Mrema Awatambia UKAWA, Amuonya Mbatia, Asema Atishwi Kabisa na Ukawa

Moshi. Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema (TLP) amedai kitendo cha yeye kubaki kwenye Bunge Maalumu la Katiba kumetumiwa vibaya na wahasimu wake wa kisiasa jimboni kwake.

“Ukawa na ubunge wa Vunjo vimegeuka propaganda chafu dhidi yangu. Wamediriki kuwaambia wananchi wangu kuwa nimeahidi kuwaachia jimbo langu,” alisema.

Mrema ambaye pia ni mwenyekiti wa taifa wa TLP, alitoa kauli hiyo jana jimboni kwake katika mkutano na waandishi wa habari aliouitisha kuelezea kwa nini hakuwaunga mkono Ukawa.

Mrema alisema malengo ya Ukawa siyo katiba bali Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na ndiyo maana tangu waliposusia Bunge agenda yao imebadilika na kuwa muungano wa kuelekea uchaguzi 2015.

“Mimi nimeamua kubaki bungeni kwa ajili ya masilahi mapana ya wananchi wa jimbo langu la Vunjo na Watanzania kwa jumla. Sitishwi na Ukawa na nitatetea kiti changu 2015,” alisisitiza.

Mrema alitumia mkutano huo kumshambulia mbunge wa kuteuliwa na Rais, ambaye ni James Mbatia kutokana na uamuzi wake wa kutangaza nia ya kuwania ubunge wa Jimbo hilo mwakani. Kwa mujibu wa Mrema, ndiye Mtanzania pekee mwenye sifa na aliweza kugombea ubunge katika majimbo matatu tofauti na kushinda.

“Mimi ni Mtanzania pekee ambaye nimewahi kuwa mbunge wa majimbo matatu tofauti ya Moshi Vijijini, Temeke na Vunjo. Sifa hizo hazipo kwa wengine,” alisema.

Chanzo: Mwananchi

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wewe mzee ushazeeka, hauna jipya tena waachie vijana

    ReplyDelete
  2. Na kweli maana huna unachoongea zaidi ni maslahi yako tuu!kubaki bungeni sio ndio kisingizio cha kutafuta katiba wananchi ila ni huo uroho wa shilingi laki tatu tuu!

    ReplyDelete
  3. Haka kababu kaokoke kajizeekee taratibu tu! Kaone kalivochoka usoni! Hivi kanaugua maradhi gani? Nilisikia mwembechai walikasomeaga albadili! Kama si Kakobe kalikuwa kashazikwa siku mingi!

    ReplyDelete
  4. Ni njaaa hawa wazeee wa pale Bongo wana njaa jamani duh. Huyu babu aliishashika vyeo kibao pale Serikalini haridhiki tu. Kwa kweli wazee wa Kibongo wana tamaaa mbaya sana

    ReplyDelete
  5. Wabongo kwa kuonyesha wanavyopenda masifa na vya mteremko ona jinsi walivyochakachua uchaguzi wa viongozi tena wa Jumuiya yao wenyewe pale ughaibuni DMV yaaani ni aibuuuuu duh

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad