YATISHA: Kijana afyatuka, Amuua mtoto wa Miaka 9 na ‘Kutafuna Ubongo’ Kisha Kujikata Uume
7
July 18, 2014
Moshi. Mkazi mmoja wa Moshi amemuua mwanafunzi wa darasa la 3 kule Samanga leo na kisha 'kula ubongo' wa mtoto huyo katika tukio la kutisha lililostua wakazi wa mji huu.
Kijana huyu aliyefahamika kwa jina la Lawrence Mramba, 20, alimshambulia mtoto huyo mwenye umri wa miaka 9 kwa panga wakati akienda shule mnamo saa 1 asubuhi Ijumaa, akampasua kichwa na kisha akaanza kutafuna ‘vipande vya ubongo wake.’
Mara baada ya kitendo hicho cha kushtusha, Mramba, aliyeonekana kuwa na matatizo ya akili, alianza kujikatakata sehemu zake za siri na wembe, huku akitafuna vipande vya mwili wake mwenyewe, kimoja baada ya kingine.
Baadhi ya mashuhuda wanadai kijana huyo ‘alionyesha kuwa na nguvu za ajabu’, huku wanakijiji wenzake wakishindwa kabisa kumdhibiti.
Wengi walilazimika kuketi kando wakimtazama jinsi anavyojikata wakishindwa kujua cha kufanya.
Iliwabidi polisi waingilie kati sakata hilo na hatimaye wakifanikiwa kumthibiti kijana huyo.
Hata hivyo, Mramba alifariki dunia muda mfupi baadaye katika hospitali ya Kilema wakati akipewa matibabu ya dharura kutokana na kupoteza damu nyingi.
duuh moshi kama watu wa bara sikuhizi kuuana tuuu
ReplyDeletewee bweeegee nini? lini umesikia habari kama hii.acha kushoboka
DeleteInauma sana jaman
ReplyDeletemmm inatisha
ReplyDeleteNimekupendaje mdau 9:42am
ReplyDeleteDuuuuuu
ReplyDeleteHivi kumbe Moshi ni pwani siku hizi? Aisée poleni sana wafiwa
ReplyDelete