Watu wanane wanashikiliwa na polisi wakiwemo Madaktari kwa tuhuma za kuhusika kwenye tukio l a kutupwa kwa mabaki ya miili ya binadamu jana jioni nje kidogo ya jiji la Dsm
Huku likiendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo,Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova ametangaza kuundwa kwa jopo la upelelezi kuchunguza tukio hilo, ili kubaini taratibu gani zilikiukwa na kujua aina ya mashtaka itakayowakabili.
Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa miili hiyo ilikua katika Taasisi ya mafunzo ya udaktari IMTU kabla ya kukutwa imetupwa eneo la Bunju.
Taasisi hiyo imekiri kwamba mabaki ya miili ilikua katika taasisi hiyo lakini haijatoa maelezo kuhusu kutupwa kwa miili hiyo.
Kamanda Kova amewatoa wasiwasi watanzania kuwa hakuna mauaji yoyote ya kimbari yaliyotokea sehemu yeyote nchini hivyo polisi iachiwe ifanye kazi yake kisha itatoa taarifa hapo baadae.
Toka lini wanafunzi wakatumia miili ya watu kwenye practical zao name sio wanyama na kama inaruhusiwa kufanyiwa MTU practical Mara nyingi anakuwa hai nasio kuua na kukausha maiti, unataka kuniambia izo maiti hazina ndugu. Usikute hawa majamaa waliteka ao watu. Hii story mpaka sasa upande wangu naona inarushwa rushwa maana hainingii akili ndugu wakafiwa wakaacha maiti zichewe na wanafunzi wa udaktari. Huu ni ukiukwaji wa haki za binadamu maiti pia inahaki ya kupumzishwa kwa amani na sio kuchezewa chezewa halafu kutupwa jalalani. Hawa watu ni wauwaji...sheria ifanye kazi hapa maana watu 20 sio kitu chakupuuzia kabisa.
ReplyDeletekama huelewi ndugu yangu uulize kwanza. mwaka wa kwanza wa udaktari lazima ujifunze viungo vyote vya binadamu kwa kukata maiti. mara nyingi maiti zinazotumiwa ni zile zisizo na ndungu na zimehifadwiwa kwa muda mrefu. wanafunzi madaktari hawaanzi kwa mgonjwa moja kwa moja.
Deleteutaratibu walio tumia kutupa mabaki ndiyo haukufuata sheria.
nenda nchi yoyote duniani, madaktari wanafunzi lazima wakate maiti
yaan hapo mdau umesema ya ukweli kabisaa,tangu lini practical ikafanyika kwa binadamu aliyekufaa? na inakupasa kufanya hivyo basi ukimaliza ya bidi maiti ikabidhie kwa ndugu ili iweze kuhifadhiwaa,unajua tatizo la nchi yetu ni kwamba viongozi wetu asilia 90 wana vyeti vya shule vya kughushii na ndio maana mtu anaweza danganya MEDIA na wakakubali kwa sababu hawana upeo wa Elimu yeyotee,na kama hiyo shule wamekubali ni wao waliotupa hizo maiti basi mkuu wa shule inabidi ahojiwe hizo maiti alizipata wapi na kwanini alifanya hivyo na ikibidi shule yake ifungwe na atiwe mbaroni huu ni unyama wa hali ya juu,na ni ukiukwaji wa haki na binadamu na cha kushangaza Raisi kikwete kakaa kimya bila kusema chochotee na wakati hii ni issue kubwa anatakiwa kuwa involved,yeye anasema ana urafiki na Baraka obama,mbona mwenzio obama huwa hapuuziii mambo kama haya?halafu tunasema nchi ina raisi ni bora atoke tuweke mwinginee tumechoka na hawa maraisi mburulaz kazi yao ni kushow off suti zao tuuu!!!!
ReplyDeleteanoy 7.20 ni hv, madactari mwaka wa kwanza kwenye somo na anatomy wanatumia miili ya binadamu kujifunza, maiti zile zinazozikwa na almashauri zilizokosa ndugu ndizo zinazotumika, na uwa kunakuwa na exchange program za maiti, hao maiti unakuta wametoka mkoa mwingine si dar, wamekaa mochwari kwa mda mrefu bila kuchukuliwa na ndugu, badala ya almashauri kwenda kuzika, kuna utaratibu maalumu vyuo vya udaktari uwa vinaomba kwa ajili ya mafunzo......kosa walilofanya IMTU ni kuvitupa uko jalalani, lakini inavyotakiwa ni kuvichoma kwenye matanuru, na ni kitu cha kawaida kinafanyika kwenye vyuo vyote vya udaktari.......tetesi zinasema walikuwa ndo wanamalizia kutupa za mwisho ili waanze kuchoma kwa kuwa tanuru lao limeharibika
ReplyDeleteKama tanuru lao limeharibika si wangeomba hata tanuru la muhimbili au Kairuki, au wangeenda kuwazika halmashauri.... Hoja ya tanuru kuharibika ndo iwafanye watupe ovyo maiti haiingii akilini kabisa....wawajibishwe
DeleteHAKUNA WASOMI HAPO MAANA HAWAFANANI WANATUONYESHA NN
ReplyDeleteNIKWELI, MAGAZETI YOTE YAMETUONYESHA WATUHUMIWA WALIOKAMATWA NI WAHINDI UDAKU MNATUONYESHA WASWAHILI, MNAFICHA NINI ? KOSA LA MWEUPE PICHA YA MWEUSI, MNAPOTEZA UHALISIA WA HABARI HUSIKA..
Delete