Anayezuia Mijadala Amepoteza Sifa za Uongozi Kama Ana Nia ya Kugombea Urais Imekula Kwake

Aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole amesema makongamano na mijadala inayohusu Katiba mpya yataendelea kwa sababu ni ya lazima pia ni haki ya kikatiba.

Akizungumza kwenye Kongamano la Katiba lilioandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) jana, Polepole alisema mtu anayezuia wananchi kuendelea kuzungumzia Katiba amepoteza sifa za kuwa kiongozi wa nchi.

Huku akishangiliwa na washiriki wa kongamano hilo, Polepole alisema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi ya kidemokrasia, inayoheshimu haki za binadamu na utawala wa kiraia. Hivyo inashangaza kusikia kuna kiongozi anajaribu kuwafunga mdomo wananchi.

“Nimesikia mtu mmoja anasema msifanye makongamano. Sijamfahamu vizuri, lakini ninachokiona ni kwamba anaendelea kupoteza sifa za kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kama alikuwa anataka kufanya hivyo,” alisema Polepole.

Ingawa hakumtaja jina, juzi Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi hivi karibuni walikaririwa wakihoji uhalali wa mijadala inayoendelea sasa kuhusu Katiba Mpya.

Sitta, akiongoza kikao cha Bunge la Katiba juzi, alimtaka Waziri wa Habari na Utamaduni kuvichunguza vyombo vya habari vinavyorusha matangazo ya watu aliodai wanapotosha ukweli kuhusu Katiba.

Ingawa Sitta hakukitaja chombo chochote, alikuwa akielekeza maoni yake kwenye mdahalo uliorushwa Jumatatu wakati wajumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, wakiongozwa na Jaji Joseph Warioba waliposhiriki na kujibu hoja mbalimbali zinazoonekana kuwa na utata kwenye Rasimu ya Katiba.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hivyo mnavyoendelea kujadili nje ya bunge mnasaidia nini? Au kwa vile midomo mali yenu na hamuingizi vocha kabla ya kuzungumza, ndio basi tena!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. kaulizane na katiba hilo swali lako la kijinga.

      Delete
  2. nyinyi viongoz mzee kigogo himself (warioba) atawashushia laana nzito

    ReplyDelete
  3. Wanasaidia sana sababu watu wengine tunapata kujua mabaya yenu nyie ccm wala haki za wanyonge hicho ndicho mnacho kiogopa na hakuna chengine .......na mabaya yenu yanaanikwa....sasa kama ulikua hujui watu inawasaidia nini habari nado hiyooooooooo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad