwake, kifo chake na baadaye mazishi yake yaliyokuwa ya siri kubwa yakiwahusisha ndugu wa karibu pekee.

Kutokana na mazingira hayo, kumekuwapo na uvumi kwamba Ballali hakufa na pengine amefichwa kusikojulikana, madai yanayochagizwa na mtu aliyejitokeza katika mitandao wa kijamii ya Twitter na facebook, akidai kwamba yeye ni Ballali na kwamba hajafa, huku akisisitiza kuwa wakati ukiwadia ukweli utafahamika.

Mtu huyo asiyefahamika hadi sasa alianza kujitokeza Twitter, Oktoba Mosi, 2012 pale aliposema “Nitakutana na Rais Kikwete (Jakaya) na ujumbe wake wiki hii hapa Marekani”. Mtu huyo alidai kwamba alikuja nchini Tanzania na kukaa karibu na Hoteli ya Hyatt Kempinski Kilimanjaro na baadaye kuondoka ghafla kwa kile alichokiita sababu za kiusalama.

Novemba 13 mwaka huo alituma ujumbe akisema:“In Dar es Salaam, Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kempinski Kilimanjaro Hotel. Feels good to be close to my former office, BoT,” akimaanisha kwamba niko Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, najisikia vizuri kuwa karibu na ofisi yangu ya zamani BoT.

Mtu huyo ambaye sasa tunaweza kuthibitisha kuwa ni feki amekuwa akiendelea kutuma ujumbe akijitambulisha kwa jina hilo la Ballali.

Ballali alifariki dunia kama ilivyotagazwa, lakini ilikuwaje akaenda safarini Washington, ugonjwa wake na hata kifo chake kilikuwaje? Je ndugu zake wanasemaje, safari

Post a Comment

20 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. There is something behind this story.natoa muda fulani utasikia tukio linalomuhusu Balali.hii story ina lengo la kupumbaza watanzania!! Why vitu hivi vinakuja sasa na sio muda mwingine wowote since 2007?!!! Serikali hii ya ccm ina mambo ya ajabu sana.wanafikiri hizi ni enzi zile za ujinga wa watanzania kudanganywa kitoto toto.narudia tena kuna kitu kinatengenezwa na serikali na ccm jiandaeni mtakuja kuniambia.

    ReplyDelete
  2. Haa haa haa hatudanganyiki

    ReplyDelete
  3. mmh wewe umezaliwa iringa ukazikwe usa,kweli??walikosa pesa za kusafirisha maiti?

    ReplyDelete
  4. mmmm mhehe akazikwe usa,walikosa pesa za kusafirisha maiti?utata mtupu

    ReplyDelete
  5. aaaaah wapiiih! hatutakiiiih!

    ReplyDelete
  6. Nakuhakikishia siku tu tukiingia 2015,tutalifukua kaburi hilo ili kuona kama kuna masalia.kweli,na kama yapo tutayapima DNA.Mtu yupo Cyprus anakula bata ninyi mnatuzuga tu hapa.Hatudanganyiki.

    ReplyDelete
  7. Hakuna kitu hapo,watz wa leo c wale wa 1961,Dec. Mkome kucheza na akili zetu miku....n..d..u yenu na mi CCM yenu mfyuuuuu

    ReplyDelete
  8. Haya alikufa, amezikwa huko USA Kama mnavyosema, lkn ndio hâta maiti yake isiagwe kweli? Mmh walikosea jinsi ya kutudanganya Sasa ndio wameona wajenge hilo kaburi waandike na maneno wapige picha, haya bana za mwizi 40 tutajua tu, Tena inawezekana wamegeukana kuna mmoja Wao anataka kuropoka kitu kwa watanzania, ndio maana wamemuwahi na picha ya kaburi, 2009, 2010, 11, 12, 13 Hadi Leo 14 ndio kaburi lionekane? Jmn hizi dhambi hadi nae shetani anashangaa mlivyozidisha nyie kijani

    ReplyDelete
    Replies
    1. msiban wanapiga piga picha maiti..ye hata moja?

      Delete
  9. Ccm imeoza hadi inatia aibu.

    ReplyDelete
  10. watoto ndo wanaweza amini huu utoko wenu fyuuuuuuuu

    ReplyDelete
  11. Huyo mtu anayejifanya yy ni balali atanas tuu.....ni watu wa upinzani....ccm chama chetu hakina ubaya wwt.....wapinza hawajafika popote mikwaruzano lundo....haaya wakipewa nyazifa tamu tamu si itakua shida simba na yanga kila kukicha malumbano...hatutaki hiyo zimwi likujualo halikuli likakwisha....ccm oyeeeee....oye saaana tuu

    ReplyDelete
  12. KUZALIWA IRINGA NA KUZIKWA MAREKANI SIO JAMBO LA AJABU. MBONA WATU KIBAO WANAZIKWA DAR ES SALAAM BADALA YA VIJINI KWAO WALIPOZALIWA? HALAFU SUALA LA KIFA CHA MTU LINAWAHUSU FAMILI YAKE SIO WATU WENGINE. NA PIA MJUE KUWA HUKO MAREKANI NDIO NYUMBANI KWA HUYO MAREHEMU KWA HIYO KUZIKWA HUKO SIO AJABU

    ReplyDelete
  13. WATANZANIA NI WATUB WA KUPUMBAZWA KILA SIKU AMEKUFA FORMEER GOVERNOR HATA MKUBWA MMOJA WA SERIKALI ASIENDE AMEUMWA KWA KUJIFICHA ANAKUFA KWA KUJIFICHA ANAZIKWA KIMYA KIMYA KWA AJILI YA NINI JE HAKUWA NA MARAFIKI AU WAFANYAKAZI WENZAKE NASISITIZA JAMAA YUKO HAI TENA WAJAMENI IPO SIKU TUTATOA USHAHIDI ILA ANAPATA SHIDA SANA MAANA ANATEMBEA ANALINDWA NA MAKOFIA MAKUBWA KAMA COW BOY NA AKIONA NGOZI NYEUSI TU INAMWANGALIA SANA MASHAKA HAYAKOSEKANI ILA SIKU HIZI ANAVAA KAMA WA NIGERIA NA MARA NYINGIBNE MAKOTI MAREFU NA KOFIA YA COWBOY PIA MIWANI NYEUSI.

    ReplyDelete
  14. KWA JINA LAKE LILIVYOKUWA KUBWA, HATA BENDERA INGEPEPEA NUSU MRINGOTI TU. LAKINI HAMNA HATA DIWANI ALIYEHUDHURIA MAZISHI WAKATI NI MTZ MWENZETU?
    CCM MNATUZUGA ACHENI HIZO

    ReplyDelete
  15. Mmhhhhhh hii ni zaidi ya hatare, haya lisemwalo lipo

    ReplyDelete
  16. Watanzania hivi kwa nini mnapenda kushupalia mambo ambayo hayanafaida yoyote?fanyeni kazi acheni midomo,ccm hoyeeeeeeeeeee!

    ReplyDelete
  17. Hahahah kula bata balali

    ReplyDelete
  18. WATANZANIA JUENI UKWELI JUU YA DAUDI BALLALI, UFISADI, UGONJWA, KIFO NA COVER UP
    Daudi Ballali hakuwa raia wa Tanzania tena baada ya kuukana uraia wa Tanzania na kuwa raia wa Marekani miaka kadhaa aliyoishi Marekani akifanya kazi World Bank. Alikuwa ameoa mmarekani na watoto wakubwa tu. Aliolea jimbo la Connecticut. Alipewa kazi na swahiba wake Ben Mkapa ambaye aliivunja katiba aliyoapa kuilinda, kuitetea, na kuihifahi kwa kumpa ajira raia wa nje Bw. Daudi Balali pindi akijua fika alifanyalo. Ben Mkapa aliwahi kuwa balozi wa Tanzania nchini Marekani miaka ya 1980s ambapo aliweza kukutana na Ballali na kuwa marafiki wa karibu zaidi. Daudi Ballali alipewa kitengo muhimu cha usimamizi wa fedha nchini kama Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, nafasi inayohitaji kushikiliwa na raia halisi. Plan hii si makosa bali ni mkakati mahususi kuihujumu nchi uliopelekea nchi kuporwa mabilioni ya pesa na mafisadi mbali mbali nchini kwa kipindi kirefu cha ongoing wa raia huyu wa kigeni. (Kashfa ya EPA) . Balali alikuwa akiumwa na hivyo alipopata mwanya wa kutoroka kabla ya kufikishwa mahakamani alifanya hivyo. Ikumbukwe nchi ya Marekani haiwezi kumpeleka raia wake nje ya nchi ashitakiwe ili miradi hajavunja sheria za Marekani. Ballali alikuwa akibeba pass mbili za kusafiria, moja ya kimarekani na nyingine ya kidiplomasia (diplomatic passport) ya Tanzania kinyume na Sheria ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Hapo 2008 Wakati wa sakata hilo, balozi Ombeni Sefue akiwa Washington DC kama balozi wa Tanzania Marekani alitoa kauli zenye utata juu ya mtuhumiwa Daudi Balali kutorudiswa nyumbani kujibu tuhuma nzito za wizi wa mabilioni Benk kuu BOT aliouidhinisha, alijibu kwa kusema Serikali ya Tanzania ilikuwa imebatilisha diplomatic passport yake na hivyo hakuwa halali nchini Marekani. Pia siku chache alitoa kauli yenye utata kuwa Bw. Ballali alikuwa mgonjwa amelazwa hospitalini Boston, jimboni Massachusetts na familia yake wanaomba privacy. Baada ya siku chache ikatangazwa bwana huyu amefariki dunia na mazishi yake yatakuwa ni ya familia tu, swala lililoushangaza umma wa watanzania wote duniani. Taarifa iliyotolewa baadaye ni kuwa mwili wa marehemu Ballali ulizikwa makaburi ya Gate of Heaven, mjini Silver Spring jimboni Maryland chini ya maili moja na maskani yangu. Mpaka leo hakuna Mtanzania yeyote anayejua ukweli wa hili kwani "cover up" kuficha ukweli kwa makusudi kumeendelea. Mabilioni ya fedha ya umma yametoweka na Siri nzima alitokomea nayo mmarekani huyu Daudi Balali. Balozi Sefue anajua ukweli lakini ameendelea kuudanganya umma kwa niaba ya serikali. Rais Mstaafu Mkapa na wengine wengi wana case kubwa za kujibu. Siku za usoni haki itatendeka. Watanzania popote walipo watakapopata nafasi ya kujua ukweli na sheria kuchukua mkondo wake.
    KWA KIFUPI: BW. BALLALI ALIKUFA LAKINI HAKUWEZA KURUDI TANZANIA HATA KABLA YA KIFO CHAKE KWANI HAKUWA RAIA WA TANZANIA, YEYE NI RAIA WA MAREKANI PASI NA SHAKA. ALIOA MKE WA KIMAREKANI JIMBONI CONNECTICUT NA ALIZAA WATOTO KABLA YA KUMTALAKI MKE HUYU. RAIS MSTAAFU BEN MKAPA ALIMWAJILI KWA MAKSUDI ILI OPERESHENI FUJA NCHI (UFISADI) UENDE VIZURI. KIFO CHAKE KIMEFURAHIWA NA MAFISADI KATIKA MTANDAO HUO MKUBWA NA WAKUTISHA, KWANI UPOTEVU/ WIZI WA MABILIONI YA FEDHA YA UMMA ULIHUSISHWA NA YEYE AMBAYE ANGEKUWA HAI HATA KUWA KATIKA ARDHI YA NCHI YETU TANZANIA ANGEKUWA MTUHUMIWA NAMBARI MOJA. RAIS MSTAAFU BEN MKAPA ALIIVUNJA KWA MAKSUDI KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA ALIYOAPA KUILINDA, KUITETEA NA KUIHIFADHI KWA KUMWAJILI RAIA WA KIGENI NAFASI YA JUU NA NYETI. HIVYO ANA KESI KUBWA YA KUJIBU. UHUJUMU UCHUMI, KULIWEKA TAIFA LETU MASHAKANI KIUSALAMA, KUSALITI KIAPO CHAKE, WIZI WA FEDHA YA UMMA, UDANGANYA KWA MAKSUDI YA KUPOTOSHA UMMA, NK.
    NDUGU WANANCHI TEGA MASIKIO UJUE UKWELI ZAIDI JUU YA KASHIFA HII YA KIHISTORIA

    Sent from my iPad

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad