Mwenyekiti wa Bongo Movie Tanzania Steve Nyerere amefunguka na kuweka wazi kuwa katika Tasnia ya filamu Tanzania hakuna muigizaji wa kiume mwenye tabia za kishoga,Steve amesema hayo leo alipokuwa katika kipindi cha Power Jams
ya East Africa Radio leo alipokuwa akielezea changamoto alizokutana nazo wakati akichat Live kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live kinachofanyika kila siku ya Jumatano kuanzia saa sita mchana.
Steve amewataka watanzania kuwa na uzalendo na kuthamini wasaniii wa nyumbani na kazi zao na sio kuwapakazia na kuwaharibia sifa zao kwa maneno machafu na kuwapakazia mambo yasiyokuwa na ukweli ndani yake,Steve alisema hayo pale alipokuwa akijibu swali la moja ya shabiki wa ukurasa wa Facebook wa EATV.