MTOTO wa kike mwenye umri wa siku moja amenusurika kufa baada ya kuokolewa na wasamaria kutoka katika shimo alimotupwa na mama yake mzazi.
Imeelezwa kuwa mwanamke huyo alifanya hivyo ili kulinda ndoa yake changa, kwa kuwa mumewe hakuwa mhusika wa ujauzito huo.
Taarifa za tukio hilo zimethibitishwa na Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Rwabigaga, Fron Nestory. Alisema tukio hilo ni la usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita katika kijiji cha Rwabigaga kata ya Kamuli wilayani Kyerwa.
Alidai siku hiyo ya tukio, mwanamke huyo, Jane Leonard alijifungua salama mtoto wa kike, lakini baadaye akamwambia mama mkwe wake, kuwa mtoto amepotea katika mazingira ya kutatanisha.
Nestory alisema kutokana na taarifa hizo, juhudi za kumsaka mtoto zilianza na ilipofika asubuhi wamlikuta mtoto huyo kwenye shimo, akiwa amefunikwa kwa maganda ya maharage na tayari siafu na wadudu wengine, walikuwa wameanza kumshambulia.
Alisema jitihada za kumuokoa mtoto huyo zilifanyika, ambapo baada ya kumuosha alipelekwa katika Kituo cha Afya Kamuli na kupatiwa huduma. Kwa sasa anaendelea vizuri na tayari amekabidhiwa kwa mama yake mzazi.
Kwa upande wake, mama mzazi wa mtoto huyo alisema alifanya hivyo, kutokana na hofu ya kuvunjika kwa ndoa yake changa, kwani imepita miezi miwili tu tangu aolewe.
Ingawa hakutaka kuingia kwa undani, imeelezwa hofu yake imetokana na ukweli kwamba, ameingia katika ndoa mpya akiwa mjamzito, ilhali mumewe wa sasa si mhusika.
Hata hivyo, Nestory aliwataka wananchi kuwa na hofu ya Mungu na kuacha vitendo vya unyanyasaji na ukatili kwa watoto, kwani mtoto ni tegemeo la taifa kwa ujamla.
Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Henry Mwaibambe alisema tukio hilo hajalipata;na alisema ameagiza polisi wilayani Kyerwa, kufuatilia zaidi na kumpa taarifa juu hilo.
Chanzo: Habari Leo
Hata kama ulitaka kulinda ndoa , hukupaswa kufanya hvyo,tumuogope mungu jamani.
ReplyDeletejinga hilo janajike pyeeeeeee
ReplyDeleteKwani wakati unaingia ndoa mpya hukujua wewe ni mjamzito huna akili huna huruma huna hofu ya mungu ndani yako ningekuita mnyama ila hata wanyama wanamapenzi sana kwa watoto wao
ReplyDeletesasa ndoa imekua ndoana mume hatapenda mwanamke katili kama wewe
ReplyDeleteMwanamke katili wewe,aliyekuambia ndoa inalindwa kwa dhambi nani?
ReplyDeleteUlaaniwe kuliko wanawake wote,pweza wewe!
Daaaaah!!! Hivi wewe manyoko wakati unatanua hukujua maskini mtoto hana hatia yoyte huyo. Halafu huyo dada ni muuaji alidhamiria kuua hujui huyo mtoto atakuja kuwa nani kesho oooho, Mama yake Christian Ronaldo naye hivyohivyo kakazana kutoa mimba iligoma kakiri, ila ni Mungu kamuonyesha huyo mtoto uliyetaka kumuua ndo tegemezi lako sahvi, tena umuombe huyo mtoto msamaha sahvi akiwa hivyohivyo malaika wa Mungu... Tubu hatokujibu ila msamaha wako utawekewa tiki hata kwa Mungu, unataka kuua damn yako kisa ndoa???? Oooh my God. Mungu akusamehe tu
ReplyDeleteNimefurahi sana kuckia kapona huyu mtoto.. mungu slampe afya njema na maisha marefu, ampe maisha ya amani na amuepushe na makatili wengine kama mama yake... huyo mama mungu amuhadhibu hapa hapa duniani, huyo mume asimpende tena na apige michepuko kama hana akili nzuri a.k.a wazimu mpaka anogewe amfuzilie mbali mkewe wenyewe.. aaaamen!!
ReplyDeleteyaan serikali yetu ni ya kipumbavu sanaaa,sasa unaona mtoto anataka uliwa na mama yake mzazi halafu unamrudishia mtoto tenaaa? why? hivi viongozi wetu wamesoma shule kweliii au ndo vyeti vya kugushiii? nini maana ya ustawi wa jamii? huyo mama anatakiwa ashtakiwe na mtoto apelekwe ustawi wa jamiii,yaaani hawa kazi hawaijui kweli kweli kazi kuchukua mishahara ya bureeeee!!!!! mtu unaona kabisaa nia yake ni kumuuua badala ya kuokoa maisha yake unamrudisha kule kule kwa adui,lol...viongoz mburulaz kweli kwelii...waangalie wenzao marekani wanavyofanya kazi watu wa ustawi wa jamii,kesi kama hii mama anaenda jela kwa kosa la kukusudia kuuwa na mtoto analelewa na serikali ktk ustawi wa jamiii na ndio kazi yaoo!!! embu rudini shule nyie viongoz mburulaz mnatutia aibuuuu...shame on you guys.
ReplyDeleteYes anony hapo juu! Nchi yetu vilaza wengi kila sehemu ni madudu unashangaa hivi Afrika tumelogwa na nani? Akili ni nywele, hizi kipilipili si nywele jamani ni funza kichwani!
ReplyDeleteMwanamke kataka kuua mtoto wake halafu eti anarudishiwa amlee! Siku nyingine atamkaba na mto amuue!
Wewe acha ujinga kwani wakati anakuoa mimba siilikua ya miezi 7 na alikuona nayo na akarizika kukuoa hivyohivyo iweje mtoto azaliwe umpute je mama yako angekutupa ungekua wapi sasa acheni roho za kishetani jaman
DeleteWANAWAKE BWANA....!KAMA SI UKATILI ULOPINDUKIA NI NINI HIKI?
ReplyDelete