Hatimaye John Shibuda Ajifukuzisha Chadema Mwenye, Atoa Shutuma Kali Dhidi ya Chadema

WAKATI Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kikijipanga wakuchukulia hatua wabunge wake waliosaliti msimamo wa Kamati Kuu na kuhudhuria vikao vya Bunge la Katiba, Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda ametangaza kutogombea ubunge tena kupita chama hicho.

Shibuda, Said Arfi (Mpanda Mjini) na Leticia Nyerere (Viti Maalum) wamewasili mjini Dodoma na kujisajili kwa lengo la kushiriki vikao hivyo, licha ya kuzuiliwa na chama chao ambacho kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kimesusia Bunge hilo.

Shibuda alitangaza uamuzi huo kwa nyakati tofauti jana, wakati akizungumza na wazee wa mji wa Maswa na Malampaka wilayani humo, walipotaka kujua hatima yake ya kisiasa ndani ya CHADEMA.

Alidai kauli za vitisho na kejeli dhidi yake zinazofanywa na baadhi ya viongozi wa CHADEMA, ndizo zimemfanya achukue hatua hiyo.

“Mimi niliingia CHADEMA kwa hiari yangu baada ya kuona dhuluma zilizokuwa ndani ya CCM, chama ambacho kimenilea kisiasa, nikaona heri niende CHADEMA ambako nilidhani kuna demokrasia na ukombozi wa kweli.

“Lakini nilichokikuta humo ni tofauti, kwani kila siku wazee wangu mnasikia napata misukosuko isiyo na maana,” alisema.

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huyu naye tapeli tu, rudi kwa mama yako ccm unalipwa kuharibu vyama pinzani kubwa Zima hovyooo

    ReplyDelete
  2. yani tokea uhamie chadema mimi sikuwaelewa viongozi wa chadema kabisa, wewe ni mlafi tu hauna maana yeyote kwenye hili taifa, wewe ulikimbilia chadema kwa ulafi wako tu, ningekuwa mimi kiongozi wa chadema nisingekukubalia hata kidogo kujiuunga na chadema, sababu wewe unajalitumbo lako tu na walasiyo masuala ya wananchi, rudi kwenu ccm!

    ReplyDelete
    Replies
    1. CHAGA DEVELOPMENT MONITORING ASSOCIATION (CHADEMA).

      Delete
    2. CCM,Chama Cha Mafisadi.je na wewe ni mmoja wapo?!

      Delete
  3. Njaa inamsumbua shibuda,kuipa kisogo lak3 kwa siku unahitaji kukomaa na uwe mtu mzima kisiasa na kifikra.

    ReplyDelete
  4. pole shibuda nenda ACT

    ReplyDelete
  5. Awadanganye tu wapiga kura wake maana ndio mizigo ya ujinga aliyotuachia Nyerere tupambane nayo. Shibuda sio bwege kihivyo bali wapiga kura wake.

    ReplyDelete
  6. Sema basi unarudi CCM au ???????????????????????????????????

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad