Kama sehemu ya vyanzo vyako vya habari ni mitandao kama vile website, blogs, facebook, twitter na Instagram inawezekana hii stori ya Gwajima ambae ni Muhubiri wa Injili kununua Helikopta uliiona hata zaidi ya mara moja.
Hata hivyo Muhubiri mwenzake Askofu Zacharia Kakobe Aug 10 2014 amenukuliwa na gazeti la Nyakati na kuizungumzia hiyo Helikopta akisema ‘kitendo cha Gwajima kununua helikopta kwa ajili ya kazi zake za Injili kinastahili kufurahiwa na Wakristo wote wa kweli, tujifunze kupongezana.. nampongeza sana’
‘Kumiliki kwake Helikopta kutachangia katika kufuta dhana potofu ambayo imedumu kwa muda mrefu ya kuyaita Makanisa ya kilokole…. makanisa ya vichochoroni, Helikopta sio starehe na hata muundo wake sio wa starehe bali ni kazi, itamwezesha pia kufika maeneo ambayo gari sio rahisi kumfikisha kutoa neno la Mungu’ – Kakobe
Kuhusu Askofu Kakobe kununua Helikopta yake, amesema >>> ‘mimi sio mtu wa mashindano na pia kila mtu anakwenda sawa kutokana na ono aliloitiwa, haya sio mambo ya kushindana… hicho ndicho kinacholeta shida mara kwa mara, Gwajima ana Helikopta ni kwa manufaa ya Ufalme wa Mungu, mimi nina chakwangu ni kwa utukufu wa Mungu, hakuna haja ya kuigana’
Kwanza Gwajima hajanunua na hana fedha hiyo, amepewa kama shukrani kutoka katika familia Fulani ya kitajiri huko Japan ambapo alikuwa kwenye mkutano na alipoombea wagonjwa mbali mbali kati ya wagonjwa waliopata muujiza wa uponyaji ni kijana wao hao matajiri. Alikuwa na ugonjwa wa cancer! Na kupitia mtumishi Gwajima, Mungu wa Israel akamponya!
ReplyDeleteMuache habari za uzushi "Gwajima kanunua"
Mungu ashuki kwa mzinzi Acha kujizushia umepinya cancer.
DeleteNitashangaa sana kuona Mchungaji mwenye ushindani kwenye material things, badala ya ushindani na shetani kumnyanganya mateka na kupeleka kwa Yesu! Hiyo ndiyo kazi ya wanafunzi wote wa Yesu! Zingine mbwembwe!
ReplyDeleteMsiongee utumbo hakuna anaeponyesha hao wote matapeli na Yesu atakuja kuwakana mnaosema mnatoa Majini na kutibu kwa jina lake.
ReplyDeleteYakikukuta utamtafuta huyo Yesu unayemtukana leo. Tumeona wengi waliobeza habari njema za Yesu baada ya madaktari kushindwa walimtafuta Dkt wa madokta Yesu.
DeleteMdau hajamkashifu Yesu,anakashifu uzinzi Wa hawo mbulula
DeleteYes ni jibu!
ReplyDeleteyesu ndio jibu na kimbilio langu nimuogope nani? ukiwa na yesu full amani.anafanya njia pasipokua na njia.
ReplyDelete