Mtuhumiwa Kinara wa Mauaji ya Wanawake jijiini Arusha Anaswa na jeshi la polisi

Mtu mmoja ambaye inadaiwa kinara wa kuua na kujeruhi wanawake maarufu, wafanyabiashara na wenye vyeo katika ofisi mbalimbali jijini Arusha, Adamu Mussa (30) mkazi wa Majengo Juu jijini Arusha ametiwa mbaroni.

Mtuhumiwa huyo ametiwa mbaroni juzi usiku na polisi na alipopekuliwa nyumbani kwake alikutwa na bastola mbili  na risasi saba na amekiri kuhusika katika mauaji na kujeruhi wanawake jijini Arusha.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha Lebaratus Sabas, alizitaja bastola mbili zilizokutwa nyumbani kwa mtuhumiwa moja ni aina ya Browning  iliyotengenezwa  Jamhuri ya Czech  yenye namba A 895936 na ilikutwa na risasi saba.

Alisema bastola ya pili aliyokutwa nyumbani kwake ni aina ya Lorsin yenye namba za usajili 379126 iliyotengezwa nchini Marekani ikiwa na risasi tatu.

Sabas alisema uchunguzi wa Polisi ulibaini kuwa bastola  aina ya Browning  ilikuwa mali ya Seleman Bakari Msuya (33) mkazi wa Sombetini jijini Arusha ambaye silaha yake hiyo iliibwa baada ya  gari lake kuvunjwa kioo siku za nyuma.

Wakati huohuo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo amewasihi wanawake kuwa na moyo wa uvumilivu na kuacha vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi zake ili kuwabaini wale wote wanaohusika na mtandao wa mauaji ya wanawake pamoja na mtoto.
Bastola iliyotumika katika shambulizi hilo. 

Mulongo aliyasema hayo jana jijini Arusha wakati alipokuwa akizungumza na wanahabari wa vyombo mbalimbali ofisini kwake juu ya ujumbe uliosambazwa kwenye simu mbalimbali kupitia mtandao wa Whatsapp kuhusu kujitokeza kwa wanawake/wasichana  leo  kwa Mkuu huyo wa Mkoa  ili kujua hatma yao.
Akizungumzia suala hilo  Mulongo alitoa rai kwa akinamama wote pamoja na wasichana kuwa watulivu na kusaidia vyombo vya ulinzi na usalama kuwafichua wale wote wanaofanya mambo hayo.

Awali juzi watu  saba walikamatwa jijini Arusha  kwa tuhuma za kuhusika kwenye mauaji ya unyang’anyi wa kutumia silaha kwa wanawake  pamoja na kusababisha  kifo cha mtoto, Christen  Nickos mwenye umri wa miaka mitatu na nusu  mkazi wa Olasiti jijini  hapa.

Kamanda wa Polisi Liberatus Sabas alisema watu wawili kati ya saba ambao ni Japhet  Lomnyaki (25) mkazi wa Sakina na Nehemia Kweka (34) mkazi wa Ngaramtoni walifikishwa mahakamani juzi.

Huku Adam Mussa (30) mkazi wa Majengo, Tito Loomoni (25) mkazi wa Shamsi, Joseph Loomoni (29) mkazi wa Shamsi, Abdallah Maglan (202) mkazi wa Oldadai na Emmanuel Maglan (23)  mkazi wa Oldadai wakiwa wanaendelea kuhojiwa na polisi.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad