Kamishna Suleiman Kova akionesha namna mguu huo wa mtu mwenye ulemavu unavyotumika kutunzia dawa za kulevya.
KIJANA mmoja ambaye ni mlemavu wa mguu, Said Tindwa (36), mkazi wa Vijibweni Kigamboni jijini Dar, anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kutumia mguu wake wa bandia kwa ajili ya kutunzia na kuuza dawa za kulevya.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum, Suleiman Kova alisema mlemavu huyo alitiwa nguvuni Agosti 1 mwaka huu kufuatia mtego uliowekwa na jeshi hilo.
Alisema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa akitumia mbinu ya kuziuza dawa hizo kwa kuzificha kwenye mguu wake wa bandia.
Aidha Kova alisema kuwa dawa alizokuwa akiziuza mlemavu huyo ni zile za viwandani kama vile cocaine, heroin na wakati mwingine bangi.
“Katika mtego maalum uliowekwa na askari wa upelelezi ndipo mlemavu huyo alikamatwa akiuza dawa hizo kwa wateja wake baada ya kuzitoa alikozificha ambapo ni ndani ya mguu huo wa bandia” alisema Kova.
Funga miaka 30
ReplyDeletenjaa kali
ReplyDeleteJamaa hazitengenezi nyumbani kwake. alizipata kwa mtu B,B alizipata kwa C ,C alizipata kwa D vivyo hivyo hadi Z,chain yake ifuatiliwe.
ReplyDeleteHuu ndio ushauri muafaka, tayari mlemavu mmemkamata na madawa, kosa lake ni kukutwa na madawa ya kulevya ashitakiwe; wakati huo huo apewe kibano awataje matajiri wakenao washitakiwe kwa kuingiza mada hayo nchini. Kova na Polisi wako kumshitaki tu huyo mlemavu, matajiri wake watatafuta muuzaji mwingine adhali za madawa hayo itaendelea kuwatasa watanzania kundi la nguvu kazi yetu.
Deletedawa nikutafuta mzizi sio matawi kwani matawi yatachipua tu huyo hana kosa mwenye kosa nialiyeingiza hayo madawa nchini na yameingilia wapi yakamfikia hapo, kazi kwenu polisi tunategemea jibu litapatikana kupitia mlemavu
ReplyDeletePolisi kweli Mambwiga mnajisifu kukamata mlemavu wakati Mawaziri na Vigogo wanaoleta MBWIMBWI mnawajua mmebaki kuwatumbulia macho tu shenzi zenu mkitaka kukomesha hiyo biashara wakameteni wanaoingiza arafu muone nani atakayesambaza.......
ReplyDeleteKOVA WHAT ABOUT WWW.AKIBASACCOS.WAPKA.MOB?WATU WANALIWA UPO TU KAMANDA WANGU?
ReplyDelete