Clouds FM Yapewa Onyo na Kupigwa Fine Kwa Kukiuka Kanuni za Utangazaji

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imetoa onyo pamoja na kutoza faini ya takribani Sh milioni 5 kwa kituo cha redio na televisheni cha Clouds, kwa kukiuka kanuni za utangazaji za mwaka 2005. 

Wakielezea uamuzi huo jana jijini Dar es Salaam, Kamati ya Maudhui ya mamlaka hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Margaret Munyagi ilisema kuwa ukiukwaji wa kanuni hizo ulifanywa kwa nyakati tofauti na vituo hivyo.

Alisema kwa upande wa kituo cha redio cha Clouds, kupitia kipindi chake cha ‘Njia Panda’ kilichorushwa hewani Juni 15 mwaka huu kati ya saa 8.00 mchana na saa 10.00 jioni kilikuwa na mada iliyohusu safari ya kuzimu ambapo maudhui yake yalijaa simulizi za kufikirika, za kishirikina na kichawi.

Aidha alisema kosa lingine kituo hicho hakikufuata kanuni za Utangazaji(maudhui) za mwaka 2005 zinazowataka kuwasilisha ratiba ya vipindi vyao kwa TCRA ili viidhinishwe na vilevile kuvichapisha katika gazeti kabla ya kurushwa hewani ambapo kipindi cha Njia Panda hakikuwasilishwa kwa ajili ya kuidhinishwa.

Wakati huo huo, kituo cha televisheni cha Clouds kilirusha kipindi cha ‘Bibi Bomba’ Mei 16 na Juni 6 mwaka huu kati ya saa 3.00 na saa 4.00 usiku ambacho kilikiuka kanuni za Utangazaji (maudhui) za mwaka 2005.

Alisema kipindi hicho kilidhalilisha mabibi hao walioshiriki pamoja na wanawake kwa ujumla kutokana na maswali ya aibu waliyokuwa wakiulizwa na waamuzi wa shindano hilo ambayo ni kinyume na kanuni hizo.

Aidha alisema kituo hicho kinatozwa faini ya Sh milioni moja na kutakiwa kuwasilisha TCRA mwongozo wa kuchuja na kusimamia maudhui yasiyofaa kabla ya kutangazwa.

TCRA imesema kama Kanuni za Utangazaji zitaendelea kukiukwa hatua kali zaidi za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Clouds hawajasoma jamani kwahiyo bora TCRA muwe macho nao. Hao watu ni makanjanja walipotilza. Vipindi vyao vinaongozwa na mob hakuna utashi wala weledi

    ReplyDelete
  2. hao TCRA awana lolote.wanataka ela tu naic kile kipindi cha njia panda jamaa alivyokuwa anatka kuyataja majina ya watu wakubwa tena na wengine wa serikali moves na music ambao aliwaona kuzimu watakuwa waliongopa maana nao watakuwa nimiongoni mwa wao ila na kuhusu bib bomba nimekifatiliakipindi vizuri tu ila cjaona kama kinawazalilisha mabibi bali kinawapa mabibi upeo wa maisha zaidi kama wanataka hela wawaombe tu na cyo kusema vimekiuka kanuni..... na hapaTZ akuna redio inayopendwa na watu wengi kama clounds na ndo maana kila leo wanazidi kupinga atua mda mfupi ulopita ilitangazwa kama imeshika nafac ya saba kati ya redio 20 Africa nzima sasa angalia afrika kuna redio ngapi ila yenyew ipo kwenye position nzuri tu ebu wa iache radio ya watu bwan

    ReplyDelete
  3. Et hakuna radio inayopendwa na watu kama clouds!!!!!!!..

    ReplyDelete
  4. haijui radio tanzania huyo.

    ReplyDelete
  5. nyie ndo amjui redio nisha sema kama wew ndo uipendi na familia yako wengine wanaipenda

    ReplyDelete
  6. Clouds ina vipindi vizuri ila baadhi ya watangazaji wake ndo makuma... akina mchomvu, wana mambo ya kisenge watu wenywewe wametoka poorini huko dar wamekanyaga 2005 wanajiona wajaaaaanja kumbe mambwiga tu!!

    ReplyDelete
  7. clounds ndo redio bora hapa Tz

    ReplyDelete
  8. clounds ndo redio bora hapa Tz

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad