Mnaoishi Nje ya nchi Acheni Kupoteza Muda Kwenye Blogs na Kulaumu Wengine Kuhusu Uraia Pacha..Leteni Hoja

RAIS Jakaya Kikwete, amewataka Watanzania waishio nje ya nchi na wanaotaka kuona Tanzania inakubali kuanzisha mfumo wa uraia pacha, kutumia muda wao kujenga hoja za jambo hilo badala ya kupoteza muda kwenye mijadala ya ‘blogu’ na kulaumu watu wengine.

Pia, aliwataka watanzania hao kusema ili wasikike, kwa sababu kimsingi hoja ya uraia pacha haina nguvu miongoni mwa Watanzania wanaoishi Tanzania, bali inatokana zaidi na msukumo wa Watanzania wanaoishi nje, ambao kwa bahati mbaya hawafanyi jitihada za kutosha kutetea hoja yao.

Aliwaambia watanzania hao, kuacha kupoteza muda kujadili mambo yasiyokuwa na maana, badala yake kuelekeza nguvu zao katika kujenga hoja yenye nguvu zaidi ya uraia pacha, jambo ambalo ni moja ya mambo yatakayojadiliwa katika mchakato wa Katiba mpya.

“Ushauri wangu ni kwamba tumieni muda wetu kusaidia kusukuma hoja yenu hii muhimu ambayo kama mnavyojua imeingizwa katika rasimu kwa mapendekezo ya CCM kwa sababu suala hilo halikuwemo katika rasimu ya kwanza,” alisema.

Rais Kikwete, ameyasema hayo Agosti 2 mwaka huu, wakati alipokutana na Watanzania wanaoishi Marekani,  hasa katika maeneo ya Jiji la Washington D.C na majimbo ya Virginia, Maryland, New York na hata California katika mkutano uliyofanyika hoteli ya Marriot Washington mjini Washington D.C.

Rais yuko katika ziara ya siku tisa nchini Marekani, ambako miongoni mwa mambo mengine atahudhuria mkutano wa kwanza wa Marekani na Afrika ambao shughuli zake zimeanza jana.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ni watanzania wangapi wenye makaratasi ya kutaka huo uraia pacha???? Wengi wao hayo makaratasi yenyewe ya huko hawana. Halafu leo hii wazungumzie uraia pacha si mpaka. Na hata hao wachache wenye makaratasi hawana hata huo uwezo wa kuzungumzia hiyo hoja na wala hawajui ni kitu gani wanataka. Kwanza wengi wao ukiwauliza maana ya uraia pacha hawajui na pia ukiwauliza yale manufaaa ya uraia pacha hawajui na wala hawataki kujua. As a matter of fact Watanzania wengi majuu wamekata tamaaa sana na Tanzania kiasi cha kwamba sio tu hawataki kurudi kwenye Nchi yao bali wengi wao hawapendi hata kujitambulisha kuwa wao ni watanzania. Wanajitambulisha kuwa wao ni kutoka nchi nyingine. Yaani kimsingi hawajivunii ule utanzania. Wanaogopa kuchekwa.....cheza na watanzania majuu wewe.

    ReplyDelete
  2. Na pia ni lazima ikumbukwe ya kuwa watanzania walioko majuu wengi wao hapendani na pia kuna viji makundi makundi na pia hawatakiani mema katika suala lolote linalohusu Maendeleo. Kwa hiyo matokeo yake ni aina ya wale watu wanao kaa hapo na kupika majungu na kusengenyana. Kwa sababu hizo ni vigumu sana kwao kukutana na kuzungumzia mambo yoyote ya maana kuhusu maisha yao na mstakabhali wao wa baadae. Hawa ni watu waliokata tamaa na maisha ni wale watu wa kuwahurumia sana. Watanzania walioko majuuu huwezi walinganisha na Raia wa Nchi nyingine kutoka Africa. Hao wa Mataifa mengine ni watu wenye ushirikiano sana. Kwa kweli ni kitu cha aibu sana kwa Watanzania waishio huko ughaibuni.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad