Fahamu Kiwango Kipya Anacholipwa Diamond Kwa Show Moja ya Mziki Hapa Tanzania

Tangu mwaka juzi tulifahamu kuwa Diamond Platinumz ndiye msanii wa Tanzania anaelipwa kiasi kikubwa cha pesa, na mwaka jana ikaelezwa kuwa bila milioni 10 au 8 za Kitanzania humpati kwenye show yako.

Lakini kiwango kipya kilichotajwa jana kitawapa kizunguzungu zaidi hasa mapromota wenye mitaji midogo wenye ndoto za kufanya kazi na mwimbaji huyo.

Kwa mujibu wa, Babu Tale ambaye ni meneja wake, hivi sasa kiwango cha chini anachochaji kwa show moja hapa nchini ni $15,000 (sawa na shilingi Milioni 25 za Tanzania).

“Tuna show Marekani show kumi na tano (15), show kumi na tano dola elfu ngapi? Na kwa hapa Tanzania hatufanyi show chini ya dola e15,000.”  Babu Tale aliiambia Bongo5.

Kwa mujibu wa Babu Tale, wanachaji kiasi cha hadi dola 25,000 kwa show moja za nje ya nchi (ikiwemo Marekani).

“Tunalipwa milioni 20 show moja, tunalipwa dola elfu 25,000 show moja, hii ni zaidi ya madawa ya kulevya.” Alisema wakati akikanusha tuhuma kuwa Diamond anauza dawa za kulevya.

Kwa mahesabu ya haraka haraka, shows 15 mara dola 25,000 ni sawa na  $375,000 (Sawa na shilingi za Tanzania 625,687,500).

Yesss! Ni zaidi ya Milioni mia sita ishirini na tano za kitanzania.

Kama ni kweli, basi Diamond anastahili kweli kuitwa Dangote wa Bongo Flava.

Bado michongo inaendelea kumiminika ambapo hivi karibuni meneja wa Trey Songz alimtumia ujumbe kuwa atakapokuwa na nafasi amshitue waongee.

Post a Comment

34 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ndiyo maana nasema, tumepata Michael Jacskon mpya TZ!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. What???????????????? Wacko Jacko alikuwa analipwa Dollar elfu 15??????????

      Delete
  2. INA MAANA HUYU DOMO ANAMZIDI YULE MSANII WA KWENYE MEDIA MWENYE VOKO NZULI MALIPO AU BABU TALE KADANGANYA?

    ReplyDelete
    Replies
    1. voko kali is not a music or quality of music

      Delete
  3. Ndoto za abunuasi! Uongo mtupu! Ni njia ya kukwepa tuhuma za madawa. Jipangeni kicjenuka!

    ReplyDelete
  4. my number one my sweety sweety ma number one sweeety sweety, ndo babu tale anatueleza!!

    ReplyDelete
  5. umeonaeeeee,wanakwepa tuhuma za madawa ya kulevya,relaxxxxxxxxxxxxxxxxx babu tele,hakuna marefu yasiyo na ncha,ipo siku ukweli tutaupata,mziki wa kibongo ulipe kiasi hicho?nyooooo,uongo mtupuuuuuu,kuna ya ziada,na ya ziada si lazima yawe madawa ya kulevya.so relaxxxx

    ReplyDelete
    Replies
    1. bila shaka utakuwa mingoni ant-businessman, kwaliothubutu biashara wana mawazo tofauti!

      Delete
  6. nani akulipe hizo dolari marekani babuuuu!!! kwa nyimbo zipi? sijasema domo hana nyimbo nzuri, lahasha anazo sana lakini hapana kwa kiasi hicho badoooo saanaaaa!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. kwasababu huamini.... jaribu kwenye kazi zako

      Delete
  7. WANA WIVU HAO HAOOOOO HAOO NA BADO

    ReplyDelete
  8. tuna wivu cc !! cccc!!!! wakitugani cc!!!cccc? hatujuiiii ccc!!! cccccc!!!!

