Wema Sepetu Amlipua Tena Kajala Baada ya Kumwita Mnafaki

Shakoor jongo na MUSA MATEJA

BEAUTIFUL Onyinye, Wema Isaac Sepetu (25), amemlipua aliyekuwa shosti wake, Kajala Masanja ‘K’ ambaye wiki iliyopita alimwita mnafiki.
Habari hiyo ya kuitwa mnafiki iliandikwa kwenye gazeti hili toleo lililopita iliyokuwa na kichwa kisemacho; ‘Kajala: Wema mnafiki’.

Katika habari hiyo, Kajala alikaririwa akisema kwamba licha ya watu wengi kuamini wamepatana, hakuna ukweli kwani rafiki yake huyo ni mnafiki kufuatia kutomthamini na kutokuwa karibu naye kama zamani likiwemo suala la kumsifia mtu ambaye alikuwa na ugomvi na Kajala (Dacutee).
Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar, Wema alisema alishangaa kuona Kajala anamwita mnafiki wakati hakuwahi kupatana naye tangu walipotofautiana kipindi cha nyuma kama alivyosema.

“Nashangaa Kajala ananiambia mimi ni mnafiki ‘ok fine’ na huo unafiki wangu unakuja pale nilipomu-wish Dacutee siku yake ya kuzaliwa, alitakaje eti? Yaani kwa kuwa yeye ana bifu la kumchukulia bwana’ke na mimi nijiingize kwenye bifu lao?

“Au tofauti zangu mimi na yeye, Aunty Ezekiel aingilie, itakuwa sahihi kweli kama wanavyofanya hao watu wake anaozurura nao siku hizi? Wanaingilia vitu ambavyo hawavijui kiundani wake? Nasema siyo sahihi kabisa mimi nitabaki kama Wema Sepetu na yeye atabaki kama Kajala Masanja na asifikirie kuwa nitakuja kuwa kama zamani na yeye halafu kama anamaindi kuhusiana na Dacutee mbona Petit Man ambaye ana uhusiano naye aliweka picha ya Dacutee na kumu-wish hajammaindi?” aliwaka Wema.

Akiendelea kutema cheche mbele ya kinasa sauti chetu, Wema alisema anachopaswa kuzungumza Kajala ni ukweli wa matatizo yao na siyo kusingizia watu wengine.

“Mbona siku ile niliwahadithia kila kitu (waandishi) kuhusiana na tatizo letu, si nimetoa kinyongo changu ambacho nilikuwa nacho siku nyingi hivi sasa najiona mwepesi na kama na yeye anataka kusafisha moyo wake anatakiwa afunguke, kuanzia leo nataka niseme sitaki kusikia na kuulizwa suala la mimi na Kajala kwani nimechoka na nina mambo mengi ya kufanya,” alisema Wema.

Akizungumzia ishu ya kukutana na Kajala na kupiga picha za pamoja wakiserebuka hivi karibuni, Wema alisema alifanya vile kuonesha kwamba hana kinyongo na ndiyo maana alivyoombwa apige picha na Kajala, hakusita kufanya hivyo.

“Mimi ni mtoto wa Kiislamu na nina imani na upendo kwa kila mtu, siwezi nikamkatisha mtu furaha yake na ndivyo ilivyotokea, niliombwa nipige picha ya pamoja na Kajala siku ile ya shughuli na nilifanya hivyo baada ya pale nikaenda zangu kulala,” alimalizia kusema Wema.

Bifu la mastaa hao wakali wa Bongo Movies liliibuka baada ya Wema kumtuhumu Kajala kuwa ametembea na aliyekuwa bwana’ke, kigogo aliyetajwa kwa jina la CK.
GPL

Post a Comment

32 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. achana nae anatapatapa huyo mfa maji.

    ReplyDelete
  2. Haya bwana mtt WA kiislam, uelewi Ata maana ya mwezi mtukufu? Kutwa kucha kugombeA wanaume amuoni aibu?? Mbona cjaona wanaume wanagombea wanawake humu? Huyo ck aliyewafanya mgombane Ni mmeo? Nyote c wezi Tu! Na sioni kosa la kajala wewe ulirudi kwa domo na yy akapata chance! Kwahiy uliyaka uwe na domo na ck kwa wkti 1! Umechakaa domo aongi bado una vitu vya ck, tunataka tuone vya domo viko wapi! Umezeeka wema pisha njia watoto wapite!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unaonesha ni jinsi gani ulivyo low in thinking capacity. Mada inasema vingine na majibu yako mengine kabisa. Inaonesha dhahiri ni jinsi gani una chuki na Wema Sepetu na anakunyima sana ucngizi. Wema alishamove on cku nyingi na yupo happy na Aunty wake lakini huyo Kajala kutwa kucha haishi kumzungumzia. Mara kwa Zamaradi, mara Global. Lakini hilo huoni. Acha chuki ziczokua na msingi ilihali hata hujui kiini hasa cha ugomvi wao. Fikiria ya maendeleo panya buku wewe.

      Delete
  3. Ni kweli wewe wema Ni mnafiki, kwenda kufuturisha domo na family yake, wakati nyie wazinzi na mapicha juu mmeshikana huo ndo uislam unavyosema? Tungekuona wamana ungewaita yatima, wajane, na wengine wenye uitaji mbona Ni wengi! Umefuturisha kwa kutaka sifa Tu! Mbona mama yko kwenye picha atumuoni? Au unampenda mama WA domo kuliko mama yako. Mnafiki Sana wewe mama yako kwanza ao wengine wafuate. C unaona domo mama yake kwanza! Unazidiwa na mtoto WA kiume anampenda Sana mama yake. Jifunze mnafiki mkubwa!

    ReplyDelete
    Replies
    1. We nawe wa wapi? Alokuambia upendo wa mama na mwana unapigwa kwa show off nani. Kwani asipopiga picha aku kuzionesha ndio hampendi mama yake. Nyoko wewe rejea kwenye mstari wa mada husika na siyo kuleta chuki zako hapa. Sasa ulitaka awaalike ukoo wako na kijiji chenu? Mbweha mkubwa wewe

      Delete
  4. wewe 8:47na huyo 8:57 ndio wanafiki,kwani lazima awe na urafiki na huyo kajala wenu,yeye kajala kashatolewa jela,aendelee na maisha yake,siyo kutwa kumtengenezea mwenzie maadui,mtu mzima kaa na watu wazima wenzio,yeye kumsaidia mwenzie laki tatu tu aliona hasara,maneno kila kona kasahau million kumi na tatu,aende nimemchukia sana sipendi wezi wa fadhila ktk maisha yangu,kwani angekaa kimya ingekuwaje,mara kwenye tv,mara magazeti alimradi watu wakuone umeonewa,kajala endelea kusikiliza ujinga wa hao wanaokudanganya,kumbuka hapa duniani CALMA NEVER FORGERT THE ADRESS,na WEMA SIKU ZOTE HAUZI,

    ReplyDelete
  5. ugonvi wa Wema na Kajala haukusababishwa na huyo ck wenu,sababu kubwa ni huo unafiki wa kajala,maana kajala yuko na ck muda mrefu,na wema alishasikia siku nyingi,tatizo kajala baada ya kuona anapewa hela nyingi na huyo bwana akaanza kumpiga mwenzie majungu,hicho ndio kilichomuumiza wema,ktk hali ya kibinadamu hata nyie mnaomtetea kajala,msingeweza kuvumilia,na akumbuke kwa kitendo cha wema kumtolea kiasi kile cha hela hili kajala atoke jela,kilipingwa san na familia ya wema hususan mama yake na dada yake,wema alipigwa na mzazi wake,na magazeti yaliandika,sasa leo wewe umekuwa binadamu wa aina gani,unasahau yote unapita kwenye vyombo vya habari kumchafua aliyekusaidia,na kuungana na kina penny,kama siyo unafiki ninini,nafsi inamsuta kajala,anajikaza,lkn mwisho wa siku anaumia,

    ReplyDelete
  6. mmh bor umeongea maana kila unalofanya kwa binadamu baya,kajala ukumbuke maneno ya waenga, tenda wema nenda zako,usingoje shukurani,hicho ndicho alichokifanya wema,kakutendea wema kwake imetosha,wewe kajala endelea na mashost zako wapya,muache na yeye aishi maisha yake,hila ukumbuke siku zote umebeba mzigo mkubwa sana,usipoulipa duniani wema alikutendea mwenzio,basi utaulipa kwa mungu,na usipoulipa wewe basi paula ataulipa,kwa njia yoyote hile,wema hauozi.

    ReplyDelete
  7. Wema Ana kiherehere kwani akuwaona mayatima wenye kuitaji msaada, au Ana ndugu zake wenye kuitaji msaada! Alitaka sifa Sana,

    ReplyDelete
  8. Mimi hapa ndo huwa naiona tofauti ya wanawake na wanaume, eti tupo sawa!!!

    ReplyDelete
  9. Mimi hapa ndo huwa naiona tofauti ya wanawake na wanaume, eti tupo sawa!!!

    ReplyDelete
  10. mwezi bado haujaisha ikifika wakati wa kufuturisha yatima,atafuturisha tu,wewe 8:57 una chuki zako binafsi,kwa hiyo umeumia diamond na familia yake kufuturu nyumbani kwa wema,unajisahaulisha kama diamond huwa anaishi na wema hapo kwake,je unajuaje hizo hela za kuaandaa futari kama diamond ndiyo katoa,acha chuki zako,na kufuturisha siyo lazima,ni maamuzi yako,na unaruhusiwa kumfuturisha yoyote alimuradi awe muislam na anafunga,na wewe ulivyomchukia wema,hata angefuturisha hao yatima,mngemsema tuu,hoo hela kaongwa hoo ushuzi gani sijui,fanyeni yenu,hovyoo.

    ReplyDelete
  11. DOMO CHUKUA KAJALA TUMUONE MTOTO WA KIISLAM.

    ReplyDelete
  12. Mhuu huyo wema mbona asomeki mi naona pilau na chaulo kenye msiba wa babaye nimeona amezikwa na kanisa huyo si mtt wa mchepuko wa mzee balozi kweli au wadau mnasemaje

    ReplyDelete
  13. Tatizo c kufutarisha! Tatizo sheria ya kiislam inaruhusu kufuturisha hawara yako! Kwani naona kipindi cha mfungo kama watu wanaishi bila ndoa wanapumzika mpaka mfungo uishe! Msitetee ufirauni! Wema ajitambui kabisa!

    ReplyDelete
  14. Heee! kumbe mapambano yanaendelea aya kajala twendeeeee !

    ReplyDelete
  15. wewe kajala huna shukrani pimbi wewe watu wanasema usimsahau mtu alie kutoa kwenye matatizo sasa wewe unamsahau wema...na alicho kufanyia hukioni...aiseeee wewe dada..mungu akulaani..wanao kutetea wote ni wambea na wanakutetea sababu ya chuki zao..hawakupendi panya wewe..na nyie mnao sema ugomvi ni kisa ck..mshindwe wema aliachana nae yupo kwa anae mpenda huyo ck wa nini..kajala wivu unakusumbua huna lolote na mwisho wa ubaya aibu..sikupendi panya buku wewe

    ReplyDelete
  16. KAJALA MUACHE MWENZIO IMETOSHA,FANYA YAKO MTU MZIMA,MWACHE PAULA AFANYE URAFIKI NA WEMA,MAANA ANGALAU WANAKARIBIANA UMRI,WEWE NENDA KWA WAKUBWA WENZIO,BASI KAMA UNATAKA URAFIKI NENDA KWA KINA BI STAHAA,AU MAMA ABDUL,MBONA MNAENDANA KI UMRI,UNAMNGANGANIA MTOTO WA WATU,KWANI JEEE,MPATA JIONI WEWE,UMEANZA KUUZA TANGU MIAKA KUMI NA TATU,PROMOTER BONGA KAKUFILIGISA WEWEE,ENZI ZILE UNACHEZA SHOW MIKOANI,MPAKA LEO BADO TU UNAUTAKA UJANA,TULIA WEWE,MWISHO UTAKUTANA NA BINTI YAKO NYUMBA YA WAGENI.

    ReplyDelete
  17. Achana naye huy kwan hn urafiki wa kwel,wema ww mshukur mungu kwa kila jambo.

    ReplyDelete
  18. KAJALA JUST ENDELEA NA LIFE YAKO WACHANA NA HUYO DRAMA QUEEN

    ReplyDelete
  19. WEMA IS A DRAMA QUEEN N CHECKI VILE MASHABIKIN WA WEMA WASHABIKIA UJINGA TUUU NA KUTUKANANA JAMANI...

    ReplyDelete
  20. utafkiri mwalipwa hizo team am simu mwanunuliwa kazi za maana hamuna ingekua munazo musingekea mwatukanana na kushabikia ujinga na upumbavu

    ReplyDelete
  21. tumechoka na mabo zenu za kipumbavu na hawa wana habari tuwekeeni mambo ya maana c mabo za kipumbavu mara wema asamehe mara wateta mara wapokonyana waumee mambo gani hayo sasa dis is shit men

    ReplyDelete
  22. kila unaposema matusi ujue wapata dhambi sasa faida gani mutukanane kwa mambo yasowahusu na matusi ya saidia nn

    ReplyDelete
  23. Kwa haraka haraka historia inaonyesha Kajala na Wema wanatoka katika familia mbili tofauti na zenye mtizamo tofauti. Wema anaonekana ana ustawi zaidi ya Kajala kwa sababu yeye anatokana na ile familia ya kwenye tabaka la Utawala/Viongozi wa Nchi wakati yeye Kajala anatokea kwenye ile familia ya kwenye tabaka la chini yaani either familia yake ni wakulima au wafanyakazi wa kawaida. Lakini historia inavyoonyesha ni kuwa Wazazi wa Kajala walikuwa Polisi pale kwenye Kituo cha Oysterbay. Kwa mtizamo huo na kama ilivyokuwa adha ya Binadamu wengi ni kuwa Kajala anakuwa mnyonge kwa Wema Sepetu. Hizo tofauti za ki familia na malezi zinamfanya Kajala aendeleee kuwa mnyonge na tegemezi kwa Wema Sepetu ambaye anatokea tabaka la juu la watawala. Sasa basi kwa mtizamo wa haraka haraka ni juu ya Kajala kufanya juhudi maalum na mahususi za kujinasua kutoka katika hali hiyo. Na zipo namna nyingi na sahihi za kujinasua kama vile kwenda Shule kufanya kazi kwa bidiii na kufanya mambo yale muhimu katika maisha ambayo yatamuweka katika mustakabali mzuri na kumuweka pale juu kama Kajala na sio yule Kajala aliyetokea kwenye familia duni ambayo Baba na Mama ni ma polisi wanaowalinda viongozi wa Nchi tabaka ambalo Wema Sepetu ndio anatokea. Kuendelea kufanya ushindani na Wema haitamsaidia sana kwani ni sawasawa na vita ya panzi na kunguru. Kuendekeza Urafiki na Wema pia haitamsaidia sana kwa sababu ya tofauti za matabaka Wema hawezi kukubali Kajala awe sawa na yeye au zaidi yake kwani hiyo ni mentality ya kawaida ya Binadamu kati ya aliyekuwa nacho na ambaye hana. Cha msingi hapa ni Kajala jitahidi kujiepusha kwa namna yoyote na Wema na shika yako. Nenda kaendeleze lile gurudumu la Maendeleo yako ili na wewe uje kuwa mtu katika watu. Achana na Wema. Kwa sasa hivi hutamuweza. Ni mpaka pale tu utakapokuwa na mafanikio kumzidi yeye. Na hilo linawezekana. Cha msingi ni kutokata tamaa na maisha. Kwani Wema anachojivunia kwa sasa ni zile juhudi zilizofanywa na Wazazi wake kumfikisha hapo alipo. Otherwise hakuna kingine.
    Na hili liwe fundisho kwa Watu wote wanaotoka matabaka ya chini na kujiendekeza kufanya Urafiki na wale wanaotoka matabaka ya juu kwa kudhani itawasaidia sana kuwapandisha kutoka pale walipo. Jitahidini na mambo yenu. Hizo tofauti za matabaka ni balaaaa.

