Mwimbaji Rose Muhando Aburuzwa Polisi Kwa Utapeli

MWANAMUZIKI wa nyimbo za Injili nchini, Rose Muhando anasakwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Kijitonyama ‘Mabatini’ jijini Dar baada ya mchungaji mmoja wa Kinigeria anayefanya shughuli zake nchini DR Congo,  Kabagambe Tchanda kumshitaki akidai kumlipa fedha ili akafanye onesho badala yake akaingia mitini.

Uchunguzi uliofanywa na Uwazi ndani ya jeshi hilo, umegundua kuwa kuna madai hayo na kwamba mchungaji huyo alitua jijini Dar na kufanya mazungumzo na Rose kwa ajili ya kwenda kutumbuiza nchini DR Congo, Julai mwaka huu katika mkutano uliohusisha wageni kutoka Ulaya na kukubaliana amlipe Dola za Marekani 5,000 (zaidi ya shilingi milioni 8).

Kwa mujibu wa chanzo, ilidaiwa kuwa mchungaji huyo alimkabidhi Rose dola 1,900 kama utangulizi na kubaki dola 3,100 ambazo angemlipa baada ya onesho. Makabidhiano hayo yalifanyika Magomeni ya Mwembechai jijini Dar.

Kutokana na sekeseke hilo, mwandishi wetu alimsaka mchungaji huyo na alipoulizwa kuhusu kuwepo kwa madai hayo, alikiri na kusema alimuamini sana Rose lakini cha ajabu mambo yamekuwa tofauti kwa kuwa hakufika kwenye tamasha.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. icho kiatu kivueeeee

    ReplyDelete
  2. Hahahaaaa....kiatu cha utapeli,kivueeer

    ReplyDelete
  3. Aaaa! Jaman! facebook facebook nini tena? unaharibu wewe si mtumish wa mungu?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad