Aibu! Aunt Ezekiel Anusurika KUPIGWA Baada ya Kufumaniwa na Mume wa Mtu

Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson anadaiwa kukinukisha nyumbani kwa Wema Isaac Sepetu baada ya kunusurika kufumaniwa na mume wa mtu, Moses Peter Iyobo a.k.a Moze Iyobo ambaye ni densa wa Nasibu Abdul ‘Diamond’.

Habari zisizokuwa na shaka zinadai kwamba tukio hilo lilijiri Jumapili iliyopita nyumbani kwa Wema, Kijitonyama, Dar ambapo Aunt alisababisha tafrani iliyosababishwa na mke wa mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina la Mwengi Ally.

Kwa mujibu wa mashuhuda wetu waliokuwa wakizungumza kwa kupokezana, Mwengi alidai kwamba Aunt amekuwa akitembea na mumewe huyo hivyo timbwili lilianzia nyumbani kwa Aunt, Mwananyamala A jijini Dar.

Ilidaiwa kwamba, huku Aunt akiwa hajui hili wala lile, ghafla waliibuka wasichana saba na kumuanzishia mwigizaji huyo.Mashuhuda hao walidadavua kwamba katika kujinusuru na kipigo ambacho alihisi akiwa peke yake, angeumizwa Aunt alikimbilia  nyumbani kwa shoga yake, Wema.

Ilidaiwa kwamba wasichana hao hawakuishia hapo kwani walimkimbiza Aunt hadi wakamuona akiingia kwa Wema ambapo walipofika getini walikutana na meneja wa msanii wa Bongo Fleva, aitwaye Mirrow, Petit Man ambaye walimuomba amtoe Aunt ili wamshikishe adabu ajifunze kukaa mbali na waume za watu.

Ilisemekana kwamba katika tafrani hiyo getini, Wema alitoka na msichana wake aitwaye Careen lakini Aunt hakutoka ambapo waliwaambia wasichana hao kuwa Aunt hawezi kutoka na isitoshe wa kulaumiwa ni Moze Iyobo kwani yeye ndiye anayedaiwa kumtongoza Aunt na kuanza kuchati naye hadi mkewe akanasa meseji zao za mapenzi.

Baada ya kujazwa data hizo, Mwandishi alimtafuta Mwengi ili kupata maelezo ya kina kuhusiana na ishu hiyo ambapo alikiri kwenda kwa Aunt na Wema lakini hakufanikiwa kumpata Aunt kwani kama angemkamata, maafa yangetokea.Mwengi alisema kuwa siku ya tukio aliitwa na Aunt maeneo ya Mlimani City, Dar na akamwambia aende na mtoto akamfanyie shopping.

Alisema baada ya kuambiwa hivyo hakuwa na hiyana kwani alijua kuwa ni kama mama yake mkubwa na shoga wa mpenzi wa baba yake mkubwa ambaye ni Diamond, kumbe nyuma ya pazia kulikuwa kuna kitu kingine kimejificha.“Niliporudi nyumbani, mume wangu aliniambia nimpige picha kwa kutumia simu yake, nilipoifungua ndipo ikaingia meseji kutoka kwa Aunt.

“Nilipoisoma ile meseji nikagundua kuwa walianza kuchati muda mrefu kuhusu mapenzi yao, ndipo nikakusanya jeshi langu na kumfuata nyumbani kwake nikamshikishe adabu, amshukuru Wema kumficha maana sipati picha kwa jambo ambalo lingetokea. Ingekuwa mwisho wake wa kupora waume za watu,” alisema Mwengi.

Alipotafutwa Aunt na kuulizwa juu ya sakata hilo, alijibu kwa kifupi: “Sina muda mchafu wa kuongea halafu nimelala, kwa sasa niache nipumzike.”

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HIVI NYIE MODS BILA WEMA,,DIAMOND NA HUYU AUNTY KWANI KIBLOG CHENU HAKISOMEKI,LETENI HABARI NYINGINE NA SI ZA HAWA VIUMBE,MBONA TULIKUWA TUMEPUMZIKA SIKU MBILI HIZI.

    ReplyDelete
  2. We Wema bila wewe nisingewajua Martin kadinda na petit man,Hivi wanakulipa?

    ReplyDelete
  3. Bila Wema umu blog ainogi Kabisaaaaaa

    ReplyDelete
  4. Kukaa mbali kote na bwana wake kumbe ni ufuska anajua akikaa naye kule uarabuni hawezi kuendeleza ufuska wake. Hao ndio mademu wa Tandale na ile nyumba ya Wema ni kama danguro tu.

    ReplyDelete
  5. Breaking newssssss!!!!!!! Mtoto Wa kiume Wa ......kakamatwa livelive china Na madawa ya ....,,

    ReplyDelete
  6. Aunt kama vile Una gundu na wanaume, aisee na ustaa wote huo unaidhi maana? Ina maana hata kuishi angalao Sinza Ni olaaaa...... Unadanganya umeolewa ndoa gani hiyo ya? Labda ya kufikoirika..... Then dansa WA Diamond mbona Ni vitoto? Poleeeee ogea maji ya bahati may be gundu litakutokaaa

    ReplyDelete
    Replies

    1. Mdau hapo juu,siku zote binadamu ukijithamini utathaminiwa na kuogopwa kinidhamu,
      kwa mtazamo wako tu,unadhani dansa wa Diamond anaweza kumtongoza Lady
      J,dee?Nadhani umenielewa.

      Delete
  7. Huyu Aunt dah ni malaya tu. Sasa ndoa yake imemshinda anabakia kupiga umalaya pale mjini na vitoto. Awaachie watu ndoa yao watunze watoto wao kwa amani. Hata haya huna malaya wewe. Ndio maana ulipigwa na chupa tulifikiria umesingiziwa kumbe ndio zako fuska mkubwa weeee

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad