Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Baby Joseph Madaha amenusurika kubakwa nchini Kenya baada ya kupanda jukwaani akiwa ametinga kivazi cha nusu utupu.
Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita katika mji wa Naivasha uliopo Nairobi nchini humo ambapo mwanadada huyo alipopanda jukwaani akiwa amevaa sketi fupi iliyokuwa imeacha sehemu kubwa ya mapaja wazi, wanaume wakware walianza kumvutia chini kwa nguvu.
“Nusura Baby Madaha abakwe, wanaume wakware walishindwa kuvumilia, palepale jukwaani wakaanza kumvuta huku wengine wakimng’ang’ania paja lake lakini aliokolewa na mabaunsa vinginevyo tungekuwa tunaongea mengine,” kilisema chanzo.
Baby Madaha Anusurika Kubakwa Baada ya Kupanda Jukwaani Akiwa na Kivazi Cha Nusu Uchi
1
August 16, 2014
Tags
muke ya meneja joe..hahah
ReplyDelete