    ReplyDelete
  24. Na pia ukimuangalia sana huyo Wema Sepetu anawachezea wasichana hao hao ambao wametoka katika hayo matabaka ya chini na ya Kimaskini. Sijui Kajala na Aunt Ezekiel. Humuoni akiwagusa wale wasichana wanaotoka katika yale matabaka ya aina yake kwa sababu anajua kwanza hawana muda naye wa kumuendekeza na pili akiwafuata hovyo hovyo watamchana chana hawatamuacha hivi hivi tu.

    ReplyDelete
  25. PIA MKUMBUKE KUMPA USIA,ASIJIONE BADO MDOGO,KUCHUKUA WANAUME WA WATU HOVYO,KWA KUDHANI NDIO ATATOKA,MTOTO WAKE AMECHAKUWA MKUBWA,MWISHO ATAJIKUTA NA BWANA WA MTOTO WAKE,PIA ASISAHAU KWA ALIYOMFANYIA MWENZIE,KUWA ATAYASAHAU KIRAHISI KAMA ALIVYOTEGEMEA,HAKUNA BINADAMU MWENYE MOYO WA HIVYO,ATAKUSAMEHE MACHONI,LKN MOYONI ATABAKI NA VIULIZO VINGI,UKIZINGATIA WEMA ALIKAA NA KAJALA KAMA NDUGU YAKE,NGUO ALIMNUNULIA,VIATU,MAPOCHI,NK,KUMBE KAJALA ALIKUWA ANATAMANI MAISHA YALE YA MWENZIE,SASA WEMA ALIVYORUDI KWA DIAMOND MATUMIZI YA HELA YAKAPUNGUA HAPO NDIPO KAJALA ULIPOKOSEA,KUTOKA NDUKI KWENDA KUJIWEKA KWA CK,ILIMURADI TU MATANUZI YAENDELEE,SASA ULICHOKIPATA HAKUNA,URAFIKI HAUPO TENA,UMEBAKI NA AIBU,USIONE WATU WANAJARIBU KUKUTETEA,LKN WAKIJARIBU KUVAA VIATU VYA WEMA,HAKUNA HATA MMOJA KATI YETU ATAKAYEWEZA KUWA NA RAFIKI WA AINA YAKO,HAWEZI KUWA KARIBU NA WEWE TENA,MAANA ANAOGOPA KAMA ULIFANYA HILO ULILOLIFANYA,HUTASHINDWA KUMFANYIA BAYA ZAIDI YA HILO,HUO NDIO UKWELI,UKATAE,UKUBALI,MATANUZI YANA MWISHO,LKN UTU UTABAKI PALEPALE,HATA UKIFA JINA LAKO LITABAKI TU,HIVYO KAJALA JICHUNGUZE JE UKO SAWA,HAKUNA MKAMILIFU,LKN DHAHIRI,SHAIRI,INAONEKANA UNA MAPUNGUFU MAKUBWA,MOYO WAKO UMETAWALIWA NA TAMAA,SASA NI WKT WAKO WA KUJICHUNGUZA,MAANA UMRI UMEKWENDA,UTATEGEMEA KWENDA KUJIUZA CHINA MPAKA LINI,

    ReplyDelete
    Replies
    1. Inawezekana kwa kile unchojaribu kukitafsiri juu ya tabia na hulka za mlengwa ambaye ni Kajala. Hatuwezi kujua ni msukumo gani alioupata wa kufanya kile kinachosemekana kumuibia Wema bwana wake. Huwezi kujua ni kwa nini hasa ukizingatia huyu ni yule msichana anayetoka katika lile tabaka la chini la walalahoi. Sasa watu kutoka katika tabaka la aina hii huwa wanakutana na changamoto nyingi sana katika maisha yao kiasi cha kwamba kwa namna moja ama nyingine huja kuziathiri zile tabia na hulka zao kwa ujumla. Huyo mwanaume ambaye amekuwa akitajwa tajwa kama ndio chanzo cha ugomvi huo ni aina ya wale Wanaume ambao wamekuwa wakitumia udhaifu huo hasa kwa wasichana kutoka hilo tabaka la chini na kuwatumia vibaya na hata kuwadhalilisha sana. Ukiangalia kwa undani sana utaona Kajala anadondokea kwenye hilo kundi la waathirika kutoka katika hilo tabaka la chini na walalahoi. Kimsingi inawezekana kabisa kwa mazingira aliyomo Kajala asiwe mtu wa kulaumiwa sana kwa janga zaidi ya kumlaumu huyo mwanaume ambaye ametumia udhaifu aliokuwa nao Kajala kumuingiza katika huo mtego. Ni lazima ikumbukwe ya kuwa suala la tabia na hulka sio lazima sana lihusishe matabaka ya watu. Tabia kama vile za Majivuno Majigambo Kejeli na Madharau kwa watu wengine ni tabia ambazo zinaweza kutoka katika tabaka lolote liwe la juu walionacho ama tabaka lile la chini la walalahoi wasiokuwanacho. Kwani kumbukumbu zinaonyesha kuwa hata huyo Wema wakati yuko kwenye mahusiano ya mapenzi na huyo bwana ni kuwa huyo bwana alikuwa katika Ndoa yake. Na Wema alikuwa analijua hilo kuwa yuko na mme wa mtu. Sasa hapo sijui unaweza kuja na hoja gani ya kimsingi ya kumtetea.
      Acheni ushabiki pale mnapoona mtu anaathirika. Kitu cha msingi ni kuuweka wazi ukweli wa mambo bila kupindisha lugha wala ukweli. Wala kumlaumu Kajala kwa sababu tu ya unyonge wake based on her background haitasaidia sana. Huyo Wema kimsingi anachokifanya ni kutumia ile nafasi aliyokuwa nayo na hilo jina kumdidimiza na kumdhalilisha mtu asiyekuwanacho. Sijui yule Mke halali wa yule Mwanaume sijui yeye kwa wakati huu atakuwa anasema nini kuhusu Wema kwa sababu alisabibisha kuvunjika kwa Ndoa yake.Na si hayo tu kwani ni pamoja na kuwa huyo Wema kusabibisha maumivu makali ya watoto aliozaa nao na huyo aliyekuwa bwana wake.

      Delete
  26. Ndugu Admin. Unajua kabisa hii Blog ni Blog aminia. Ni Blog ambayo haminyiminyi maoni ya watu kama hizo Blog nyingine uchwara. Lakini sijui imekuwaje na wewe umeamua kufuata mkumbo wa kuminya maoni ya watu wengine kama hizo Blog nyingine uchwara. That's unfair.

    ReplyDelete
  27. mwaandika barua salala mhhh angekua atoka familia ya utajiri angekua akirombeza na ck matajirini ni kama bahressa wema nn mbele yao mcheeew andikeni gazeti yenu kumsifia wema na domo tuuuuuu. na mtukaneni kajala mwanae mwacheni hayamhusu kabisa mulokosa heshima.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hizo post ndio umeziona za maana mxewwwwwwwwww

      Delete
  28. Wema Ana lolote eti ametoka familia za uongozi, uongozi bongo na uongozi wenyewe WA mwaka 47, ujinga mtupu. kumsaidia mtu c mpaka matangazo hata mungu apendi, ukimsaidia mtu c mpaka ujitangaze kweny magazeti. Hiyo wema ulitoa ili usafishe jina na uzidi kupatA mabwana. Wema olin'janga muno, ne minwangali. Watamiraaaaaa engataaa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad