Fiesta imeandaliwa chini ya uzamini wa bia ya Serengeti (SBL) na Kili Music Tour imedhaminiwa na bia ya
Kilimanjaro (TBL). Wote wanafanya kazi nzuri kwa wasanii wetu, na inawapa ajira na kipato wabongo!!
Swali langu, kwanini msingepeana nafasi mmoja aanze na mwingine amalizie kuliko mnachofanya sasahivi,
huku kuna Fiesta kule kuna Kili Tour??? Ila binafsi ninaona kama mnashindana ambako hakuna sababu
yeyote ile..ni kwa faida ya nani??? Wote mnataka kuwatumia wasanii wale wale na sehemu zile zile.
Nadhani mngewanufaisha wasanii wetu na kutoa fursa kwa watu wengi kama mngepeana nafasi mmoja
aanze na mwingine amalizie....kuliko huu utoto mnaofanya. Mfano Fiesta ilianzia Mwanza...Kili Tour ikawa
Mbeya the same weekend!!! WHY???
Kila brand ingetafuta muda sahihi na sio kukomoana, mnawanyima fursa wasanii na wapenzi wa burudani.
Mandla.
Acha chokochoko na majungu yako.INAHUSU!
ReplyDeleteKilamtu atakula kwa urefu wakamba yake hapo
ReplyDeleteasante mdau
DeleteMbona maduka ya nguo kariakoo yamejipanga tele na yote yanafunguliwa asubuhi mpaka jioni, kwa nini wasisubiriane mwingine afunge na mwingine ndo'afungue. Wacha uchonganishi, fanya yako....... hovyoooooooo!!
ReplyDeleteHahahaaaa mdau hapo juu nimechekaje?! Uwiiiii mbavu zangu jamani kwel Admn aache uchonganishi
ReplyDeletemawazo yako admin yanaonyesha jins gani ulivo na low thinking capacity nxt time post mada zenye mtazamo chanya
ReplyDelete