Utabiri wa Kifo Chake Aunty Ezekiel Amwaga Machozi

SIKU chache baada ya Nabii wa Huduma ya Ufufuo, Buza jijini Dar, Yaspi Paul Bendera kutabiri kuwa vifo vya mastaa vitaendelea, staa wa sinema Bongo, Aunt Ezekiel amemwaga machozi baada ya kuhusishwa kuwa yeye ndiye anayefuata kufa.

Kupitia gazeti la Ijumaa, Juni 13, mwaka huu, Nabii Bendera alisema ameoneshwa kwamba wasanii 20 wangekufa hivyo kama wanataka kujinusuru, wafike kanisani kwake na kupakwa mafuta.
Wakati gazeti hilo lilipoingia mtaani, ukurasa wa mbele uliambatanisha picha mbalimbali za baadhi ya wasanii waliofariki pamoja na wengine ambao wapo hai akiwemo Aunt Ezekiel (pichani) ndipo utata ulipoanzia.

Chanzo kilicho karibu na staa huyo, kilipenyeza habari kuwa, ndugu zake walimpigia simu Aunt ambapo walionesha kuwa na hofu ya kifo ambayo ilimfanya mwigizaji huyo naye aangue kilio mara kwa mara.
“Ndugu zake walilia sana kwani baada ya kuona picha ya Aunt katika gazeti, waliamini maneno ya nabii huyo kwa kujua pengine anayefuata kufa kati ya hao kumi ni ndugu yao.

“Aunt alilia sana siku hiyo na Wema (Sepetu) ndiye alisimama kumsihi asiendelee lakini kama haitoshi, bado amekuwa akiteseka mara kwa mara kila anapokumbuka tu, anakosa amani na kujikuta analia,” kilisema chanzo.

Hata hivyo, chanzo kimeeleza kuwa baada nguvu kubwa kutoka kwa marafiki wa karibu wa Aunt akiwemo Wema wamekuwa wakimsihi amuombe Mungu kwani si kwamba picha yake kutumika gazetini ndiyo atakufa wala maneno ya nabii huyo si sababu ya kuamini kwamba kweli vifo hivyo vitatokea.

“Wamemtaka amuombe Mungu na kutosikiliza maneno ya watu maana kuna watu ambao wamekuwa wakishadadia ishu hiyo katika mitandao na kumfanya Aunt aingiwe na hofu ya kifo, kidogo ameanza kuwaelewa,” kilisema chanzo.

Baada ya kupata habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Aunt, alipopatikana aliweka wazi kuwa suala hilo limemkosesha amani sana pamoja na ndugu zake.

“Walijua ndiyo nakufa, na mimi pia niliposikia harakaharaka niliamini nimetajwa mimi hususan waliponiambia picha yangu imetumika gazetini, nililia sana siku hiyo na siku zilizofuata pia watu walizidi kuniliza mitandaoni, mwisho wa siku nimemwomba Mungu anisimamie, atakaponichukua ni kwa mapenzi yake kama maandiko yanavyosema,” alisema Aunt.

Kwenye utabiri huo, nabii huyo alinukuliwa kuwa ndani ya mwezi Juni, idadi ya wasanii 20 wangefariki lakini hadi sasa hakuna kifo chochote kilichotokea hali ambayo inawafanya baadhi ya watu kuamini kwamba masuala ya kifo ni Mungu pekee anayejua nani atakufa lini.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyo mchungaji alitaka hao wasanii waende kanisani kwake akawapake mafuta ili aanza kuwatumia wasingeweza kutoka tena katika kanisa hilo. Mungu ndie anayepanga na haKuna binadamu atakayeweza kupangua litakalopangwa na Mungu mwamini Mungu ndio jibu pekee katka maisha yako.

    ReplyDelete
  2. usiogope miss Mungu ndie mpangaji wa kila jambo huyo ni mwanadamu asiwatisheni, halafu msipende kuyumbishwa na wanadamu

    ReplyDelete
  3. huu uchungaji ulianzishwa siku hizi ni balaa, watu wanajivisha majukumu ya Mungu, hata mitume hawakujua ni lini wangekufa vipi wewe mchungaji?

    ReplyDelete
  4. Usiogope, Mungu mwenyewe ndie anaefahamu hatima ya kila mmoja. Na usiwe na hofu kwani hofu inatoka kwa ibilisi, muamini YEHOVA na umsikilize na kumfuata yeye pekee...usiwe na hofu kwani " life is not how long we live bt how well we live sambamba na kufuata mapenzi ya Mungu". Muombe Mungu akupe moyo wa ujasiri wa kutotishwa na maneno ya watu, bali fuata neno la Mungu tu mdada.

    ReplyDelete
  5. ahaha kifo sio mchezo kinatisha na ndo maana ikaekwa siri Mungu ni mwaminifu hayo mabo ya kuona destiny za watu yabaki kuwa muvie tu yake haoni iweje aone ya watu ... hata yesu yesu alipoonyeshwa picha nzima ya atakavo kufa aliomba kikombe kimuepuke iweje so huyo mchungaji aache kutafuta kick God is everywea sio kanisani kwake tu na kama anauwezo wa kubadilisha vifo vya watu aanze na ukoo wake kwanza afu ndo ss tufate eti wakitaka wasife waje kanisani kupakwa mafuta hahaha ajipake yeye tuone kama ataishi milele,,, watu wanamchezea sana Mungu yani

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad