Devera wa Basi la Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA) ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja, amejikuta akipewa kibanokizito na askari wa usalama barabarani ‘trafiki’ baada ya kuleta ubabe wakati alipotakiwa kutii sheria bila shuruti.
Tukio hilo la aina yake lililosababisha usumbufu kwa abiria wa basi hilo, lilitokea juzi Bamaga-Mwenge jijini Dar kufuatia dereva huyo kukataa kuegesha pembeni basi hilo lenye namba za usajili T 619 CVP lililokuwa limevunja sheria ya usalama barabarani.
Imedaiwa kuwa, basi hilo lilishusha abiria kinyume na sheria kwenye kituo kisicho rasmi maeneo ya Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama, Barabara ya Shekilango.
Chanzo makini kilichoshuhudia tukio hilo kimedai kuwa, kufuatia hali hiyo ndipo trafiki hao watatu walio makini na kazi yao, walilisimamisha basi hilo ili kumsomea mashitaka dereva huyo sambamba na kondakta wake lakini wakaleta ubishi na kutoa lugha chafu kitendo ambacho trafiki hao walishindwa kukivumilia.
“Waliendelea kutoa lugha chafu, hawakuonesha kutii amri ili waambiwe walichokosea ndipo trafiki wakalazimika kuwadhibiti kwa kuwafunga pingu baada ya kukataa kutii sheria bila shuruti, tunawapongeza trafiki hawa kwa kuwataiti,” kilisema chanzo hicho.
Siku za hivi karibuni kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi kwamba, madereva wa mabasi ya Uda wamekuwa wakivunja sana sheria kama wao wako juu ya sheria kuliko madereva wengine.
Walimsimamisha kumsomea mashtaka kwani wao ni mahakimu?
ReplyDeleteMatraffic watatu basi moja ujue ni rushwa tupu! Ndiyo sababu walijibiwa vibaya!
Kama ana kosa kamata peleka polisi kama Kibonde!
Hivi serikali imeacha kulipa mishahara traffic nadhani!
Kama kuna taasisi inafanya kazi kwa bidii nchini ni traffic! Mishahara minono sana pale barabarani