Mtoto wa Miaka Nane Apigwa Risasi ya Kichwa na Majambazi Arusha Akiwa na Wazazi Wake

Kumradhi kwa picha ya Malaika huyu " Hii imetokea arusha jana saa tano usiku jamaa yuko na mke na watoto wao wawili wa kike wanatoka dinner wanarudi nyumbani mara jamaa wa toyo wawili wakasimamisha gari yao na kuwaamuru watoe vyote walivyonavyo kaka hakusimama akawasha gari na kukimbia wakaanza kukimbizana wanaelekea mbauda ndipo watu waliokua kwenye Toyo wakapiga risasi kwa nyuma maskin ikampata mtoto wake wa miaka nane ambae alikuwa amelala kwenye siti ya nyuma straight kwenye ubongo na hawakua na habari ile wamefika mahala penye usalama wacheki ni nn wanaona mtoto damu zinamtoka machon kumkimbiza hospitali mount meru wameshindwa kumtoa risas mtoto akafarik jana hyohyo majira ya saa saba .. Huzun sana baba mtoto anafanya kaz UN liberia alirud tu likizo na hyo mambo ya ebola juzi sasa ndio alikua anarud kwenye kazi yake kuhusu kudeal na ugonjwa wa ebola liberia na jana ilikuwa last night na familia kaipeleka dinner haya mtoto wake ndo huyo kauawa wazazi wake wamechanganyikiwa... Kumradhi kwa picha ya mtoto"

Jamani wezi huyu malaika mkamuua kwa tamaa zenu za kutaka mali bila kuzitolea jasho!!!! ee Mungu Okoa Taifa hili... vijana wawezeshwe Ajira za halali waondokane na dhambi hii na hali yao ya kujitoa muhanga kwa kazi hii ngumu ya wizi na inaleta maumivu kwa watu wasio na Hatia kama hii familia...wajaalie Wenye dhamana na Taifa hili waache ulafi na ufisadi ili rasilimali za nchi hii ziwanufaishe
By Joyce Kiria

Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Inauma sana mungu ailaze roho yake mahali pema peponi poleni sana na mungu aiyone hiyo familia.

    ReplyDelete
  2. Pumzika kwa amani Mwanangu Mungu atawachoma moto wote waliotenda ukatili huo

    ReplyDelete
  3. sheria ya ukikutana na mtu mwenye silaha fanya chochote atakacho. simu na hela haviwezi kufikia thaman ya uhai.

    ReplyDelete
  4. Hawa majambazi sasa wanatisha nchi, dawa yao ni kuwauwa tu mtandao wao sio mkubwa wengi wao wanaishi mbagala, kigamboni, buguruni, manzese, mburahati, kunduchi, kinondoni, majumba sita, tandika, mtoni, kinyerezi, yombo, kijitonyama, na sehemu nyinginezo polisi na wananchi tufanyeni msako huko

    ReplyDelete
    Replies
    1. Halafu kwani hawajulikani hao majambazi minashindwa kuwaelewa wanaokumbatia majambazi.maamae zao.ueniwote maana mnawajua namsipowauwa basi watauwa watu mpakanyie mnaowakumbatia.wanachosha nakutia hasira tena arusha wamezidi wauweni tuu sio mnakamata mnawaachia.biblia iliandika atakaeua kwa upanga nae auliwe.mnashoiashoia nini km wahindi taahira kazikukumbatia dhambi tu na mungu atawalaani wote mnaowajua wahalifu nabado mnawakumbatia.mtakufa kwa vifafa tumewachoka

      Delete
  5. Arusha kuna ninii jamanii?mbona hali inatisha sanaa?!maana hili ni tukio la tatu sasa la namna hii...juzi rafiki zangu 2 walikutana na watu kama hao wa pikipiki...wakapiga risasi ikampata dada mtu...Mungu mwema yuko sawa sasa...baada ya hapo tukaskia tena mke wa tajiri mmoja huko huko Arusha alipigwa risasi...kwa kweli huu mtandao lazima ufatiliwe kwa makini na serikali.

    ReplyDelete
  6. juzi tu wamempiga mtu risasi ya jicho,Sinza Vatcan masikini wamemtoboa jicho kijana wa watu mdogo kabisa hivyo hawezi kuona tena kwa tamaa zao za pesa..

    ReplyDelete
  7. Tatizo ajira watu wamesoma alafu ajira hakna bongo ndo kitu ambacho knapelekea watu kujihusisha na vitu viovu cz hata kaz zikitangazwa zina wenyewe sasa maisha gan? R.I.P MTOTO

    ReplyDelete
  8. Mie sidhani kama mtu kweli toka awali alikuwa hana tabia ya ujambazi eti kwa sababu kakosa ajira ndo awe jambazi na kuwa mkatiri namna hiyo mpaka kuuwa jamani....we sema pengine huyo mtu alokosa ajira anaweza kuwa omba omba au kama ni tabia yake mbaya akawa hata mdokozi,lakini si ujambazi wa kuuwa au kuvamia watu usiku wa manane...Mwenyezi Mungu Atuhifadhi na hao majambazi na mafisadi na walarushwa...Mola Awatokomeze kwani wametunyonya muda mrefu mno..

    ReplyDelete
  9. Mkwere kashindwa nchi! Vijana wamejazana mtaani, hamna ajira wala shughuli yoyote ya kuwapa maisha!
    Maisha bora kwa kila mtz imegeuka maisha shubiri! Vijana wa kiume wanabwia unga, wengine majambazi na wa kike ni umalaya kwenda mbele!
    Hawa wanaofanya ujambazi wanaona kikundi cha watu wachache walioko madarakani na familia zao kinavoishi kama peponi na kufuru za anasa kwa kufaidi rasilimali za nchi wakati watoto wa masikini wamejaa vijiweni wakikosa uhakika wa mlo mmoja kwa siku!

    ReplyDelete
  10. jamani mimi niko arusha huyu mtoto ameniliza toka siku ya tukio roho inaniuma sina namna ya kumsahau naiomba serikali itusaidie hata arusha tutangazwe mkoa maalum wa kijeshi.....its about time serikali ifanye kitu coz hata watalii wanapungua....nani apendi usalama....plz for the sake of this economy and taifa govnt must react now.....

    ReplyDelete
  11. what is wrong whis this taifa of ours ....tumefeli kwenye elimu ,huduma za jamii na vingine vingi but hata usalama....watu wanauawa mchana wakionekana ....can't we do anything ....tunatengeneza taifa lipi......na hata wakikamatwa after months mnapishana mtaani wako huru money talks.....jamani wanaharakati wekeni hata makongamano pengine hata jeshi letu ni feki...tusemeje sasa...plz kiongozi mkubwa its about time tuwe serious na security and all country affairs. R.I.P mtoto lovin u ,dad n mummmy does as well mit you some day but you go n tell god evrthn

    ReplyDelete
    Replies
    1. huwezi kuongea kiswahili moja kwa moja? huoni ndio utaeleweka vizuri na utakuwa muungwana.

      Delete
  12. Kama kizungu kimekupiga chenga pole kachukue kamusi.watu tunahasira kilamtu ataongea kwa lugha atakayo mradi ujumbe umefika.nyie wakuu hivi hili tatizo la mauaji mnaliona movie wakati watuwanauwawa hovyo.halafu arusha sijui watuwanaroho gani au tunasema watu kumbe wengi ni mashetani maana mashetani kaziyao kunywa tu damu zawatu.kilasiku arusha kuuana mashetani wakubwa wote mnaoua maanina zenu.nawakubwa wa nchi endeleeni kuenjoy huku watu wanakufa akifa mwenzenu mmoja mtanyanyuka mfanye kazi namtawaua nawao.kamanikudhibiti mnauwezo ilamnafumbia macho.sasa akifa wakwenu mtainuka

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad