Mjuwe Bakhresa Katika Picha, Najua Wengi Hamjawahi Kumuona Mzee Huyu Asiye na Makuu

KATI ya miaka ya 1960 hadi 1980, mtu kuwa tajiri alionekana ni hatari kwa taifa, tena mali zake alizimiliki kwa kificho, vinginevyo angeitwa mhujumu uchumi. Lakini kwa sasa mambo yamebadilika, taratibu sera za kibepari zinatawala, ujamaa unapewa kisogo.
Mtu kama ni mbunifu, ana nidhamu ya kutofuja pesa na anafanya kazi sana kwa nini asiwe tajiri? Utandawazi unasaidia ndiyo maana leo tunaweza kuwatambua mabilionea wakubwa ambao wanastahili pongezi kwa hatua walizopiga. Tusisahau kuwa wanaibeba nchi kwa ulipaji kodi.


1. SAID BAKHRESA
Jina lake kamili ni Said Salim Awadh Bakhresa. Jarida la Forbes mwaka jana, lilimuorodhesha miongoni mwa matajiri 40 Afrika kwamba anamiliki utajiri wenye thamani ya dola milioni 620 (karibu shilingi trilioni moja). Hata hivyo, inadaiwa kuwa tabia ya usiri wa Bakhresa inafanya mali zake zisijulikane sana, ila ni tajiri zaidi ya kiwango hicho.
Ndiye mmiliki wa makampuni ya Bakhresa yanayotoa bidhaa zenye chapa ya Azam ambazo zinauzwa nchi mbalimbali Afrika. Ana viwanda vya nafaka na vinywaji, vyombo vya usafiri wa majini, uuzaji wa chakula, bidhaa za plastiki na kadhalika. Ndiye mmiliki wa Klabu ya Azam FC.

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Apana chezeya yupo juuuuu mungu amzidishie kweli tulikua hatumjui kwa sababu hapendi kujionyesha unaonyesha vtendo tu daaah!!!! Penda sana baba huyu

    ReplyDelete
  2. MASHALLAH...ALLAH akulinde

    ReplyDelete
  3. Wangetokea watu kama Bakresa watano tu Tanzania ingenda mbali, kwa kuwa si mtu wa dhuluma, au wizi, anatafuta mali yake kihalali si kwa ufisadi,

    ReplyDelete
  4. Anatoa misaada sana huyu baba, acha jamani,kimyakimya lakini wengine wakitoa msaada kila siku mpaka wawaite
    GPL,mwananchi ,ITV nk waitwe,lol

    ReplyDelete
  5. Mungu azidi kumlinda huyu baba, hana mashauzi, hapendi majisifu. Pamoja na mali alizonazo lakini huwezi kusikia kajinadi au kanadiwa eti 'fulani aonyesha jeuri ya pesa', ingekuwa ndio hao wanaojiona wana 'jeuri ya pesa' kisa kanunua gari, nafikiri magazeti yote yangejaa habari zake tu!

    ReplyDelete
  6. Allah ampe zaidi inshallah na amuondolee hasada amewapa vijana wengi ajira hilo ndio kubwa

    ReplyDelete
  7. Ajenge shule na hospitali na siyo kujenga misikiti huku waumini walioizunguka ni masikini wa kutupwa!!

    ReplyDelete
  8. Diamond utulie unaona mabilinaire haooo wako kimya siyo ww matangazo kila kukicha

    ReplyDelete
  9. Amenisomesha huyu mzee o level to high school. Yupo juu aisee..respect.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad