Mainda: Nimefanya Sana Anasa Hapa Duniani ila Kwa Sasa Basi

STAA wa filamu Bongo aliyeamua kumpokea Yesu, Ruth Suka ‘Mainda’ amesema kipindi cha nyuma alipotangaza kuokoka alikuwa ni kama anamtania Mungu ila sasa ameokoka kikwelikweli.

Akipiga stori na Udaku Special alisema awali alipofunguka kuwa ameokoka, hakuwa siriasi kwani alikuwa akiendeleza anasa za hapa na pale lakini sasa yeye na Yesu, Yesu na yeye.

“Mwanzo nilikuwa kama namtania Mungu, nilisema nimeokoka lakini kimyakimya nilikuwa naendeleza anasa, nimefanya sana anasa lakini sasa basi.

“Huwezi kunikuta sehemu yoyote ya starehe hata siku moja, wala kuniona nimevaa mavazi ya ajabu na hata filamu nikicheza siwezi kuonekana kama mwanzo, nachagua vipande vya kucheza ambavyo haviwezi kunivua wokovu wangu,” alisema Mainda.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. sura tu inaonyesha ulikuwa balaa!! bora umemrudia Mungu, na usimtanie sasa hivi.

    ReplyDelete
  2. Ukapimwe na Ukimwi ili kuhakikisha uko salama na wokovu wako.

    ReplyDelete
  3. Hongera bi dada,Na kwa damu ya yesu umetekasika.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad