Bunge la Katiba Kufuru, Wateketeza Mamilion Kwenye Kikombe cha Chai na Biskuti Licha ya Kwamba Wanapokea Posho

Gazeti la Mtanzania August 28 2014 ndio limeripoti hii stori kuhusu Bunge la Katiba linaloendelea Dodoma, kikubwa ni gharama mbalimbali zinazotumiwa na Wajumbe.
Wameandika bunge la katiba lateketeza mamilioni ya fedha ambapo kikombe cha chai na biskuti au karanga kinalipiwa shilingi elfu 10 kila siku kwa kila Mjumbe mmoja licha ya kwamba kila Mjumbe anapokea posho ya siku ambayo ni laki mbili na elfu 30.
Kwenye sentensi ya pili wameandika, chakula cha mchana kila Mjumbe analipiwa elfu 16 kwa siku ambapo kwa siku hiyohiyo iendayo kwa Mungu, ni shilingi milioni 8 hulipwa kama gharama za ukumbi wa kufanyia mikutano.
Una chochote cha kusema kutokana na hili?

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nakatiba still hakuna Mungu awarehemu enyi viongozi

    ReplyDelete
  2. Watu waliochaguliwa ni watanzania halisi njaa kali lazima watoe hasira!

    ReplyDelete
  3. yana mwisho hayo na mwisho wake utakuwa mbaya sana upande wao

    ReplyDelete
  4. Ni zaidi ya ufisadi dhidi ya wanyonge waliowengi

    ReplyDelete
  5. hayana tofauti na mamchwa!! yanakula tu bila huruma!!!

    ReplyDelete
  6. Ccm oyeeee! na mbaki madarakani milele nawependa sana, uncle wangu yupo bunge hilo ndo maana anamalizia nyumba yake fasta na bungeni hakai sana.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad