Kondom za MALAYA wa Morogoro Zawaathiri Watoto Wanaoziokota na Kuzifanya Mapulizo

Biashara ya ngono iliyokithiri katika mji wa Morogoro imegeuka kuwa kero kwa wakaazi wa eneo hilo na familia zao hali inayowaweka hatarini zaidi watoto wadogo wasio na hatia wanaokutana na kondom zilizotumika huku mkuu wa Mkoa huo, Mheshimiwa Joel Bendera akinawa mikono kuhusu suala hilo.

Wakati hayo yakiendelea Morogoro, serikali kuu imekuwa ikitafuta dawa kali ya kuweza kudhibiti biashara hiyo hapa nchini.

Edson Mkisi Jr wa Times Fm, hivi karibuni alitembelea mkoa huo na kushuhudia kushamili kwa biashara ya ngono sehemu mbalimbali za mkoa wa Morogoro hususani katika maeneo ya Kaumba na Itigi mkoani humo.

Taarifa zilizopatikana awali toka kwa baadhi ya wakazi wa maeneo ya mji wa Morogoro zilidai kuwa biashara ya ngono imekuwa kero mkoani humo kutokana na utupwaji hovyo wa kondom zilizotumika katika mitaa hiyo.

Kondom hizo zilizotumika zinahatarisha afya ya watoto wanaozitumia kama mapulizo.

“Kiukweli hii biashara mbali ya kutuaibisha sisi akina mama lakini pia inatukera sana kutokana na utupwaji hovyo wa kondom unaofanywa na hao akina dada….na baada ya kondom hizo kutupwa watoto wetu wanaziokota na kuanza kupuliza kama maputo kwakweli inatukera sio siri,” anasema mama Sakina mfanyabiashara maarufu wa samaki Msamvu Morogoro.

Baadae mwendesha bodabodo eneo hilo alimuonysha mwandishi wetu Hotel moja maaufu na kudai kwamba Hotel hiyo imekodiwa na MALAYA  hao kwa ajili ya kufanyabiashara hiyo na serikali ya mkoa wanatambua ‘ishu’ hiyo!

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad