Wiki za hivi karibuni mwanamuziki wa bongo fleva ambaye pia ni mwanaharakati wa kupinga matumizi ya dawa za kulevya Rehema Chamila ‘Ray C’ amepatwa na misukosuko mingi ambayo haikuwa mbali sana na mahusiano na dawa za kulevya….
Ni wiki mbili zilizopita tangu mwanadada huyo achezee kichapo toka kwa mwanamuziki wa bongo fleva Rashid Makwilo maarufu kama Chid Benz akimtuhumu kumpotosha mkewe….
Ikumbukwe kuwa kabla ya tukio hilo la Chid, Ray C alikwaruzana na Legend wa bongo fleva TID baada ya kuposti kwenye mtandao wake ujumbe wa kumuomba waongee….
TID alimuijia juu mrembo huyo kwa matusi kibao na kumtaka akae mbali nae na asimfuatefuate….
Ni hivi karibuni Ray C ameanza harakati za kuokoa wasanii na watu ambao wanahisiwa kutumia madawa ya kulevya, hali ambayo imemfanya ajijengee maadaui wengi kwenye jamii ya watumiaji wa madawa ya kulevya ambao wameapa kumsambaratisha….
“Ray C anajisumbua bure tu, anashindana na sisi, sisi kama anaona tumepotea atuache,kwanini asihangaike na mabwana zake kwanza? huyu demu vipi?,” alisikika teja mmoja maarufu kwa jina la Lima wa Tandika.
Lima aliyekuwa akipewa sapoti na wenzake waliokuwa pembeni yake aliendelea kufunguka kuwa Ray C asiendelee kuumiza kichwa kudili nao, kama yeye ni mwanaharakati wa kweli basi adili na wanaowafikishia hayo madawa….
“Mi nashangaa kumuona akihangaika na sisi wakati kuna watu ambao anapaswa adili nao. Awatafute wale kama kweli yeye ni shujaa,” aliongeza kijana mmoja aliyeonekana kuzidiwa na kilevi.
Kijana huyo alimuonya mwanadada huyo asiwafuatilie, lasivyo atahatarisha maisha yake kwani wakubwa wakijua watakasirika sana na wanaweza kumfanyia chochote.
“Mngemshauri tu aachane na sisi, wakubwa wetu wakijua ni kesi kubwa mno, sijui kama anaweza kupambana nao,” aliongeza kijana huyo.
Teja huyo alienda mbali zaidi na kudai kuwa alichofanyiwa na TID na Chid Benz ni trela tu, akitaka picha kamili aendelee kuwafuatilia.