    ReplyDelete
  9. Ndio maana wa bongo hatufiki mbali tunachukiana wenyewe kwa wenyewe na kama angekuwa msanii kutoka nje ungeona watu watavyo msifu,lazima tupende vya kwetu sio kila siku kusifu wa Naigeria tu na wageni wengine mtu kwao na mtu chake mkataa kwao mtumwa...Sorry kama kuna nilie mkera haya ni maoni yangu tu.

    ReplyDelete
  10. HUKO MAREKAN MNAKWENDA KUWAIMBIA WATANZANIA WANAOOSHA WABII NA WENGINE NI WANAFUNZI HIZO DOLA ELFU ISHIRINI NA TANO ZITATOKA WAPI JAMANI?KWANZA WATANZANIA WANAOISHI HUKO WANA MAISHA MAGUMU MNO,KIINGILIO TU MBINDE,ACHENI POROJO;KULE MNAKWENDA KUOSHA MACHO TU;HAKUNA HELA COZ MNAKWENDA KUWABURUDISHA WATANZANIA AMBAO HAWAJARUDI NYUMBAN SIKU NYINGI;NA HAWANA MAISHA MAZURI KIIVYO;KIINGILIO DOLA20;JAMAN MUOGOPEN MUNGU

    ReplyDelete
    Replies
    1. another poor mind!

      Delete
    2. mziki wake uko sehemu kubwa afrika ( west,east, south and some parts of central Africa) so stop arguing as if u can think properly!

      Delete
    3. Uyo mjinga anayesema watanzania walio nchi za nje maskini labda ndugu zake!!! inamaana watu wanashindwa kupata wateja wa dola 50 per head! Wapo watu kibao wanaishi vizuri na wanavibarua vinawalipa vizuri. Acha kuropoka viingilio na sponsors wanatosha kumlipa hiyo pesa na chenji inabaki! akili za kimaskini bwana!!!

      Delete
  11. diamondi ndiye msaniii tajiri hapa tz anaeibisha akajinyonge na kamc.... na kwa maombi ya mashabiki zake pamoja na wale wanaomdic.machoni japo moyoni wanamkubali very soon atakuwa tajiri wa afrika nzima na inawezekana tu akiendelea hivi hivi alivyo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Msanii tajiri?? Msanii tajiri hana hata uwezo wa kununua nyumba maeneo hot cake kama Masaki alafu unasema tajiri? umewahi kuona duniani Star tajiri anatembelea Prado au Toyota??? Je unajua kiwango cha utajiri kinapimwaje????

      Delete
    2. Mind you big mouth ananymous 10 30am August 23. Anaposema msanii tajiri anamlinganisha na wasanii wa kwetu Dar es salaam!! Na kua na property masaki sio njia pekee ya kuonyesha utajiri. Mtu anaweza akanunua property nyingii maeneo tafauti na thamani zinapanda na zikazidi property moja masaki. In addition rich people dont do things to impress people! NENDA KALETE ACCOUNT BALANCE YAKO KAMA UNAWEZA KUTENGENEZA HELA HIZO KWA MDA WA MWAKA! MSSSCH..mapepo ya umaskini tu.

      Delete
    3. Chukua tym pumbavuuuuuu ww, utajiri unaenda na status ww, matajiri wote duniani wanaishi hot cake areas, hata uwe na nyumba 100 tandale kama hauwezi kumiuliki nyumba maeneo hadimu, we ni poor tu.......kama hutaki kajiueeeeeeeeeee

      Delete
  12. Jamani msiumize vchwa si mnajua yupo kwenye dini yake wacheni awe kama yule mchonga pua yeye atachonga mdomo haaa haaa haaa haaa

    ReplyDelete
  13. Jamani msiumize vchwa si mnajua yupo kwenye dini yake wacheni awe kama yule mchonga pua yeye atachonga mdomo haaa haaa haaa haaa

    ReplyDelete
  14. ama kweri 2taenderea kuwa ivi ivi nyie nuhu wario terekezwa ivi domo kama analipwa iyo era davido atalipwa shinfapi angalien nyuma ya pazia mtakuta anauza unga nani gay domo anakazinyingi na huyo msenge anayesema msanii mwenyeera tz na binti machozi ay

    ReplyDelete
  15. shoo $ 5,000, sembe $ 20,000 bonus ndiyo inakamilisha $ 25, 000 dolari!!! babu tela utawadanganya hawahawa mazezeta ambayo hayajawai toka nje ya hii nchi!!! unajua wengi wa watz ambao hawajawahi toka nje ya TZ, bado akili ndogo sana kwahiyo hawajui kinachoendelea duniani, wako gizani kweli masikini!! hata me mwenyewe kabla sijatoka nilikuwa hivyo hivyo, kwahiyo naelewa!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe anonymous 8:03am ni maskini mwingine! unaendaga nchi zanje ila kwa budget kali! jus coz hua hauna pocket money ya kutosha doesn't mean kila mbongo overseas hana!! Kuna watanzania wako vizuri sana! Exposure bila pesa nayo shida!! Shows kama hizo mbona wanalipwa it is very possible kama sponsors na wanunuzi wa ticket wapo.

      Delete
  16. Hakuna asiyejua kama Bob Tale na Fellla ni wauza unga wakubwa Dar es salaam hii, anaebisha atakuwa ni mgeni wa hili jiji. So ishu ya Diamond kuuza unga sio kitu cha ajabu kabisa, kwani huyu dogo yupo karibu sana na wauza wakubwa akiwemo mtoto wa Kingunge Ngombale Mwilu (Kinje). Na huyu Kinje ndo anawaharibu sana hawa vijana wa bongo flava, amewabebesha wengi sana akiwemo marehemu Albert Mangwea. So hii serikali iache unafiki, ianze na vigogo walio kwenye system na sio kuwaandama hawa vijana ambao ni ma supplier wa mwisho tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. We nawewe achaga maneno ya Bar!! Kisa umesikia umbea bar kati ya wanaume unadhani kila kitu ukweli! utafungwa. umeshawaona wakibeba! yaani mtu dar akiwa na pesa unga!! kwanini msiwaze biashara zingine. maongezi na walevi bwana! wanapenda kujipa moyo kwa kukashfu pesa za wenzao. Mbona hamsemi jayz anauza madawa?

      Delete
  17. na wewe unauhakika gani kama ni maneno ya bar? au wewe ni mmojawapo? mtakuja umbuka nyie baada ya 2015!! shauri zenu.

    ReplyDelete
  18. diamondi ni tajiri san acha ajiite dangote wa kibongo ebu angalia anawasomesha watoto wenye.ali ngumu kwenye shule za kimataifa ni msaanii gani hapa bong anaweza rudisha fadhila kwa jamii yake na ndo maana mungu anazidi kumuinua na kumbariki pia kama kuna wasanii hapa bongo wanalipwa kama diamondi na kujitoa kwenye jamii zao bac hata watano awafiki ebu tupende nya kwetu kwa nin mpaka hii karine ya 21 twazindi kutawaliwa tubadilike aisee waTz wezangu

    ReplyDelete
  19. Kwani kuna tatizo wape hesabu zako hao wachunguzi waliopewa kazi ya kuchunguza uhalali wa mapato yako . Hujui kama hayo maelezo meneja wako anayotoa yataakumiza wewe maana utatakiwa uonyeshe kodi ya serikali uliyolipa kwa mapato hayo.

    ReplyDelete
  20. tusubiri top ten ya forbes ya matajiri Tz inayokuja, nadhani atakuwemo kwenye kumi bora, nyie waswahili nini nyie mbona wivu!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad