John Mnyika:Katiba Mpya Haipatikani Mwaka 2014 Kama Ilivyokuwa Ikitarajiwa na Wengi

Mbunge wa jimbo la Ubungo Mh.John Mnyika amefunguka na kuweka wazi kuwa Katiba Mpya haiwezi kupatikana mwaka 2014 kama ambavyo ilikuwa ikitarajiwa,Mnyika amefunguka hayo leo akiwa katika kipengele cha Kikaangoni Live

kinachofanyika kila siku ya Jumatano kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV.
Mnyika amesema kuwa hata kama ikitokea UKAWA wakirudi bungeni suala la kupatikana kwa katiba mpya litakuwa ni kitendawili kutokana na namna mchakato ambao ni lazima kupitia ili kupata hiyo Katiba mpya.
"Ni kweli 2014 haiwezekani kupatikana kwa Katiba mpya,kwani siku 60 alizotoa Rais Kikwete hata kama UKAWA ikirudi bungeni hazitoshi kumaliza ibara zote 271 na sura 17 kama mpaka sasa zinabishaniwa sura mbili tu. Hata kama ikipatikana, itahitaji kupigiwa kura ya maoni, kwa taarifa nilizonazo toka ndani ya tume ni kwamba inawezekana ikiwa Mwezi Machi 2015.Hata ikiwa muda huo, Shirikisho la Serikali Tatu likiwa ndio muundo Katiba za Tanganyika na Zanzibar zitapaswa kuandikwa upya. Hivyo, kutahitajika Bunge Maalum na kura ya maoni ya Tanganyika, na hata tume ya maoni hata kama itatumia maoni kwa sehemu yaliyokusanywa na Warioba na rasimu ambayo wanadai wanayotayari. Hata kama ingekuwa katiba mpya ya Serikali mbili, bado Sheria muhimu zinazokinzana na katiba mpya zitapaswa kuandikwa upya. Hivyo, kwa vyovyote vile, katiba mpya haiwezi kutumika kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Mbali na hilo Mnyika ameweka wazi msimamo wa Umoja wa Katiba ya Wanchi (UKAWA) kuwa hawawezi kurudi katika Bunge Maalumu la Katiba kama hakutakuwa na maridhiano yenye kuheshimu na kutambua maoni ya wananchi na kutambua misingi ya rasimu ya Katiba uliyotokana na maoni ya wananchi

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Yeeeeeeeessss Mnyika ni kichwa bwana! Hebu imagine akifikia umri wa sitta atakuwaje?

    ReplyDelete
  2. We subiri uone tutawanyoosha mpk washike adabu .ukawa mbele adanganywi mtu hapa.

    ReplyDelete
  3. hongeraa kijana bunge
    lako ni mitandao jamii tu chezea mshahara kutoka Mbowe ?

    ReplyDelete
  4. mnyika kibaraka wa mbowe

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unaakili wewe ni zaidi ya kibaraka akisema ndio yeye hawezi sema hapana ni ndio tuu

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad